Janet Jackson apata mtoto akiwa na miaka 50

Mwanamuziki wa Marekani Janet Jackson akitulia kwa ajili ya picha Mei 23, 2013 alipokuwa akiwasili katika mkutano wa mwaka wa masuala ya Ukimwi kusini mwa Ufaransa.

JANET Jackson amezaa mtoto wa kiume, kulingana na mwakilishi wa nyota huyo wa muziki wa pop nchini Marekani.

Jackson, 50, na mumewe, Wissam Al Mana, amemkaribisha mwanae wa kwanza, aliyepewa jina la Eissa, jana Jumanne.

“Janet amezaa vizuri kabila bila tatizo lolote na amepumzika,” alisema mwakilishi wa mwanamuziki huyo.

Mwezi April, Jackson alitangaza kwamba anaahirisha ziara huku uvumi ukiwa umeenea kwamba alikuwa na mimba.

“Nadhani ni muhimu kwamba mfahamu,” alisema katika video ambayo ilisambazwa kwa mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii. “Mume wangu na mimi tunajenga familia, kwa hiyo nitachelewesha ziara kwa sasa.”

Baada ya hapo, Jackson aliondoka kwenye maisha ya hadharani, japokuwa aliwahi kuonekana akinunua mahitaji kwenye duka kubwa mwezi Septemba na alionekana kuwa na mimba katika picha ambazo zilichapishwa katika jarida la Entertainment Tonight.

Mwimbaji huyo alithibitisha kwamba alikuwa anatarajia kujifungua katika mahojiano na jarida la People mwezi October. Jackson alifunga ndoa na mfanyabiashara wa Qatar Al Mana mwaka 2012.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *