All posts by Joseph Mihangwa

Mfalme akitinga utupu hadharani, ni uhaini kutosema yuko uchi

HAIKUWA kwa bahati mbaya wala kutotarajiwa, bali kwa stahiki yake na haki; pale mheshimiwa Mikogo Mingi, mwana wa Mfalme Mingi Mikwara, aliposhika kiti cha ufalme kumrithi baba yake aliyeitwa na Mungu katikati ya mwezi Machi mwaka huo. Mfalme huyo kijana ambaye kabla ya hapo hakujisumbua

Je, Magufuli ataweza kutawala kwa ujasiri bila kuitwa dikteta?

“Kosa la mtu mdogo, kutangazwa si muhimu Hasara yake kidogo, kama la mwendawazimu. Kosa la mtu mkubwa, wajibu kulitangaza Kwa herufi kubwa kubwa, na wino wa kuangaza   Mdogo hatendi jambo, dunia lenye kimo Kulitangaza uchimbo, makubwa yakiwa yamo. Dunia huharibiwa kwa makosa ya mkubwa

Haya ndiyo ya Vatican ya Kiingereza na Zanzibar ya Muungano

KUNA mkanganyiko wa kutoelewa mambo kuhusu uhusiano wa kimataifa wa Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani na Mkuu wa nchi ndogo kuliko zote duniani, iitwayo “Vatican”.  Mkanganyiko huo huja wakati mkuu huyo anayefahamika kwa jina la ukuu wa kikanisa kama (Baba Mtakatifu) “Papa”, na nchi huru

Ukweli gani Azimio la Zanzibar liliua Azimio la Arusha? [2]

KUZUNGUMZIA “Ujamaa” siku hizi ni kukubali kuitwa mwendawazimu.  Hii ni kwa sababu watu wengi wanaamini kwamba Ujamaa na Siasa ya Kujitegemea vilikufa kufuatia Azimio la Zanzibar la mwaka 1992 lililofungua milango kwa sera za uchumi wa soko huria na vyama vingi vya siasa Vivyo hivyo,

Mgomo wa wasomi JKT ulizaa Azimio la Arusha?

FEBRUARI 5, mwaka huu, Watanzania wameadhimisha miaka 50 ya Azimio la Arusha ambalo ni mwongozo wa sera za Uchumi na Maendeleo ya nchi yetu. Haya yakiendelea, inawezekana, watu wengi na hasa wa kizazi hiki cha chini ya umri wa miaka 50, hawaelewi vyema chimbuko la

Uhuru wa siasa kwanza au uchumi kwa maendeleo? (2)

KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya, tulijadili dhana ya uhuru wa siasa na uhuru wa uchumi katika maendeleo kuona kipi kitangulie kwa ustawi wa nchi. Tulijadili pia dhana ya uchumi wa soko huria kuona kama ni sahihi kwa serikali kujiondoa katika jukumu la kupanga