Jacob Zuma: Msiitembelee Israel

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

RAIS wa Afrika Kusin Jacob Zuma amewataka raia wan chi yake kuacha kuitembelea Israeli ili kuonyesha kuwaunga mkono “watu wa Palestina,” mtandao wa Africa News umesema Jumapili.

Matamshi ya Zuma yamekuja katika kumbukumbu ya miaka 105 ya chama kinachotawala cha African National Congress ANC, ambapo alirejea mshikamano na “watu wanaoonewa wa dunia,” na kuonyesha “Palestina” kama mfano.

“Watu wa Palestina wanaendelea kuteseka katika mapambano yao ya kutafuta kujiamulia mambo yao wenyewe … Tunarudia tena kwamba tunapinga safari kwenda Israel kwa sababu ambazo hazihusiani na kuendeleza amani katika eneo hilo,” Zuma alikaririwa akisema katika hotuba ambayo ilisikilizwa na maelfu ya wafuasi wa chama chake.

Zuma pia alisema chama chake kiliunga mkono azimio namba 2334 la Umoja wa Mataifa, ambalo lilipitishwa mwezi ulipita na Baraza la Usalama na ambalo linashutumu uwepo wa Israel huko Judea, Samaria, na ukanda wa Gaza. Aliwataka watu wa Palestina kuungana ili kufikia lengo lao, kulingana na mtandao wa Africa News.

Zuma na wanachama wengine wa chama chake wameendelea kutoa matamshi dhidi ya Israel katika miaka ya hivi karibuni.

Serikali nchini humo imekuwa ikiishutumu Israel mara kwa mara kwa kutekeleza sera za “kibaguzi” dhidi ya Waarabu wa Palestina. Mfano wa hilo ni pale chama cha ANC kilipopendekeza sheria mpya kuhusu uraia wa nchi mbili ambayo ilikuwa inataka kuwakataza raia wa Afrika Kusini kujiunga na jeshi la Israel, IDF.

Rabi Mkuu wa Afrika Kusini Dokta Warren Goldstein alitoa majibu makali kwa sheria hiyo pendekezi, na kukiita chama cha ANC kwa unafiki na msimamo wake dhidi ya taifa la Israel.

Afrika Kusini imeanzisha sheria ambazo inazitaka bidhaa zinazoingizwa nchini humo kutoka Judea, Samaria na Jerusalem Mashariki kuwa na nembo maalumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *