All posts by Ahmed Rajab

Ibrahim Noor: Msanii anayeutetea Uswahili

PROFESA Ibrahim Noor Sharif Albakry ni msomi, msanii, na mwandishi mwenye sifa nyingi. Wengi wanamjua kwa majina yake mawili ya mwanzo na kwa vitabu vyake kadhaa kuhusu lugha na utamaduni wa Kiswahili pamoja na maandishi yake ya historia na siasa.  Mwandishi hupata taabu anapojaribu kuandika

Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu

SIJUI kwa nini hasa, ingawa nina hakika sababu ninazo, lakini tangu juzi akili yangu imetekwa na ndege na kasisi.  Imekuwa ikivutwa na kuvutiwa na viumbe hivyo. Nimekuwa nikiufikiria ujanja wa ndege na nikiyakumbuka maneno ya Martin Niemöller, kasisi wa Kijerumani aliyepata umaarufu katika zama za

Hizi siasa si mchezo wa karata

SAFARI moja Mei 2001, Marehemu Kanali Muammar Qadhafi, kiongozi wa Libya wa wakati huo,  alikuwa Uganda kwa ziara ya siku nne.  Alipokuwa huko alisema maneno ya kumshajiisha mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni asistaafu 2006 kama alivyotakiwa afanye kwa mujibu wa Katiba ya nchi yake ya

“Njaa mwana malegeza, shibe mwana malevya”

SINA tena haja ya kushawishiwa.  Sasa ninaamini kwamba ni kweli baadhi ya viongozi wetu ni miongoni mwa wale wanaotajwa kwenye Qur’ani kuwa ni “summun, bukmun, umyun” (wasiosikia, wasiosema na wasioona).  Qur’ani inaendelea kuwaelezea kuwa hawatoweza tena kurudi katika njia iliyonyoka. Kwa ufupi, wameangamia. Tunapowaangalia na

Kama si leo kesho, Jammeh yuko njiani

WASILI Banjul, mji mkuu wa Gambia, halafu panda gari. Fanya kama unakwenda mji wa Serrekunda kupitia barabara kuu ya kuelekea huko.  Mwendo wa kama dakika sita hivi utaona mahala palipozungukwa na kuta nene na refu. Pamekaa kama kambi. Rais Yahya Jammeh anasema kuwa hiyo ni

Historia itatuhukumu na kutulaani

HISTORIA ni nzito. Tukiingia 2017 tunaiona yetu sisi kuwa ni zigo kubwa la dhambi za watawala wetu pamoja na zetu wenye kuwaachia watawala wafanye wayafanyayo. Tunawaachia wajifanyie watakavyo kwa sababu, kama walivyo watawala na sisi pia, hatuna uadilifu.   Tunayaona makosa yanayotendwa na watawala, tunaona

Trump anao wa kumnusuru Afrika

USO wake wa duara umejazajaza na nyuma ya miwani yake kuna macho yanayokuangalia kana kwamba yanakuchuja. Ni mfupi na ana mwili tipwatipwa. Akipiga suti na akavaa tai yake ya shingoni (bow) yake huenda ukamdhania kuwa ni mfanyabiashara wa Kichina aliyeloa utamaduni wa kizungu.  Hiyo ndiyo

Aliyoyaona Fidel Castro alipozuru Afrika

WIKI iliyopita tuligusia kuwa Jumapili Aprili 3, mwaka 1977 Fidel Castro, wakati huo akiwa Rais wa Cuba, alikutana kwa mazungumzo jijini Berlin ya Mashariki na Erich Honecker aliyekuwa kiongozi wa Kikomunisti wa nchi ambayo siku hizi si nchi tena, Ujerumani ya Mashariki.   Mkutano wenyewe