Hifadhi: Burudani & Michezo

No Thumbnail

Simba, Yanga bado hazijasajili

WACHEZAJI wa timu za soka za Simba, Yanga bado wanaendelea kuuza kurasa za mbele za magazeti ya michezo nchini. Na wanauza kweli kweli. Wasomaji wanapenda kuona picha za mastaa wao zikikaa kurasa za mbele, huku wahariri wa magazeti hayo wakitumia umahiri huo kunogesha taarifa ili

Yanga na maisha yasio rasmi kwao

KILA hatua ya mbele na nyuma wanayoipiga watu wa klau ya soka ya Yanga wakati huu, namkumbuka Yussuph Mahboub Manji. Ni Manji aliyewafanya watu hao wajihisi wanaishi kwenye sayari yao isiyoguswa na kiumbe kingine. Ni Manji aliyekuwa akitoa furaha nyusoni mwao. Ni Manji aliyekuwa na

Sioni Malinzi akishindwa Uchaguzi Mkuu TFF

NATAMANI Rais Jamal Malinzi ashindwe Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utakaofanyika Agosti 12. Sababu yangu ni moja na nyepesi tu. Nayo ni kwama mpira wetu haujawahi kuwa na mafanikio makubwa, lakini chini ya Malinzi umerudi nyuma badala ya kwenda mbele. Hii ndiyo

Stori za Wakenya na Derby ya ‘Mashemeji’

MCHEZO wa fainali ya michuano ya Super Cup iliyokutanisha timu za Gor Mahia na AFC Leopard za Kenya, zimeleta jina jipya kwenye soka la Tanzania. Timu hizo kila zinapokutana mchezo huo huitwa “Mashemeji Derby”. Kwa asili, klabu ya Gor Mahia huhusishwa na kabila la Wajaluo

Tunahitaji akili kuwaelewa Azam, sio ‘mapovu’

VIONGOZI wa klabu ya Azam kwa akili zao timamu bila kushawishiwa na yeyote yule wameamua kuja na sera ya kupunguza matumizi yasiyokuwa na ulazima klabuni mwao. Hawajaishia kupunguza matumizi tu, wameamua kupunguzana na wao wenyewe. Inahitaji zaidi ya akili kuwaelewa Azam kwa hiki wanachokifanya sasa.

Ajib anatushangaa tunavyomshangaa

NILISAFIRI basi moja na mchezaji wa Simba Ibrahim Ajib kutoka Dodoma kulikokuwa na mchezo wa timu yake dhidi ya Mbao hadi Dar es Salaam. Muda mrefu ndani ya viti tulivyokuwa tumekaa tulizungumza masuala mengi ya kimaisha. Tulizungumzia kuhusu maisha ya soka na nje ya soka.

Ukosefu wa umakini unaathiri ngumi Tanzania

KANDO ya mchezo wa soka nchini, inatajwa mchezo wa ngumi ndiyo wenye watazamaji wengi. Ngumi zinapendwa, lakini watu walioko ndani ya mchezo wenyewe hawajui thamani ya mchezo wao, ndiyo maana kila kukicha kuna ‘sinema’ nyingi ndani ya mchezo huo. Ni kitu cha kawaida kuwashuhudia wacheza

Nyota Serengeti Boys amtoa machozi mamaye

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mama wa mshambuliaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), Yohana Nkomola, amemtoa machozi  mama yake mzazi, Neema Nkomola, baada ya kumuona kwenye luninga akiiwakilisha Tanzania kwenye mechi ya Tanzania dhidi ya Mali.