Kiongozi wa upinzani Afrika Kusini akabiliwa na shutuma baada ya kuitembelea Israel

Mmusi Maimane. (picha credit:REUTERS)

THE Democratic Alliance (DA), chama cha upinzani nchini Afrika Kusini, kimejibu mashambulizi baada ya kiongozi wake Mmusi Maimane kuitembelea Israel.

Tukio hili ni baada ya chama tawala nchini humo, cha African National Congress, ANC, kutoa shutuma jana baada ya Maimane kuitembelea Israel.

Jarida la The Jerusalem Post lilipotoa taarifa kwamba kiongozi huyo mwenye mvuto wa upinzani alikuwa kwenye ziara ya siri, binafsi nchini Israel, siku mbili tu baada ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kuwataka wananchi wake kutoitembelea Israel.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, chama cha ANC kilisema kwamba kinatambua hasira na kuungana na “Waafrika Kusini wengine katika kushutumu ziara ya kiongozi wa DA Maimane kwenda Israel na kwa Waziri Mkuu wa Israel.”

“ANC pamoja na taasisi nyingine za kimaendeleo hakishangazwi na ziara ya DA huko Israel na kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu,” taarifa hiyo ilisema.

“Katika wakati ambao dunia,” taarifa hiyo iliendelea, “inaendelea kuwa na msimamo dhidi ya ujenzi wa makazi kinyume na sheria, ikiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa, inasikitisha kwamba DA inaunga mkono utawala wa  Israel badala ya kupinga ukiukaji wake wa sheria za kimataifa.”

“Shutuma kwamba chama cha DA kinafadhiliwa na wapenzi wa Israel ya kibaguzi inaonekana kuwa kweli,” iliongeza.

Pia ilikionya chama hicho cha upinzani kutowadanganya watu kwa kusema kwamba serikali ya Afrika Kusini na chama cha ANC vinamsimamo unaofanana na ule wa chama cha DA juu ya taifa la Wapalestina.

“ANC sio tu kwamba inaunga mkono suluhisho sahihi lakini pia, kwa miaka kadhaa kimehudhuria, kuunga mkono na kuandaa kampeni za kimataifa na watu wa Palestina. Sisi, tofauti na DA, tunataka vitendo vya kibaguzi vya Israel dhidi ya wakimbizi wa kiafrika, tunashutumu sera za kibaguzi za Israel na ukiukaji wa sheria za kimataifa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa makazi kinyume na sheria.”

ANC imesema inaunga mkono uamuzi wa serikali kukataa uhusiano wa aina yoyote na Israel hadi pale nchi hiyo itafuata sheria za kimataifa na mchakato wa amani. Iwapo kutaungwa mkono na watu wengi wa Afrika Kusini, ANC imesima itahakikisha kwamba serikali  itatekeleza sheria kali dhidi ya mataifa ambayo yanakiuka sheria za kimataifa na haki za binadamu.
Msemaji wa chama cha DA, Phumzile Van Damme alifoka kwamba Maimane alikuwa akiitembelea Israel na maeneo ya Wapalestina ili kusikiliza na kujifunza juu ya mgogoro huo.

“Yupo kule kuzungumzia jinsi Afrika Kusini inapaswa kuwa na jukumu la kijenga zaidi katika kuleta pande zote kwa ajili ya amani. “Pia yupo huko, kama mtu wa imani, kutembelea baadhi ya maeneo matakatifu ambayo yana maana kwake kiroho,” alisema.

Pamoja na kwamba Maimane alikutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na kiongozi wa upinzani, wa chama cha Zionist Union Mk Issac Herzog, Van Damme alisema kuwa mkutano na Rais wa Mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas ulipangwa, lakini ulifutwa na ofisi yake kutokana na ratiba yake kuingiliana na ile ya Rais.

“Maimane alikutana na maafisa wa Wapalestina huko Ramallah na Rawabi, wanaharakati wa haki za binadamu wa Kipalestina, pia wawakilishi wa ngazi za juu wa wafanyabiashara wa Kipalestina na Kiisrael kuzungumzia jinsi biashara inaweza kutumiwa kupeleka amani wakati siasa imeshindwa kupata maendeleo,” alisema.

Pamoja na shutuma nyingi, vyama vya marafiki wa Israel wa Afrika Kusini, SAFI na kile cha SA Zionist Federation, SAZF, vimemsifu Maimane kwa uamuzi wake kuitembelea Israel.

“Ni matumaini yetu kwamba uzoefu alioupata Maimane na mazungumzo yake na viongozi katika Mashariki ya Kati vitampa mtazamo anaohitaji kwa ajili ya kutafuta suluhisho la kudumu la amani katika ukanda huo,” alisema mwenyekiti wa SAZF Ben Swartz.

“Maimane anawakilisha maadili ya kweli ya Afrika Kusini ya mazungumzo na mawasiliano na ameonyesha maono na ujasiri katika nyakazi za upinzani mkali dhidi ya taifa la Israel.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *