All posts by Richard Mabala

MB akakunja mikono, akakunja uso, kidogo akunje ngumi nakuambia

Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke, Uzitoni Street, Bongo. Frank mpenzi wangu, UNAENDELEAJE mpenzi wangu?  Uko mzima kweli?  Nakuomba sana ujihadhari sana usije ukapatwa na majanga ya jumla.  Nisingependa kabisa kukuchangia pale hospitalini kumbe mchango wangu unatumika kuchimba vyoo vya shule fulani.   Yaani mwenzangu?  Tangu

Ama kwa hofu, ama kwa hila, ama kwa hongo

Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke, Uzitoni Street, Bongo. Mpenzi Frank, Mzima mpenzi wangu? Mimi ni mzima kabisa, hasa baada ya kupata barua yako.  Nakuambia kila nikipata barua yako pepe, inafutadiliti mapepe ya wasiwasi na kujaza mapepe ya furaha kama si upupu.  Tena siku hizi,

Ama kweli kazi ya upambe ni nuksi. Nuksi kwa mpambe mwenyewe

Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke, Uzitoni Street, Bongo. Mpenzi Frank, Vipi huko mwenzangu?  Kweli mnakumbwa na matukio ya ajabu kila siku kama hapa.  Zamani nilipenda kukaa mjini lakini haya maisha ya mwendokasi yananishinda.  Duh!  Waziri mzima, mara kulindwa, mara kulengwa.  Mwimbaji na wimbo wake

Unaweza kumkingia mtu kifua kumbe atakutokea puani

Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke, Uzitoni Street, Bongo. Habari za huko mpenzi wangu wa moyo? Nina imani kwamba una amani huko licha ya mihangaiko ya kutafuta shilingi zilizojificha.  Angalau afadhali huko maana naamini mawimbi ya matingisho ya Dar yanawafikia kidogo tu.  Yaani.  Wiki hii

Sera ya nini? La muhimu ni sura

Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke, Uzitoni Street, Bongo. Frank wangu, Yaani ninavyokumiss mwenzangu!  Natamani kuja kununua vitu kwenye kioski chako kila baada ya saa moja niweze kukuona kila wakati.   Wewe ni dhahabu ndani ya mgodi wangu na dhahabu isipoonekana, linalobaki ni shimo kubwa chafu