All posts by Ezekiel Kamwaga

Tunahitaji baraka kwelikweli, la sivyo twafa!

MCHANA mmoja wa mwaka 1999, marais watatu mashuhuri wa Afrika wakati huo, Thabo Mbeki (Afrika Kusini), Olusegun Obasanjo (Nigeria) na Abdelaziz Bouteflika (Algeria); walipatwa na aibu ambayo hawakuitarajia. Walikuwa wamealikwa kuhudhuria mojapowa ya mikutano ya mataifa tajiri duniani (G8) uliokuwa ukifanyika nchini Japan. Mbeki alialikwa

Ningemwambia Magufuli aniepushe na kikombe hicho

MARA baada ya Jaji Themistocles Kaijage kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC); niliamua kuuliza kidogo kwa watu waliomfahamu kuhusu wasifu wake. Niliambiwa kwamba ni mtu makini, muungwana na anayefuata maadili. Mmoja wa wanasheria mahiri hapa nchini aliniambia kwamba alidhani huyu ni

Watajwa kumrithi Jaji Mkuu Chande

JAJI Mkuu wa Tanzania, Chande Othman (65),  anatarajiwa kustaafu mwezi huu na tayari majina matano yanatajwa kuweza kurithi nafasi hiyo, Raia Mwema limeambiwa. Jaji Othman anastaafu baada ya kuwa ameitumikia nafasi hiyo kwa takribani miaka sita; kuanzia Desemba 26, mwaka 2010, wakati alipoteuliwa kuchukua nafasi

Ninavyousoma mchezo wa Shinzo Abe

DESEMBA 26 mwaka jana, nilimuona kwenye televisheni Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, akiweka shada la maua katika bandari ya Pearl, kule Hawaii, Marekani, ambako marubani wa jeshi la Japan walijilipua kwa staili ya Kamikaze, mwishoni mwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Ziara ya

Vita ikitokea kesho, tutanunua nyama mabuchani?

SASA ni wazi kwamba Tanzania imepania kujitosa kindakindaki kwenye uchumi wa viwanda. Ahadi hii ya serikali ya Rais John Magufuli ni maarufu kiasi kwamba ifikapo mwaka 2020, ni wazi mojawapo ya hoja zitakazozungumzwa sana itakuwa ni kwa kiasi gani hili limetimizwa. Mimi ni miongoni mwa

Mwijage: Waziri anayehubiri mafanikio kabla ya ushahidi

TAKRIBANI mara tatu katika maisha yake ya utu uzima, Charles John Mwijage, ametumika kama Meneja Masoko wa kampuni tofauti katika sekta ya mafuta. Alikuwa Ofisa Masoko wa Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kati ya mwaka 1991 hadi 1993, akawa tena Ofisa Masoko

Natamani Kiba na Diamond wasipatane

KAMA wewe ni shabiki wa muziki wa kizazi kipya, ni lazima utakuwa unafahamu kuhusu miamba miwili inayotamba hapa nchini hivi sasa; Diamond na Ali Kiba. Kwa sasa, hawa ndiyo mabalozi wakubwa zaidi wa muziki wa Tanzania. Bila wao, pengine leo tungekuwa tunazungumza mengine kuhusu muziki

Barongo : TPDC ilianza na mimi, peke yangu

MWEZI Julai mwaka 1973, Sylvester Barongo (76), wakati huo angali kijana mdogo wa umri wa miaka 33 tu, aliteuliwa kuwa Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli (TPDC). Kazi yake kubwa aliyotakiwa kufanya ilikuwa ni kutengeneza taasisi kinara katika eneo