All posts by Mwandishi Wetu

Mkutano wa Nape waota mbawa

KAMANDA wa Polisi Kanda ya Kinondoni amepiga marufuku kufanyika kwa mkutano na wanahabari uliopangwa kufanywa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Nape Nnauye katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam. Meneja wa Hoteli hiyo, Selemani Nasao, aliwaambia waandishi wa habari waliofurika

Namna ANC na DA vinavyowawajibisha wanachama wao

HELEN Zille ni jina maarufu hapa Afrika Kusini sawa na akina Freeman Mbowe, Tundu Lissu, Halima Mdee au wengineo maarufu katika kambi ya upinzani nchini Tanzania. Kwa muda wa miaka nane tangu Mei 2007 hadi Mei 2015, Zille alikuwa ndiye kiongozi mkuu wa chama kikuu

Natamani neema za SAGCOT zifike Kilimanjaro

HIVI majuzi nilitembelea mikoa ya Njombe na Iringa ambako nilifurahi mno kuona jinsi familia za huko zimeanza kubuni miradi ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa, na tayari mifugo hiyo imeanza kuwapatia kipato cha uhakika. Shujaaa wangu  huko alikuwa ni mama mmoja anayejulikana kwa jina la

Sayansi ya kuendesha nchi, ulaghai na ujuaji wetu

NDUGU msomaji natumaini si mara ya kwanza kusikia neno ulaghai au ujuaji, haya ni maneno tuliyoyazoea. Lakini sina hakika ni mara ngapi umesikia neno “sayansi ya kuendesha nchi” kwani hata mimi ni mara yangu ya kwanza kuliandika. Hii haimaanishi kuwa sikijui ninachotaka kukiandika, la hasha

Utata Jaji Mkuu

HATUA ya Rais John Magufuli kumteua Profesa Ibrahim Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania imeibua utata kuhusu dhamira yake kwenye kufanya hivyo, Raia Mwema limeambiwa. Tangu Uhuru wa Tanganyika, hakuna Rais aliyewahi kumteua mtu kuwa Kaimu Jaji Mkuu; baada ya Jaji Mkuu aliyekuwepo madarakani

Kizungumkuti cha Magufuli

KWA mara nyingine, Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa mtata  wa Dar es Salaam, amekwepa panga la Rais John Magufuli, ambalo limeangukia watumishi na viongozi wa serikali wengi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Hata hivyo, hatua hiyo imezua maswali kuhusu namna Rais Magufuli anavyowatenda tofauti

Magufuli: Ruksa kuoana bila cheti cha kuzaliwa

RAIS John Magufuli leo amefuta agizo la Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe, la kutaka wanandoa wawe kwanza na cheti cha kuzaliwa kabla ya kuoana. Akizungumza na wandishi wa habari katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Magufuli alisema kwa sasa idadi ya Watanzania