All posts by Christopher Gamaina

Ofisi ya madini Mwanza taabani

OFISI ya Madini Mkoa wa Mwanza inakabiliwa na ukata hivyo kujikuta inadaiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) deni la pango la nyumba linalofikia Sh milioni 70 kwa sasa. Taarifa ya ofisi hiyo iliyowasilishwa kwenye kikao cha wajumbe wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Mwanza

Chai yachochea wazee kufurika kupata matibabu

HUDUMA ya chai na vitafunwa imetajwa kuongeza mahudhurio ya wazee wanaokwenda kutafuta matibabu katika Kituo cha Afya Kahangala wilayani Magu, Mwanza kutoka watano kwa siku mwaka 2014 hadi 20 mwaka huu. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho cha Serikali, Joyce

Shoka kali kwa wavuvi haramu Buchosa

SIKU chache baada ya Raia Mwema kuripoti ukubwa wa tatizo la uvuvi haramu katika Ziwa Victoria, Serikali wilayani Sengerema, Mwanza imekunjua makucha kwa kukamata tani 12 za samaki wachanga wenye thamani ya Sh milioni 72. Samaki hao aina ya sangara wenye urefu wa chini ya

Wadau wapendekeza sumu ya uvuvi haramu

Sengerema, Mwanza WADAU wa uvuvi wamependekeza mbinu mpya zinazoweza kukomesha uvuvi haramu unaotishia kukomboa samaki katika Ziwa Victoria, kuathiri uchumi na ajira mkoani Mwanza. Miongoni mwa wadau hao ni Shirika la Umoja wa Wavuvi (FUO) linalopendekeza mambo 10 yanayoweza kumaliza tatizo hilo, kuwezesha ongezeko la

Watahadharishwa juu ya matumizi holela ya maji

Mwanza, Tanzania BODI ya Maji Bonde la Ziwa Victoria (LVBWB) imesisitiza matumizi ya kisheria ya maji, vinginevyo ni kukaribisha migogoro ya maji na kuhatarisha maisha ya watu, wanyama, mimea na viumbe hai wengine. Imetaja matumizi sahihi kuwa ni yanayozingatia Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za

Mwenge ulivyomulika mradi wa maji Mwanza

USEMI wa ‘mgeni njoo mwenyeji apone’ umedhihirika jijini Mwanza Jumapili iliyopita, pale kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu, Amour Hamad Amour, alipozindua mradi wa maji ya bomba wa Fumagila kwa uangalizi. Awali, taarifa iliyowasilishwa kwake wakati wa mapokezi ya mwenge huo

No Thumbnail

Shule ya Mennonite haijasajiliwa Ilemela

NA MWANDISHI WETU SHULE ya Msingi Mennonite ya mchepuo wa Kiingereza iliyopo Nyakato Sokoni, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Mwanza haijasajiliwa serikalini, Raia Mwema limebaini. Shule hiyo inamilikiwa na Kanisa la Mennonite Ilemela. Ilianzishwa mwaka 2014, kwa sasa inahudumia wanafunzi 400 wa darasa la kwanza

Kiwanda cha Fu Hua Mwanza chachafua Ziwa Victoria

NA CHRISTOPHER GAMAINA, MWANZA KIWANDA cha mifuko ya plastiki kijulikanacho kwa jina la Fu Hua cha jijini Mwanza, kinamwaga maji machafu katika Ziwa Victoria kupitia mto Mirongo, Raia Mwema limethibitisha. Hali hiyo, licha ya kukaidi Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Namba 20 ya Mwaka 2004,