KUFIKIA mwanzoni mwa mwezi wa Aprili mwaka 1964, kama miezi mitatu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, mambo Visiwani humo yalikuwa shwari. Hali ya kisiasa ilikuwa thabiti na hivyo mazingira ya kijamii nayo yalikuwa mazuri.
Mandhari ya kisiasa ya wakati huo yalikuwa ya kimapinduzi. Hata steshini ya Redio ya Serikali iliacha kupiga nyimbo za taarab zilizokuwa na maudhui ya kimapenzi. Badala yake ikipiga nyimbo kuwaenzi wakwezi na wakulima na nyingine kuhusu Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
Serikali ya Mapinduzi, ikiongozwa na Sheikh Abeid Amani Karume, ilikuwa Serikali iliyokuwa na umoja. Wakati huo ilikwishaanza kuchukua hatua mbalimbali zilizokuwa na lengo la kuleta usawa katika jamii.
Hatua hizo, zikiwa pamoja na kutoa huduma bure za afya na elimu bure kwa watoto wote na kutaifisha ardhi, ziliwavutia wananchi wengi wa kawaida katika nchi nyingine za Afrika ya Mashariki.
Iwapo kuna wataosema kwamba hatua hizo hazikufanikiwa, ni swali jingine. Ukweli ni kwamba hatua hizo zilizitia homa serikali fulani. Haikustaajabisha kwamba mara baada ya Mapinduzi ya Januari 12 wanajeshi waliasi nchini Tanganyika (Januari 20), Uganda (Januari 23) na Kenya (Januari 24). Uasi huo haukushangaza kwa vile serikali za nchi hizo hazikuonyesha ari ya kuchukua hatua kama zile za Zanzibar ambazo zingewanyanyua watu wao.
Lakini labda waliotishika zaidi walikuwa wakubwa wa serikali za Kimagharibi. Pamoja na mengine walitishika na jina jipya la ‘Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.’ Nchi hiyo haikuwa Jamhuri tu ya kawaida baada ya kuondoshwa usultani lakini ilijitambulisha rasmi kuwa ni ‘Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.’
Kulikuwa tofauti kubwa kiitikadi kati ya nchi iliyokuwa ikijiita ‘Jamhuri’ na ile iliyokuwa ikijinata kuwa ni ‘Jamhuri ya Watu.’
Isimu hiyo ya pili ikitumiwa na serikali zilizokuwa zikijigamba kwamba zinatawala kwa maslahi ya wengi wa watu wao. Kinyume na Zanzibar lakini nyingi ya serikali hizo zikifuata itikadi ya kisiasa ya Kimarx na Kilenin au ya Kikomunisti.
Kufikia mwanzoni mwa Aprili 1964 wengi wa Wazanzibari walikuwa wamekwishayakubali Mapinduzi kuwa ni kudura ya Mungu. Watu wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.
Vituko vya watu kufukuzwa kazini kwa sababu za kikabila au za kisiasa vilizuka baadaye pamoja na visa vya kamatakamata na misiba ya mauaji.
Serikali ikiwapeleka nchi za nje kwa masomo ya juu wanafunzi wa kila kabila na ikiendesha shughuli zake kwa nidhamu. Hakukuwa na segemnege katika uendeshaji wa vyombo vya dola.
Ingawa mazingara yalikuwa tofauti na yale ya serikali iliyopinduliwa, watumishi wakuu wa serikali waliiendesha nchi kwa mujibu wa sheria zilizokuwapo na mpya zilizotungwa na Baraza la Mapinduzi.
Hali hiyo iliyodumu kwa muda mfupi iliwafanya wengi wawe na matumaini na mustakbali wa taifa lao jipya. Leo tukikaa na kuipima hali ya mambo ilivyokuwa hatuoni ushahidi kwamba utawala wa Karume ulikabiliwa na kitisho kikubwa cha kutaka kuuangusha.
Sisemi kwamba hakujakuwako watu waliokuwa wakiiapiza serikali yake na waliokuwa wakiomba isambaratike au ipinduliwe moja kwa moja. Walikuwepo. Lakini nguvu zao za kuandaa mapinduzi ya kuyapinga Mapinduzi ya Januari 12 zilikuwa dhaifu. Hakuna mpinga Mapinduzi aliyethubutu kufurukuta wakati huo.
Tarehe Aprili 13 Karume alimwambia Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Salim Rashid, kwamba Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa Tanganyika, alimpigia simu akimtaka ende Dar es Salaam. Siku ya pili yake Karume na Salim Rashid wakafunga safari kwenda kwa Mwalimu.
Walipofika Ikulu, Dar es Salaam, Mwalimu huku akimuangalia Salim Rashid aliwaambia wasaidizi wake: ‘Mpeni gari (Salim) akanyoe ndevu.’
Ni wazi kuwa Nyerere hakutaka Katibu wa Baraza la Mapinduzi asikie aliyokuwa amepanga kumwambia Karume. Ndipo Salim Rashid akashika njia kwenda kwa kinyozi akimuacha Karume na Mwalimu. Mbali ya Marais hao wawili hakuna mtu anayejuwa kwa uhakika nini hasa kilijiri kati yao sebleni Ikulu.
Kuna wanaoshikilia kwamba Nyerere alimtisha Karume kwa kumwambia kulikuwa na njama za kumpindua na kwamba muungano wa nchi zao utampa himaya.
Na kuna wasemao kwamba wakati huohuo Nyerere alisema atawarejesha kwao askari polisi 300 Wakitanganyika waliokuwa na silaha na waliopelekwa Zanzibar kusaidia kuzuia fujo.
Miaka michache kabla ya hapo Karume aliwahi kutaja nia yake ya kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika na kuifanya iwe jamhuri. Kauli hiyo, aliyoitoa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na iliyoripotiwa kwenye gazeti la Mwongozo la chama cha Zanzibar Nationalist Party (maarufu kwa jina la Hizbu), ilimchongea baadaye amuangukie na kumtaka radhi sultani wa wakati huo Seyyid Khalifa bin Haroub.
Ingawa tangu hapo Karume alikuwa na ndoto ya Muungano wa Zanzibar na Tangayika hatujui akitaka uundwe kwa masharti gani au uwe wa aina gani. Tunachoweza kufikiria ni kwamba matamshi ya Nyerere ya Aprili 14 yalimtia hawafu kubwa Karume kiasi cha kumfanya ampe mwenzake aliyemzidi akili uhuru kamili wa kuziunganisha nchi zao.
Aliporejea Zanzibar Karume aliwaficha memba wenzake wa Baraza la Mapinduzi alichokubaliana na Nyerere. Siri ya Muungano ilikuwa yake peke yake Zanzibar. Hakulishauri Baraza la Mapinduzi, hakuishauri serikali wala hajakishauri chama cha Afro-Shirazi Party (ASP).
Wadadisi na wataalamu wengi wenye kuitalii kwa kina historia ya Muungano wanaamini kwamba ingawa Nyerere alikuwa mtetezi wa umoja wa Afrika na ingawa Karume alikwishadokeza kwamba angependelea Zanzibar na Tanganyika ziungane, Muungano ulioundwa Aprili 26 mwaka 1964 uliandaliwa ili kuliridhia matakwa ya dharura ya Marekani.
Wakati huo Marekani kwa kweli ilikuwa hamnazo, majununi kabisa, kuifikiria Zanzibar kuwa ngome ya ukomunisti upande wa Afrika ya Mashariki na kitisho kwa maslahi yake. Marekani ikawa mbioni kutafuta njia au mamba wa kuyameza Mapinduzi ya Zanzibar.
Siku tatu au nne baada ya huo mkutano wa siri wa Marais wawili Karume alipelekewa Hati za Muungano kutoka Dar es Salaam. Hati hizo alikabidhiwa Ikulu ya Zanzibar na aliyekuwa waziri mdogo wa mambo ya kigeni wa Tanganyika.
Hii leo mustakbali wa Zanzibar uko njia panda kama ulivyokuwa pale Karume na Nyerere walipoziunganisha nchi zao. Lakini hali halisi za Aprili 1964 na za leo zimebadilika sana. Hii ni kwa sababu kwanza hali ya ndani ya Zanzibar kwenyewe imebadilika; pili, mahusiano yake na nchi zilizo ngeni kwake yamebadilika na tatu, mazingara ya ulimwengu pia yamebadilika.
Mnamo Aprili 1964 mustakbali wa Zanzibar uliamuliwa kwa njama zilizoandaliwa na Marekani pamoja na madola mengine ya Kimagharibi, ambayo tunaweza kuyabandika lakabu ya ‘wapishi wa kimataifa’. Mpishi mwengine alikuwa jirani Tanganyika.
Kama inavyokumbushwa mara kwa mara Muungano uliopo leo sio ule ulioelezwa na Hati za Muungano, zilizokuwa na mambo 11 tu ya Muungano. Kwa muda wa miongo kadhaa Zanzibar ikiachiwa ijiendeshe yenyewe.
Kwa mfano, ilikuwa na uhuru kamili wa kisiasa toka 1964 hadi 1972 alipouliwa Sheikh Karume.
Kwa upande wa uchumi serikali za Zanzibar ziliendelea kuwa na uhuru kamili mpaka ilipoingia ile ya awamu ya tano ya Rais (Mstaafu) Salmin Amour. Serikali hiyo ilishindwa nguvu na shinikizo za Bara. Ikabidi isalimu amri na kuchanganya sera yake ya fedha pamoja na kodi na ushuru na ile ya Bara (yaani ya serikali ya Muungano).
Tukiuzingatia umoja walio nao Wazanzibari na matarajio yao kwa Serikali yao ya Umoja wa Kitaifa, halitokuwa la ajabu iwapo mchakato utaopelekea kupatikana kwa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania utayathibitisha matakwa yao.
Matakwa hayo yatabainika watapotoa maoni yao kwenye Tume ya Katiba na yataonyesha kuwa wengi wao watataka pawepo Muungano wa Mkataba na si wa Katiba.
Ushahidi kwamba hali ya mahusiano ya Zanzibar na Muungano ni tofauti na ilivyokuwa zamani ni ile migogoro isiyokwisha kati ya pande hizo mbili. Shtuma zilizoko Visiwani ni kuwa Serikali ya Muungano yenyewe ndiyo inayoianzisha migogoro hiyo, kama kwa mfano kwa kuandikiana mikataba na jumuiya za kimataifa kwa niaba ya Zanzibar au kwa kuwa na makubaliano ya kibalozi kwa niaba ya Zanzibar na madola ya nje, mfano Norway.
Serikali ya Tanzania haina haki ya kufanya hivyo hata ikiwa sekta zote zinazohusika za utawala ziko chini ya mamlaka yake. Na hivyo sivyo ilivyo. Tena haina haki hiyo kwa sababu mfumo wa Muungano uliopo sasa si wa kudumu kwa vile kuna huu mchakato wa kuamua kuhusu majaaliwa ya Muungano wenyewe pamoja na mfumo wake na katiba yake.
Wakuu wa Bara watapata taabu Zanzibar na huenda hata wakahatarisha usalama endapo watajaribu kushikilia kwamba mfumo uliopo sasa wa Muungano uendelezwe kama ulivyo.
Hatimaye tukumbuke kuwa ulimwengu nao pia umebadilika. Tujuavyo, tena kwa uhakika, ni kuwa kinyume na mwanzoni mwa 1964 hii leo nchi kadhaa za Kimagharibi ziko tayari kuiunga mkono Zanzibar ikiwa itadai mamlaka yake kamili kutoka Serikali ya Muungano. Tumeyadaka haya faraghani yakidondoka kutoka ndimi za wanabalozi wa nchi fulani wasiotaka kutajwa.
Maoni ya Wasomaji
Ndio maana kila siku tunasema
Ndio maana kila siku tunasema sisi wazanzibari matatizo yote yanayotusibu ni siasa za kijanja na choyo za Mwalimu Nyerere, kwani hilo hakulifanya tuu Zanzibar ila maeneo mengi ya Tanganyika ambayo alikuwa na chuki binafsi na maeneo hayo. Wazanzibari Nyerere ndie adui yetu namba moja, wa pili Mkapa
We mchangiaji aweje adui yako
We mchangiaji aweje adui yako namba moja Nyerere na sio Karume alokuwa ametaka kuunganisha Zanzibar na Tanganyika hata kabla ya mapinduzi??? Na Mkapa anaingiaje hapa au unachuki na Wakristo?? TANZANIA ni nchi yetu sote Wakristo kwa Waislamu, na mnadhani Wanzibar watapata misaada ya falme za kiarabu au mnataka tena mrawaliwe na Masultani toka Oman?? Mnataka kuweka tena tabala la mwarabu,mnyamwezi na mmakonde?
Ulaya wanajaribu kuungana sisi TANZANIA eti twataka kutengana, sijui ni zimwi gani hili. Marekani imeitwa Umoja wa nchi za Amerika (United states of America) kwa sababu wameunganisha vi-state vyao likwa nchi kubwa na sasa lina nguvu kubwa duniani sisi twatengana. Na mkisha maliza kuitenga Zanzibar toka Tanganyika baada ya miaka 20 tutaona madai ya Nchi ya Pemba na nchi ya Unguja.
Nilitamani Zanzibar iwe kama mkoa wa Tanzania.Ili Mzanibari ajisikie sawa na Mkilimanjaro au Mbeya, pasiwepo na serikali ya Zanzibar lakini hoja hii ya Mwalimu yafa kwa uroho wetu kisa mafuta ya pemba.
Langu jicho
Kusema kuwa Zanzibar tunataka
Kusema kuwa Zanzibar tunataka kutawaliwa na Waarabu ni matusi. Tunachotaka ni kuwaondoa wakoloni weusi kutoka bara ili tuweze kujitawala wenyewe. Tumekaa katika ukoloni miaka zaidi ya 40 na hatujakiona tulichopata zaidi ya kuletewa Wakristo kuja kujenga makanisa Zanzibar na kuleta wasichana wa bara kuja kutuenezea ukimwi. Tuachieni nchi yetu. Kwani mkituachia tujitawale wenyewe nyinyi mtakosa nini. Mbona bara nchi kubwa, mnaishikilia Zanzibar kwanini?
habari yko kaka pole na
habari yko kaka pole na majukumu ya kila siku kila siku siku naeleza au nakuelaza kaka Ahbed rajabu kuwa milango ipo wazi muungano ni km koti ukiona linakubana ruhusa kulitoa ss cjui kinacho washindwa nn kuvua koti wakati kwa madai yenu linawabana km rais mnae tatizo lenu kubwa unafiki unawagarimu sna AMANI KARUME halijifanya mie ntarudisha ASP wpi mpk leo sie wenyewe tumewashoka karikoo zima maduka karibu yote wamejaa wapemba
no doubt about it.
No doubt about it.
Ahmed, kama unadhani nchi za
Ahmed, kama unadhani nchi za magharibi zina nia njema endelea kuwashawishi wazanzibar hivyo. Mbona hawaungi mkono Haiti iliyo karibu na New York.
Pili, mbona hutaji mambo 11 na yale yaliyoongezwa ili tujue yanamsaidia nani na nani anafaidi
Tatu, Unadhani Mbara anafaidika nini kutoka Zanzibar
" , Unadhani Mbara anafaidika
" , Unadhani Mbara anafaidika nini kutoka Zanzibar"
1. Anafaidika kusambaza ukatoliki na kujenga makanisa yasiokuwa na waumini wakizanzibari.
2. Kuleta majambazi wenye kutumia silaha za moto. Kuleta UKIMWI wa kuleta makahaba kuja kufanya biashara ya umalaya.
3.Kutibia rasilamali zetu mchana tena kweupe (Bahari, mafuta......)
Wabara wananufaika sana
Wabara wananufaika sana Zanzibar kwa kuwa wanakuja kueneza Ukristo na kujenga makanisa. Pia wako mstari wa mbele kujenga vilabu vya pombe. Ni kinyume kabisa na wazanzibari wanaoishi bara ambao wanafanya biashara. Wabara wakija Zanzibar kufanya biashara basi huenda maeneo ya baharini wakajenga vibanda ikawa kazi yao kufanya ufuska, ukahaba, kuuza pombe na kubaka wasichana.
Kuamini kwamba eti baada ya
Kuamini kwamba eti baada ya kuungana bado Zanzibar inaweza kufanya shughuli zake za kibalozi peke yake, ni ujinga wa asubuhi. Semeni kama hamtaki Muungano mwende zenu; Muungano haukuletwa na Wamarekani bali Nyerere na Karume kama ulivyosema mwenyewe hapo juu. Hakuna balozi yeyote anayeunga mkono kuvunja Muungano. Kama yupo mtaje, usilete lugha ndefu. Magharibi wanahofu kuwa mtakuwa magaidi huko Zanzibar, unadhani wao wajinga?
Pili, nadhani hili gazeti ni la Kiswahili. Ni heri mwandishi ukatumia Kiswahili sanifu badala Kiunguja na Kiingereza-Kiswahili.
Msomaji wa Raia Mwema.
Kwa kukufahamisha tu,
Kwa kukufahamisha tu, KIUNGUJA ndio Kiswahili sanifu.
Kama unatoka kapa kwa baadhi ya maneno ndio ujijue kuwa hujui Kiswahili
Na hata Jumuiya ya Afrika ya Mashariki imeridhia hilo. Tafuta magazeti mengine yanayoandika Kitanganyika usome.
Kwa kweli inshangaza sana
Kwa kweli inshangaza sana kuona kuwa watu wa bara ambao Kiswahili ni lugha yao ya pili kujifanya wanajua Kiswahili kuliko wenye Kiswahili yaani wazanzibari. Hii ni sawa na kuwaona wanaigeria wakajifanya wanajua English kuliko Waingereza.
kaka adui wa tatu ni nani?
kaka adui wa tatu ni nani?.kwani nchi imetawaliwa na wengi na bado hajalekebisha. sasa tunaomba wa tatu kama humtaji wewe ni mnafki na uwatakii mema wazanzibari ila chuki binafsi.kinachotakiwa ni kiongozi atakayevunja muunganoa kama maraisi wametawala 4 na wote hawavunja muungano na wewe unawataja wawili tu wewe ni mnafki
Watanganyika kama kutajiwa
Watanganyika kama kutajiwa zanzibar kujitenga mna hamaki, basi mutazidi kuhamaki kwa vile sasa wazanzibar wameamka na wameapa kuwa wakati wa mjadala wa katiba mpya wataamua na hususan kupitia kura ya maoni kwa hiyo kaeni mkao wa kula. acheni kumshambulia ahmed rajab anayosema yote ni ya kweli, sasa hivi tunapita kila mtaa, kijiji, mwilaya na mkoa kutoa elimu ya kujitenga na mkoloni mweusi tanganyika.
Mwandishi mnafiki anapomtaja
Mwandishi mnafiki anapomtaja Nyerere na Mkapa wakati tumekuwa na Mwinyi ambaye pia amewahi kuwa rais wa Zanzibar kabla ya kuja bara, hasemi kama ameharibu chochote katika muungano au amejenga chochote, ni mnafiki aliyejaa chuki zisizo na mpango
<p>Inawezekana ni mdini......
<p>Inawezekana ni mdini......</p>
Nona Razak umeshtuka sana
Nona Razak umeshtuka sana kutajwa Nyerere na Mkapa na unataka lazima Mwinyi atajwe kuwa na yeye ameharibu chochote.wakati wa utawala wake. Nikuulize, kwani hujui kuwa Mwinyi ndie aliyekutoweni kwenye umasikini wa kutupwa ambao mlikuwa mkitembea matako nje kwa suruali kuwa na viraka. mmesahau kuwa mkifuata gunia la sukari kama mmeiona almasi.
Lazima mumshukuru Mungu kwa kumleta Mwinyi angalau leo mmejuwa kuiba na kuwa na nguo nzuri, gari nzuri na nyumba nzuri
Kwani kitu gani ambacho
Kwani kitu gani ambacho Nyerere amekifanya kibaya kwa wazanzibari haya sasa unamuingiza na Mkapa amewaudhi nini nyie wazanzibari mbona mwinyi hamumsemi au huyu bwana mkubwa wa sasa acha chuki za udini ndg yangu jenga taifa lako acha ujinga looh.
@ Ahmed Razak
@ Ahmed Razak
Rais Mwinyi hakumtaja kwa sababu ni mwenzenu kutoka bara na ndio maana Nyerere akampa urais wa Tanzania.
Mwinyi ni Mzaramo kutoka Tanganyika na alililetwa Zanzibar katika miaka ya 40's na kulelewa na ukoo wa kina marehemu Maalim Amour Ali Ameir AL Marhubby. Alipoletwa Zanzibar jina lake la Kizaramo lilikuwa Nzasa na ndipo walezi wake walipolibadilisha na kuitwa Ali. Baadae walimpeleka skuli kuanza masomo yake ya primary na kumalizia masomo yake katika skuli ya Dole ambapo wakati huo ilikuwa maarufu. Baada ya hapo ndipo ailipokwenda kusoma Teacher's Traininng na kuwa mwalimu.
Ali Hassan Mwinyi si Mzanzibari wa kuzalliwa na wala wazee wake si Wazanzibari bali aliupata Uraia wa Zanzibar kwa kukata Tajnis yaani Registration. Hivyo basi ndio maana Mwandishi wa makala hii hakumtaja Mwinyi katika makala yake kwa sababu anamjuwa fika Mwinyi ni mtu wa aina gani.
wakati umefika wa kura ya
wakati umefika wa kura ya maoni ya kuamua hatma ya muungano huu,ikiwa ridhaa ya wananchi wa pande hizi mbili watakubali vipengele vya muungano kwa maslahi yao basi taabu hizi zitakwisha.
Ifahamike kuwa muungano huu hauna ridhaa ya wananchi wa pande zote na yalikuwa ni makubaliano ya viongozi pekee,jiulize wewe mtanganyika je uliwahi kukubalit taifa lako liungane na taifa lingine(zanzibar)? pia mzanzibari hivyohivyo.
Wenyenchi umefika muda tudai haki zetu juu ya muungano huu
Hatufaidiki na Zanzibar
Hatufaidiki na Zanzibar afadhali huu muungano ufe. Wewe mzanzibari unayejifanya unajua kiswahili hujui kiunguja siyo kiswahili sanifu ila kinafanana, umetumia neno "umetoka kapa" hiyo ni kiswahili chetu wabara, usijisifie bure na kiunguja....je unajua BAKITA ndiyo inayo-regulate kiswahili? mtabaki na kiswahili kisichoendelea kama ambavyo visiwa vyenu vilivyo. Badala ya kufanya kazi kwa bidii mnategemea kupewa kila kitu...mnadhani kila kitu kitatoka arabuni? mjifunze kufanya kazi kwa ufanisi, mmeshaachwa mbali sana na Bara. HATUNA HAJA NA UPUUZI HUU UNAOITWA MUUNGANO. Mbona mna wabunge wenu huko Dodoma wanafanya nini huko? kwa nini msiwaambie mdai nchi yenu? hakuna hata mbunge mmoja anayedai kuuvunja huo muungano ambao sisi huku bara tumechoka nao.
Kila unavyozidi kuandika
Kila unavyozidi kuandika ndivyo unavyojionesha UJINGA WAKO. Hupo hata duniani.
Unamlaumu muandishi kwa kuandika kingereza-kiswahili wewe umeandika utumbo gani Eti " usijisifie bure na kiunguja....je unajua BAKITA ndiyo inayo-regulate kiswahili? Hiyo lugha gani kama si Kitanganyika?
Hivi wewe huna hata akili za kiwendawazimu ukijua kuwa Wazanzibari japo ni milioni moja tu inakuatwaleni kisiasa na kiuchumi? Tuna wabunge na tuna mawaziri ndani ya serikali yenu ya Tanganyika lakini Zanzibar hampo. Nani mwenye Akili?
Andika hoja za msingi na soma na kama hujui uliza, tena waulize hata BAKITA Kiswahili wanachotumia ni kipi. Ni KIUNGUJA. Inaonekana hata lahaja za Kiswahili huzijui
Msimamizi wa lugha ya Kiswahili ni Zanzibar. Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki wameridhia. Soma ujue au uliza ujifunze,utokane na ujinga
Hata wazanzibari hawataki kabisa Muungano na watu ambao bado mpaka karne hii hawajasttarabika: WANACHUNANA NGOZI NA KUWAKATA VIUNGO WALEMAVU WA NGOZI"
Imefika hatua kuwa Mtangahyika hawezi kukaribishwa kwenye nyumba kwa kuogopa ima ni Jambazi, Mchuna ngozi, mkata viungo au kahaba. LO TUMECHOKA
Kwakweli, mie naombnea huu
Kwakweli, mie naombnea huu Muungano uvunjike haraka, halafu tuwaone hao wazanzibar watakavyomalizana, mana wapemba hawatakubali mafuta waliyonayo watumie pamoja, na piapemba watataka uhuiru wao
mMZANZIBAR ANAPATAJE UKIMWI
mMZANZIBAR ANAPATAJE UKIMWI BILAM KUWA MALAYA, FAFANUA
<p>Bwana Ahmed Rajabu ni
<p>Bwana Ahmed Rajabu ni mwandishi aliye bias, unasema hujuia mwalimu aliongea nini na karume still unasema alimtisha... unajua unamdhalilisha karume kwa kusema ni muoga??? inakuaje kiongozi wa mapinduzi.... awe muonga?? unamjua karume vizuri wewe?? mtu aliyekubali kufa kwaajili ya watu wake gafla aogope na kuwatia watu wake kwenye mabalaaa?? unajua unawafanya nini wazanzibar wenzio kwa kuongea hivi??? unawakumbuka waandishi wa kimbali???...... Muungano Sheikh Karume ndiye aliyekua mtu wa kwanza kuutaka... kwasababu ya usalama wa watu wake baada ya uhuru... tatizo la muungano ulifanyika kwa haraka mambo mengi hayakupitiwa vizuri..... na uharaka wake unaeleweka... sasahivi muungano umeingiliwa na siasa.... hakuna mtu wa Tanganyika ambaye anataka huu muungano kama si wanasiasa vivyo hivyo kwa wazanzibar... Chama tawala kinajua kwanini kinataka huu muungano, na watu wake wanaotaka haya wapo bara na visiwani..... watu wa bara hatuna tabia ya kuchukia watu tunakaribisha wageni hatujali dini rangi wala tabia... na ndiyo maana wazanzibar ni wengi sana bara na wengine sijui kama wanampango wa kurudi, waulze kama walishawahi kufanyiwa aina yoyote ya ubaguzi.... wabara hawajalelewa hivyo.... umeuliza wabara wanaokaa huko zanzibar??? wanaitwa machogo... watanganyika nchi yao imefutwa kisa muungano hivi unajua wanajisikiaje??? hivi Tanganyika ni nchi ya kuwa na tamaa na nchi nyingine kwa rasilimali zote zilizopo?? Nini kipo Zanzibar hamna Tanganyika??? karafuu?? unajua vilivyo bara havipo zanzibar??? watanganyika kamwe hatutawalaumu wazanzibar kwa umasikini wetu sababu tunazijua na tunazishughulikia moja ni siasa zisizo na mwelekeo..... mmeweza kushughulikia swala la upemba na uunguja sasa mnazua la ubara na uvisiwani..... hamchoki kuzua na likiisha hili sijui mtaelekea wapi..... KAKA AHMEDI RAJABU USIHANGAIKE KUTAFUTA MCHAWI WA UMASIKINI WA WAZANZIBAR.... MCHAWI NI WAO WENYEWE....</p>
Napenda kwa mara nyengine
Napenda kwa mara nyengine kumpongeza Mwandishi Ahmed Rajab kwa makala nzuri na napenda kukuhakikishia kuwa tuko wasomaji wengi ambao tunavutiwa sana na makala zako.
Mwisho, napenda kuungana na wewe kuwa Wakuu Bara asilazimishe kuwa lazima mfumo uliopo sasa uendelee maana na kwa maoni yangu kuwa watakuwa wamechezea shillingi chooni/
Naona wote waliokuwa wakitoa
Naona wote waliokuwa wakitoa maoni wana jazba, mwandishi nampongeza kwa uandishi uliojingiza ndani. Ni kati yako wewe na mimi yaani Tanganyika nchi iliyokufa na Zanzibari Tuamue je twahitaji muungano au la. Tunataka maoni hayo kwenye mchakato wa Katiba mpya. Isipokuwa mimi ninavyojua Bara na Visiwani walikuwa wakishirikiana tokea enzi za babu zetu. Ukoloni ndio uliotenganisha. Kama kuna matatizo ya muungano yajadiliwe bila jAZBA. hAKUNA ANAYEFAIDI MUUNGANO WOTE BILA.Isipokuwa muungano utakapovyunyika tutaona nani aliyekuwa anfaidi kutoka kwa mwenzake. Sijui Wapemba wa Kariakoo wanasemaje
Mimi nashangazwa sana kuhusu
Mimi nashangazwa sana kuhusu Mwalimu-kweli alikuwa kiongozi hodari wa kujenga hoja na busara isipokuwa alinishangaza kuhusu msimamo wake kuhusu Biafra akijua ni sehemu ya shirikisho la Nigeria,alinishangaza kuingiza nchi katika vita na Idi Amin kwa sababu ya Obote na mambo ya Amin nchini mwake.Alinishangaza sana jinsi alivyouwa uchumi kwa kuwapeleka maswahiba zake kwenye uzalishaji viwandani na katika utengenezaji wa sera za kiuchumi.Alinishangaza sana jinsi alivyokuwa mdini mkandamizaji huku akiimba kijamaa akicheza kikatoliki.Wakati wa ukoloni waislam wakiunda vyama katika nchi hii walikuwa na madai ya msingi kuhusu haki zao na usawa.Kipindi chote alichokaa madarakani HAKUWEZA KUREKEBISHA BALI ALIZIDI KUWAKANDAMIZA.Kwa upande wa Karume ulikuwa ni ujinga wake wa madaraka- hofu dhidi ya Kina Okelo na wakomunisti ambao wengine walikuwa maarufu kuliko yeye.Siasa za Zanzibar ni miongoni mwa siasa chafu kwani hadi leo wengi wetu hatujui nani alipanga MAPINDUZI.Wale wazanzibar hawakufanya mapinduzi...Katu hawakufanya. Ni John Okello na kundi lake.Nani aliwatuma hadi leo hakuna majibu sahihi.Tukija katika Muungano kulikuwa na hila.Haukuwa na RIDHAA-Karume alilazimika.Kwa nini?Kama Bwana hautaingia mkataba huu jua suala la John Okelo na wakomunisti utajua utapambana nalo vipi?Draft zilifanya kwa upande mmoja yakiwa makubaliano baina ya nchi mbili.