Hifadhi: Kanda ya Ziwa

Chungu, tamu ziara ya JPM Simiyu, Shinyanga

WIKI iliyopita Rais Dk. John Pombe Magufuli (JPM) alifanya ziara katika mikoa ya Simiyu na Shinyanga ambako alionekana kivutio kutokana na kauli zake mbalimbali, baadhi zikiwa tamu na nyingine chungu kwa viongozi na wakazi wa mikoa hiyo. Ilishuhudiwa akipata mapokezi makubwa ya watu katika maeneo

Kiwanda cha Nyakato chahatarisha afya

WAKAZI wa Nyakato wilayani Ilemela, Mwanza wako katika hatari ya kuathiriwa afya kutokana na moshi unaofuka kutoka kiwanda cha kutengeneza nondo cha Nyakato Steel Limited. Kiwanda hicho kinadaiwa kukiuka maelekezo ya kitaalamu yanayohimiza udhibiti wa moshi wakati wa uzalishaji wa nondo, hali inayosababisha uchafuzi wa

Mali za NCU kurejeshwa mwezi huu

HATIMAYE mali za Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza – NCU (1984) Ltd zilizouzwa kinyemela na kwa bei ya kutupa zinatarajiwa kuanza kurejeshwa na kufidiwa mwezi huu, Raia Mwema limeelezwa. Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli linalolenga kusisimua uchumi wa

Wanafunzi hewa kuwang’oa vigogo Mwanza

HOFU imetanda miongoni mwa vigogo wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutokana na kuvuja kwa taarifa za kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria waliohusika kughushi takwimu za wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Kuna taarifa kwamba watumishi wa jiji hilo wanaojijua walihusika katika mchezo

Milioni 87/- zahofiwa kuliwa kifisadi

WINGU kubwa limetanda juu ya shilingi milioni 87 za Chama cha Ushirika cha Msingi cha Akiba na Mikopo cha Tubeamoi jijini Mwanza, zinazodaiwa kuchukuliwa na meneja wa chama hicho, Christian Ishengoma, bila kuainisha matumizi yake. Tuhuma hizo zimeibuliwa na Kamati ya Usimamizi ya Tubeamoi Saccos

Serikali yawageukia wenye maduka Mwanza

BAADA ya kufanikiwa kuwaondoa wafanyabiashara ndogo-ndogo (machinga) katikati ya Jiji la Mwanza wiki iliyopita, serikali sasa imewageukia wenye maduka kwa kuwapiga marufuku kuweka bidhaa zao kwenye baraza za maduka kama maonesho. Marufuku hiyo inayotajwa kuwa ni amri halali ya serikali, inawalenga pia wamiliki wa nyumba

Serikali, machinga Mwanza wapimana ubabe

KUNA kila dalili ya kuzuka vurugu kati ya vyombo vya dola na wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa jina la machinga jijini Mwanza ikiwa mamlaka za juu hazitaingilia kati mvutano mkubwa uliopo baina ya pande hizo mbili. Wakati viongozi wa serikali wa wilaya za Nyamagana na Ilemela