Hifadhi: Tahariri

Hongera Magufuli, TRA wamekusikia

MACHI 19, Jumatatu ya wiki hii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli alikutana na Baraza la Wafanyabiashara Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam. Mengi yamejiri katika mkutano huo. Wafanyabiashara mbalimbali waliohudhuria mkutano husika walipata fursa ya kuzungumza kwa uhuru, pamoja na

Tuje na mtazamo mpya kuhusu rushwa barabarani, adhabu

KUNA mambo hayajakaa sawa. Kiasi cha wiki moja iliyopita zilisambaa taarifa ya kuwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) inakusudia kuweka maofisa wake barabarani kuwabaini madereva watoa rushwa kwa askari wa Usalama wa Barabara. Bila shaka hatua hiyo ya Takukuru imechagizwa na malalamiko mengi

No Thumbnail

Matamko haya yatekelezwe kwa vitendo kuboresha Pamba

HIVI karibuni serikali imetangaza mpango mkakati wake wa kuboresha kilimo cha Pamba kukifanya kiwe chenye tija kwa wakulima, wanunuzi na Taifa kwa jumla. Dhamira hiyo ya serikali ilitangazwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, katika mkutano na wadau wa Pamba jijini Mwanza, akitoa maelekezo mbalimbali ya

No Thumbnail

Tunapoanza upya tuitazame pia mikataba

TUMESHUHUDIA mara kadhaa malalamiko dhidi ya wataalamu wetu  walioshiriki kuandaa mikataba mbalimbali ya uwekezaji isiyo na tija. Na hawa ni wale ambao Taifa hili limevuja jasho jingi kuwafikisha hapo walipo katika vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi. Hatutaki kutaja majina ya vyuo, lakini

Bora tumeanza kuiepuka aibu hii!

MWISHONI mwa wiki iliyopita, mitandao ya jamii ilisheheni habari kuhusu namna viongozi wa nchi masikini kutoka Afrika wanavyovuja fedha za umma wakati wa mikutano ya kimataifa. Taarifa hizo zilikusanywa wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) uliofanyika New York, Marekani, wiki iliyopita na

Spika, wabunge wawe kitu kimoja

MKUTANO wa Nane wa Bunge la 11 umemalizika mjini Dodoma wiki iliyopita huku ukiwa umetawaliwa na matukio ya nje ya ukumbi huo kuliko yale yaliyotokea ndani ya ukumbi huo. Ni matukio ambayo yameacha alama ambayo huenda isifutike katika historia ya mhimili huo wa dola. Kubwa

Kwa hili la Lissu haki itendeke na ionekana kuwa imetendeka

WIKI iliyopita, taifa letu liliingia katika rekodi mbaya miongoni mwa jamii ya kimataifa kutokana na tukio la kupigwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Tundu Lissu. Pasipo kupapasa maneno, tukio lile limeitia aibu nchi yetu ambayo imekuwa