BUNGE hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linasisitiza kwamba, kama ambavyo siku zote limejiepusha na migongano kati yake na Mahakama kwa kuweka kanuni hiyo (subjudice rule) chini ya Kanuni ya 64 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la 2007, Mahakama nazo lazima ziwe makini katika kuepuka kutoa hukumu au matamshi ambayo, kwa dhahiri kabisa, yanasababisha mgongano kati ya Mahakama na Bunge