All posts by Elias Mhegera

Wadau sekta ya elimu washauri mabadiliko yasifanyike kwa kasi kubwa

WADAU katika sekta ya elimu wameishauri serikali isifanye mabadiliko ya mara kwa mara katika mfumo kwani kwa kufanya hivyo inaweza kuwakanganya walimu na hata wanafunzi pia. Ushauri huo ulitolewa katika mjadala ulioandaliwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Konrad Adenaeur Stiftung (KAS) kutoka Ujerumani na

Wadau washinikiza sera za kilimo sasa zifanyiwe kazi

WATAALAMU wa kilimo na wadau wengine wameshauri kwamba serikali ianze kutekeleza kikamilifu zaidi maazimio na sera zake za kukiendeleza kilimo ili kitoe mchango stahiki kwa pato la taifa. Msisitizo huo ulitokana na mjadala juu ya mchango wa kilimo katika maendeleo ya nchi kwa ujumla katika

Ada elekezi: Mchango wa sekta binafsi elimu uthaminiwe

NIMEUSIKIA mvutano unaoendelea chini kwa chini kati ya Serikali na shule binafsi hususani katika suala la ulipaji wa ada. Nimejipa muda wa kufanya mahojiano na sehemu kadhaa za mvutano huu na mahojiano hayo ndiyo yamezaa makala hii. Kimsingi Serikali ya Tanzania inao wajibu wa kusimamia

Migogoro ya ardhi itafutiwe ufumbuzi wa kudumu

KWA sasa imekuwa kama vile ni wimbo wa taifa kusikia migogoro ya wakulima na wafugaji wakigombea ardhi. Hata hivyo huo ni mmoja tu kati ya migogoro mingi inayohusiana na ardhi. Nchini Tanzania kumekuwapo na migogoro mingi hususani katika kugombea maeneo ya kilimo, malisho ya wanyama,

Uchumi wa dunia unalazimisha muungano wa Afrika

MIONGONI mwa mambo yanayolikwamisha Bara la Afrika kufikia maendeleo stahiki ni kukosekana kwa umoja. Wiki iliyopita nilizungumzia dhana hii ndani ya nchi moja ya Kenya leo nataka niende mbele zaidi kati ya nchi na nchi. Ninarejea kuchota uzoefu wa China ili kuiwasilisha mada hii kwa

Masumbwi ya wabunge Kenya na hatima ya Umoja wa Afrika

NIMELAZIMIKA kuandika makala inayohusu yaliyojiri bungeni Kenya kwa sababu mambo ya aina hiyo na mengine yenye kufanana nayo yana mwangwi mkubwa juu ya hatima ya Umoja wa Afrika. Nimekifuatilia kisa hiki katika vyombo vya habari na hata kwenye mitandao ya jamii, na huu ni ushahidi

Tupate funzo kutoka Sichuan kuhusu tetemeko la Kagera

HIVI karibuni nikiwa bado nje ya nchi nilisoma katika mitandao ya jamii malalamiko juu ya matumizi ya pesa za misaada kwa waathirika wa tetemeko la Kagera. Katika hali ya utani wengi wakasema kwamba uamuzi wa serikali kwamba pesa za michango zitatumika kwa ajili ya ujenzi

Tukiondoa hofu tutapata busara!

MWANADAMU katika kila kizazi hutawaliwa na uelewa wa kiwango fulani ambao ama huupata kutokana na mazingira aliyomo, mapokeo au hata mfumo wa elimu uliopo katika jamii yake. Kwa nchi zetu za Kiafrika jambo hilo limekuwa na athari kubwa mbili: kwanza, wapo wale ambao wana hofu