Hifadhi: Afrika

Mchungaji nchini Zimbabwe akamatwa kwa kutabiri kifo cha Mugabe

HARARE, ZIMBABWE POLISI wa Zimbabwe jana tarehe 16 Januari 2017 walimweka kizuizini mchungaji ambaye anadai kwamba kiongozi wa muda mrefu Rais Robert Mugabe, ambaye atafikisha umri wa miaka 93 mwezi ujao, atafariki mwezi Oktoba, mwanasheria wake alisema. Gift Mtisi alisema mchungaji Patrick Mugadza alikamatwa katika

Jacob Zuma: Msiitembelee Israel

RAIS wa Afrika Kusin Jacob Zuma amewataka raia wan chi yake kuacha kuitembelea Israeli ili kuonyesha kuwaunga mkono “watu wa Palestina,” mtandao wa Africa News umesema Jumapili. Matamshi ya Zuma yamekuja katika kumbukumbu ya miaka 105 ya chama kinachotawala cha African National Congress ANC, ambapo

Waziri wa Ulinzi wa Ivory Coast aachiwa huru na askari waasi

ASKARI waliogoma huko Ivory Coast wamemuachia huru Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo baada ya kumshikilia kwa masaa mawili katika mgomo juu ya malipo. Alain Richard Donwahi alishikiliwa katika mji wa Bouake na wanajeshi ambao walikataa masharti yaliyotangazwa na Rais Allassane Quattara. Quattara alisema alikuwa

Rais wa DRC Joseph Kabila: mwanamageuzi au dikteta

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila, hivi karibuni ameonyesha matumaini madogo ya kuwepo kwa amani zaidi ya kueneza wasiwasi wa kuwepo kwa machafuko mapya nchini humo. Kabila alikataa kuachia ngazi mapema mwezi Desemba baada ya muhula wake madarakani kumalizika kwa kusema

Mugabe aacha hali tete Zimbabwe aenda mapumzikoni nje ya nchi

HARARE, ZIMBABWE WAKATI Zimbabwe ikitajwa kuwa katika wakati mgumu kiuchumi kiasi cha kushindwa kulipa mishahara watumishi wa serikali, Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo, akiwa na msafara mkubwa, amekwenda kujipumzisha nje ya nchi hiyo.  Mugabe na familia yake, pamoja na msafara uliohusisha kundi la wasaidizi