Je, bado Michael Carrick ni muhimu katika kumsaidia Paul Pogba kufanya vizuri uwanjani kwa Manchester United?

Je, Paul Pogba anategemea sana pasi za Michael Carrick?

KIUNGO wa Manchester United Michael Carrick amekuwa akipumzishwa baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza katika mechi mbili za mwisho za timu hiyo katika uwanja wa Old Trafford. Lakini je, hii ni njia sahihi ya kuweza kupata ubora halisi wa Paul Pogba? Ili kumfikishia mchezaji huyo ghali zaidi duniani katika maeneo ya hatari zaidi uwanjani ni muhimu, anasema Adam Bate.

Ushindi wa Manchester United wa mabao 4-1 dhidi ya Leicester City mwezi Septemba mwaka jana ulikuwa ni muda muafaka kwa Paul Pogba kuonyesha kipaji chake. Alifunga bao lake la kwanza na kupewa tuzo ya mchezaji bora katika mechi hiyo, hivyo kupunguza kidogo mzigo unaotokana na fedha zilizotumika kumnunua.

Lakini labda ishara kubwa kwa Pogba kuweza kucheza katika kiwango kizuri akiwa na klabu ya Manchester United ilikuja baadae katika mechi hiyo – wakati ushindi ukiwa umeshapatikana – kiungo mwenye uzoefu Michael Carrick aliingia uwanjani kucheza mechi yake ya kwanza kabisa ya msimu wa ligi.

Kitu cha kushangaza ni kwamba Carrick hakuwa anapangwa wakati msimu unaanza kwa kuwa kocha Jose Mourinho alikuwa anatumia wachezaji wengine. Na kwa kweli, hakucheza tena kwa mwezi mzima baada ya mchezo ule na Leicester – na alianza katika ushindi mwingine wa mabao 4-1, dhidi ya Fenerbahce.

Katika mchezo huo, Mourinho alisema kwamba Carrick “alifanya timu itengemae vizuri” katikati na, kwa sehemu kubwa, hilo limethibitika. United imeshinda mechi 14 kati ya 19 ambazo Carrick ameanza msimu huu, ukilinganisha ni mechi 8 tu kati ya 18 ambazo hakucheza kabisa.

Limekuwa ni jambo la kawaida kwa watu kuzungumzia juu ya utulivu na udhibiti ambao unaletwa na kiungo huyo awapo uwanjani, kusikia jinsi anavyowasaidia wachezaji wanaomzunguka kuwa bora zaidi. Lakini huwa anawezaje kufanya hayo? Kuweza kutoa pasi kwa wachezaji kama Pogba mara nyingi inavyowezekana ni jambo muhimu sana.

Hata muda mfupi aliokuwa uwanjani dhidi ya Leicester ulitoa dokezo. Carrick alipiga pasi nane kwa Pogba pamoja na kwamba aliingia katika dakika ya 78 ya mchezi. Hajafikia kiwango hicho tena lakini kiungo huyo amekuwa ndiye mchezaji aliyepiga pasi nyingi zaidi kwa Pogba kuliko mchezaji mwingine yeyote.

Kwa sasa Carrick amepiga wastani wa pasi 14.1 kwenda kwa Pogba kwa kila dakika 90 ambazo wamekuwa uwanjani pamoja katika ligi kuu ya Uingereza msimu huu. Ander Herrera ni mtumiaji mzuri wa mpira lakini hata yeye ametoa wastani wa pasi 10.2 tu katika muda wa dakika 90.

Marouane Fellaini hupiga pasi kwa Pogba mara tisa katika mechi. Wayne Rooney, Juan Mata na Henrikh Mkhitaryan wanampa pasi 7. Inaweza kuonekana kuwa ni jambo dogo lakini ni muhimu sana katika kumsaidia Pogba kumiliki mchezo.

Kina nani humpa pasi Paul Pogba?

