Hifadhi: Uchumi na Biashara

Biashara ya hisa za TBL yatawala soko

PAMOJA na kuwepo kwa biashara mpya ya toleo la hisa za awali (IPO) za kampuni ya Vodacom Tanzania, Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) limeendelea kuchangamka. Kwa kawaida biashara ya hisa za awali (IPO) huwa inavutia wawekezaji zaidi ya hisa ambazo zimeorodheshwa kwenye soko,

SIDO yafanikisha mradi wa kukuza ujasiriamali vijijini

MRADI wa Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini(MUVI) uliobuniwa na Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) umekuwa na mafanikio makubwa kwa upande wa Tanzania Bara. Hadi sasa baadhi ya wananchi kwenye mikoa saba wamefundishwa stadi za kutofautisha kati ya kilimo cha biashara na cha kujikimu. Mradi huu

Wawekezaji wa nje watawala soko la hisa

WAWEKEZAJI kutoka nje ya nchi wiki iliyopita walifurika kwa wingi kwenye soko la hisa la Dar es Salaam kununua hisa, hatua ilisababisha ukuaji mkubwa wa mauzo ikilinganishwa na wiki ya awali. Hatua hiyo ni muondelezo wa muda mrefu kwani ripoti za awali zimeonyesha kwamba wawekezaji

Hatari za uwekezaji kwenye soko la hisa?

MTU yeyote anapofikiria kuwekeza fedha zake sehemu yoyote ile ya kiuchumi, basi suala la faida huwa ni kitu cha kwanza kabisa kwenye fikra zake. Kwa kuwa faida ndiyo malengo ya biashara yoyote duniani, basi kila mtu anayewekeza huwa anapenda kuona fedha yake ikikua na kumletea

Hisa; Utajirisho usio na kificho

Wakati ananunua hisa za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) mwishoni mwa mwaka 1998, Zacharia Meshack, 51 (sio jina halisi) alikuwa na mpango wa kuziuza ndani ya kipindi kifupi kama walivyofanya wawekezaji wengine. Kitu cha kwanza alichofikiria wakati anawekeza ni kuwa pale bei ya hisa itakapopanda

Mauzo ya hisa yashuka DSE

Mauzo ya hisa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yalishuka hadi kufikia shilingi milioni 511 wiki iliyopita kutoka shilingi milioni 787 za wiki ya awali. Hata hivyo, pamoja na kushuka kwa kiasi cha mauzo, idadi ya hisa zilizonunuliwa katika kipindi cha wiki

Vilio na vicheko sekta ya benki

SEKTA ya benki nchini huenda ilikabiliwa na hali ngumu ya kibiashara kwenye robo ya mwisho ya mwaka jana, baada ya ripoti za benki mbalimbali kwenye kipindi hicho kuonyesha kupungua kwa amana za wateja, faida na mikopo kwenye sekta mbalimbali za uchumi. Hata hivyo, pamoja na