All posts by Deusdedith Kahangwa

Mrejesho wa wasomaji juu ya makala ‘Afrika, uchawi na maswali magumu ya Padre Ngowi’

KATIKA makala iliyopita, nilipendekeza kwamba, changamoto ya uchawi Afrika inapaswa kutatuliwa kwa kuuliza na kujibu maswali magumu, katika namna ambayo itaporomosha imani potofu tulizonazo. Kimsingi, nilipendekeza kutumia hoja za kiteolojia, kisayansi na kifalsafa kuyakosoa mafundisho kadhaa kama tunayoyapata kutoka kwa baadhi ya wanateolojia na wanafalsafa.

Wasemayo wanateolojia, wanafalsafa na wanasayansi

HIVI karibuni, Padre Ngowi ameuliza, "Afrika na uchawi: Hatujui kuuliza maswali magumu?" Aliuliza swali hili kupitia ukurasa wa tisa wa toleo namba 480 la gazeti hili. Ameendeleza hoja yake katika matoleo kadhaa yaliyofuata. Akiandika katika muktadha wa kihistoria, Ngowi amejadili "uhusiano baina ya sayansi, dini