All posts by Paul Sarwatt

Waandishi Arusha wamgomea Waziri Lukuvi

22/12/2016 –  WAANDISHI wa habari Mkoa wa Arusha leo wamegoma kuripoti ziara ya  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi baada ya kukamatwa kwa mwandishi wa kituo cha televisheni cha ITV, Halfan Lihundi. Lihundi ambaye huripoti ITV kutokea Arusha, alikamatwa jana na polisi kupitia amri ya Mkuu wa

Mgogoro wa ushirika Moshi wapanda joto

Moshi, Kilimanjaro MGOGORO ulioibuka katika Ushirika wa Mema na Mabaya unaoundwa na watumishi  wa Idara ya Kilimo na Mifugo katika Manispaa ya Moshi na Halmashauri ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro umepanuka zaidi baada ya wanachama kuwataka Wakurugenzi wa Halmashauri hizo kusitisha mara moja  makato ya fedha za michango katika

Vijana CCM Babati wakiri kucheza rafu

BABATI, MANYARA WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Babati  ‘wameungama’ kwa viongozi wa wilaya hiyo wakisema walitumika kwa kulipwa fedha ili kuchochea mgogoro wa muda mrefu ndani ya chama hicho baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka jana. Viongozi wa

Saccos ya idara ya kilimo Moshi washitukia ufisadi

MOSHI WANACHAMA wa Ushirika wa Mema na Mabaya unaoundwa na watumishi wa Idara ya Kilimo na Mifugo katika Manispaa ya Moshi na Halmashauri ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro wameulalamikia uongozi wa chama hicho kwa kushindwa kuwahudumia kwa mujibu wa katiba yao. Ushirika huo ulianzishwa mwaka

Chuo chazoa ada bila usajili

WANAFUNZI zaidi ya 140 wa chuo binafsi cha Rians Institute of Professional  Studies kilichopo eneo la Usa-river wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha wamerudishwa nyumbani baada ya chuo kubainika kutosajiliwa. Chuo hicho kilikuwa kikitoa kozi za ngazi ya cheti katika masomo ya ualimu wa awali kwa watoto wadogo (chekechea),

Zaidi ya milioni 100/- zachotwa kifisadi

HALMASHAURI ya Jiji la Arusha imepoteza kiasi cha shilingi 104,985,900 baada kuvikopesha vikundi hewa vya vijana na wanawake kati ya mwaka 2009-2016. Upotevu wa fedha hizo uko katika taarifa ya kamati ndogo ya Madiwani wa Jiji la Arusha iliyochunguza ufutaji wa madeni ya pamoja na