Baadhi ya wachezaji

Dakiki walizocheza na Pogba

Pasi kwa Pogba

Pasi kwa Pogba / dakika 90

Michael Carrick

821

129

14.1

Ander Herrera

1547

175

10.2

Marouane Fellaini

758

76

9.0

Wayne Rooney

836

68

7.3

Juan Mata

1013

74

6.6

Henrikh Mkhitaryan

692

50

6.5

Washambuliaji huishi kwa kutegemea huduma ya pasi lakini viungo washambuliaji pia wanahitaji huduma hiyo. Pogba, hasa, ni aina ya mchezaji ambaye anapenda kujaribu vitu tofauti anapopokea mpira. Na kwa kweli, amepoteza umiliki wa mpira mara nyingi zaidi ya mchezaji mwingine katika klabu ya Manchester United msimu huu.

Ni mmoja miongoni mwa wachezaji tisa katika ligi kuu ya Uingereza ambao wamepoteza mipira zaidi ya mara 400. Hata hivyo, ndiye mchezaji mbunifu zaidi kwa United awapo uwanjani. Anapopewa nafasi zaidi mwishoni anategemewa atakuja kuwa na majibu.

Hiki ndicho Carrick afanyacho. Si jambo dogo kuona kwamba Pogba amehusika zaidi na magoli katika dakiki 821 ambazi amekuwa uwanjani na Carrick kuliko katika dakika 1158 ambazo amecheza bila kuwa na kiungo huyo mzoefu uwanjani.

Pogba akishangilia bao na Carrick baada ya kufunga bao la kwanza dhidi ya Swansea

“Ameanza kuzoeana na wachezaji wengine,” alisema Mourinho kuhusu Pogba mwezi Novemba. “Anajisikia vizuri awapo uwanjani sasa. Hiyo ni njia nzuri ya kusema hilo. Kiungo chenye Pogba, Carrick na Herrera kinafanya vizuri.”

Hata hivyo, katika mechi mbili za mwisho za Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Liverpool na Hull – Mourinho amekuwa mwepesi kuachana na kiungo kinachowajumuisha wachezaji hao watatu, kwa kumtoa Carrick baada ya kumalizika kipindi cha kwanza. Timu nyingi hujaribu kuwazuia wachezaji hao kucheza mpira.

Sehemu kubwa ya mafanikio ya Liverpool katika kuidhibiti United kwenye uwanja wa Old Trafford mwezi uliopita ni kutokana na ukweli kwamba Carrick aliweza kumpa mpira Pogba mara mbili tu. Kutokana na Mfaransa huyo kuwa na hasira na kusababisha kucheza vibaya katika mechi hiyo ambayo alikuwa akitaka kufanya kila kitu lakini matokeo hayakuwa yakionekana.

Carrick mwenyewe hakuwa katika hali yake ya kawaida dhidi ya Liverpool, hivyo kuukumbusha ulimwengu wa soka kwamba, akiwa na umri wa miaka 35, si suluhisho la kudumu kwa United. Ni lazima Pogba atafute njia mbadala ili aweze kutoa matunda hata pale anapokuwa uwanjani bila Carrick nyuma yake.

Lakini kwa sasa inaonekana wazi kwamba timu bora ya Mourinho inapaswa kuwa na wachezaji hao wawili pamoja uawanjani. Na kwa kweli, baada ya kutolewa kwa Carrick dhidi ya Huu, jambo lililomlazimu Pogba kurudi nyuma zaidi, halikuifanya United icheze vizuri.

Kwa hiyo wakati Mourinho anapoamua timu itakayocheza mwisho wa wiki hii, tegemea kwamba Carrick na Pogba watakuwepo. Ni ushirika ambao Leicester watahitaji kuudhibiti iwapo wanataka kufanikiwa. Na ni ushirika huo ambao Mourinho anahitaji kuuamini iwapo United inataka kufanikiwa msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *