Hapo zamani kulikuwa na misitu iliyokuwa ikimilikiwa na Serikali za Mitaa na ile ambayo ilikuwa ikimilikiwa kwa ajili ya kuabudu. Lakini hivi sasa huwezi kuona misitu ya kuabudu ambayo kwa upande mwingine ilikuwa ikisaidia kuhifadhi misitu mingi
Kesi Bodi ya Mikopo iharakishwe kwa haki
JUMATATU wiki hii, Mfanyakazi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB), Esther Budili, alifikishwa mahakamani kwa tuhuma tisa za kughushi majina hewa ya wanafunzi na kisha kujipatia takriban Sh milioni 90.7.
Kutokana na unyeti wa suala hili kwa nchi, tunashauri kesi hii iendeshwe kwa kasi ya kipekee. Ushauri wetu unazingatia pande zote mbili katika mchakato huo wa kesi, yaani upande wa mtuhumiwa na upande wa mashitaka.
Katikati ya pande hizo mbili, yapo mazingira maalumu tunayoyabaini ambayo, busara inaelekeza ni vema kesi iharakishwe. Kwanza, ni kweli kama ilivyo kwa wananchi wengi, tunapinga ubadhirifu wa aina yoyote wa mali ya umma.
Kama ilivyo kwa Watanzania wengi, tuliungana kulaani wizi wa mabilioni katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na ufisadi mwingine katika maeneo mengi, na hasa ndani ya taasisi za umma. Bado msimamo wetu ni kupinga na hata kushinikiza kila inapobidi, watuhumiwa wafikishwe mahakamani.
Ni kweli, ufisadi ni ufisadi. Si sahihi kusema ufisadi wa aina hii athari zake ni chache ikilinganishwa na ufisadi wa aina nyingine. Au kusema ufisadi katika maliasili za nchi ni wenye athari chache ikilinganishwa na ufisadi katika sekta nyingine za huduma kwa umma.
Lakini pamoja na ukweli huo, tunaamini unyeti wa sekta moja hadi nyingine katika nchi unatofautiana. Kwa hiyo, udhaifu wa sekta moja hadi nyingine na hasa katika nidhamu na umakini unaweza kutofautiana.
Hivyo basi, ingawa tunalaani uovu wowote na popote kisekta, lakini tunaamini hujuma katika sekta ya elimu (iwe wa juu, kati au ya msingi), ni jambo baya zaidi ya uhujumu uchumi. Na katika kuamini hivyo, ndiyo maana tunasisitiza kesi hii ya aina yake isikilizwe haraka ili kutoa haki kwa pande zinazohusika.
Kuchelewa kuendeshwa kwa kesi hii kunaweza kuleta maafa kwa pande mbili. Kwa mfano, upande wa umma na hasa wanafunzi wa vyuo vikuu au familia zao ambao kwa muda mrefu wamekuwa na migogoro kuhusu mikopo ya elimu, wanaweza kupoteza imani na mwenendo wa kesi hii kama ushauri wetu hautazingatiwa. Na inapotokea kundi hili likakata tamaa wanaweza kujichukulia “sheria mkononi” dhidi ya upande wa mshitakiwa.
Lakini kwa upande wa pili, mtuhumiwa naye usalama wake pengine na familia yake upo shakani na kwa kadiri kesi itakavyochelewa ndivyo hatima ya usalama wake utazidi kuwa finyu na hasa inapotokea, nyuma yake wapo wakubwa wengine wanaohusika. Huyu anaweza kupata misukosuko mingi ambayo wakati mwingine si ya lazima au inaweza kuepukwa kama kesi itaendeshwa kwa kasi zaidi.
Elimu ni nguzo ya taifa. Vyombo vya umma na hasa Mahakama kwa sasa inabidi kuonyesha unyeti wa suala husika kwa kuendesha kesi hii kwa kasi inayolingana na uzito wa mazingira.
Tunaweza kuzembea kwingine kwa kigezo cha utawala bora na tukaishi kwa matumaini, lakini kuzembea katika utawala bora kwenye sekta ya elimu ni kuwaondoa Watanzania katika kuishi kwa matumaini. Bila kuingilia uhuru wa Mahakama, tukumbushane kuwa, wakati kuna tuhuma za wizi wa bilioni hizi zaidi ya 90, bado wanafunzi wanahitaji mabilioni ya mikopo.
Comments
Hivi huu ufisadi ni tatizo
Hivi huu ufisadi ni tatizo lisilioweza kutatulika kabisa Tanzania? Kwa nini viongozi mafisadi nao hawajachukuliwa hatua zozote hadi leo? Je,inawezekana kwamba hata huyu dada ni mtoto wa Kigogo naye na huenda akawa huru tu na haitakuwa jambo la kushangaza?
Bwana Bwire..Na wale
Bwana Bwire..Na wale wanafunzi wa UDSM waliofungwa mahabusu au kufukuzwa chuo kwa masuala haya ya Mikopo waachiwe huru ,mara moja.Hapa huyu mama hawezi kuwa peke yake..kuna msururu.Kodi zetu jamani
<p>Inauma sana kuona wenzetu
<p>Inauma sana kuona wenzetu kuacha chuo kisa serikali haina pesa wakati mama kama huyu anatafuna pesa za serikali. Hebu serikali oneni aibu na kumuogopa MUNGU na msimamaie kwa ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya kama mlivyozoea kusema wenyewe.</p>
Huyu ni chambo tu jamani.
Huyu ni chambo tu jamani. Wewe uliza alikuwa na nafasi gani? Huyu ametumiwa tu kama chambo. Bodi imeoza sana. Wanaokatwa mikopo ndio majina yao yamewekwa kwamba hawalipi. Na ambao hawajawahi kulipa hata kidogo majina yao hayajawekwa. Wale wote ambao walimaliza chuo na kujiajiri wenyewe pia majina yao hayajawekwa. Chunguza uone shirika la mafisadi
SUALA LA UFISADI BODI YA
SUALA LA UFISADI BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU SI GENI KWANI HATA WAKUBWA WA IKULU YA MAGOGONI WANALIJUA FIKA HUYU DADA ANATAKA KUFANYWA MBUZI WA KAFARA TU.YAWEZEKANA KABISA HUYU DADA AMETOFAUTIANA KWENYE MGAWO NA WAKUBWA NDIO MAANA UNAONA KAKUMBWA NA MISUKOSUKO KWANI PALE BODI KILA MFANYAKAZI PALE ANA MTU WAKE MKUBWA WA KUMLINDA HUKO JUU KABISA NDIO MAANA MADAI YA WANFUNZI WA VYUO VIKUU SIKU ZOTE HAYATILIWI MAANANI HATA KIDOGO.HESLB NI MRADI WA ''WAKUBWA'', NINAPOSEMA WAKUBWA NAMAANISHA KUWA WAKUBWA KABISA KTK NCHI HII,FUATILIA KWA MAKINI AU FANYA UCHUNGUZI WA KINA UTAGUNDUA TU KUWA BODI YA MIKOPO NI MRADI WA WAKUBWA
hii nchi jaman mbona utu na
hii nchi jaman mbona utu na kumwogopa Mungu kumeisha... Siku watz wakizinduka! Hapatakalika hapa.
Mimi nimemchoka Rais kabisa
Mimi nimemchoka Rais kabisa wala sitaki tena kusikia habari zake. Nikifikiria mambo ya ajabu anayo yakalia kimya kama vile hayupo!! Sioni sababu ya kuwa na Kiongozi wa aina hii HAKI YA MUNGU. 1. Wabunge na posho za 330,000 kwa kukalisha matako Bungeni na kuchapa usingizi baada ya bia za jioni na makahaba wao wa kirangi na kizanzibar wanao jiuza Dodoma City jioni kunapo kuwa na vikao vya Bunge- QUICK SIGNATURE 2. Ma-Daktari kunyimwa posho na kunyanyaswa kama vile vitoto vya paka mwenye virusi bila msaada - DEAF EAR, BIG SILENCE. Kufungwa watoto wa wakulima kwa kudai posho za kujikimu vyuoni na kuteswa na polisi na kufikishwa mahakamani bila huruma kwamba wazazi wao wapiga kura wake wanaumia mioyo yao kuona mtoto aliaga nyumbani kwenda chuo lakini badala yake anaishia kufungwa jela na kuteseka bila msaada - STUPID SILENCE AND A DEAF EAR. Kelele za wananchi kwa mafisadi na wawekezaji wakorofi, wanao inyonya nchi hadi wengine hapa Arusha wanatorosha wanyama hai huko Moshono ambako wamejichimbia - CLOSED EYES, DEAF EAR AND SILENCE. Watu kusingiziwa kesi na kubambikiwa makosa bila sababu - NO HELP, DEAF EAR, REJOICING. p>Mimi nimemchoka Rais kabisa wala sitaki tena kusikia habari zake. Nikifikiria mambo ya ajabu anayo yakali kimya kama vile hayupo!! Sioni sababu ya kuwa na Kiongozi wa aina hii HAKI YA MUNGU.
1. Wabunge na posho za 330,000 kwa kukalisha matako Bungeni na kuchapa usingizi baada ya bia za jioni na makahaba wanao wa kirangi na kizanzibar wanao jiuza Dodoma City jioni - QUICK SIGNATURE
2. Ma-Daktari kunyimwa posho na kunyanyaswa kama vile vitoto vya paka mwenye virusi bila msaada - DEAF EAR, BIG SILENCE.
Kufungwa watoto wa wakulima kwa kudai posho za kujikimu vyuoni na kuteswa na polisi na kufikishwa mahakamani bila huruma kwamba wazazi wao wapiga kura wake wanaumia mioyo yao kuona mtoto aliaga nyumbani kwenda chuo lakini badala yake anaishia kufungwa jela na kuteseka bila msaada - STUPID SILENCE AND A DEAF EAR.
Kelele za wananchi kwa mafisadi na wawekezaji wakorofi, wanao inyonya nchi hadi wengine hapa Arusha wanatorosha wanyama hai huko Moshono ambao wamejichimbia - CLOSED EYES, DEAF EAR AND SILENCE.
Watu kusingiziwa kesi na kubambikiwa makosa bila sababu - NO HELP, DEAF EAR, REJOICING.
Viongozi wake anao waweka ni GFs wake nini, mtu ana guts gani kuiba pesa za watoto wanao teseka vyuoni na wengine kufungwa kwa kukosa uvumilivu na yeye kula hizo pesa, haoni aibu, anategemea mgongo wa nani kama nguzo yake JK au Waziri gani? tuambieni na kama ni hivyo basi wale watoto walioko kifungoni waachiwe maana imedhihirika wazi pesa zilikuwa zinaliwa ndiyo maana hamkutaka vilio vyao kusikika kwa wananchi SHAME ON YOU ALL, NOT ONLY HER BUT ALL INCLUDING YOUR PRESIDENT.

Add new comment