
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Mkoa wa Arusha kuwa ni Aprili Mosi mwaka huu.
Uchaguzi huo unalenga kuziba nafasi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Jeremia Sumari aliyefariki dunia Jaruari 19 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva, jana, wananchi wametakiwa kutunza vitambulisho vya kupigia kura kwa kuwa hakutakuwa na uandikishaki badala yake daftari la kudumu la wapiga kura ndilo litakalotumika.
Alisema uteuzi wa wagombea utakuwa Machi 8, na kufuatiwa na kampeni kwa ajili ya uchaguzi huo kuanzia Machi 9 hadi Machi 31.
” Ifahamike kwamba, hakutakuwa na kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya chaguzi hizo. Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita ndilo litakalotumika katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki na chaguzi zote ndogo za madiwani.
Vituo vitakavyotumika kupiga kura ni vile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2010,”alisema Jaji Lubuva katika taarifa yake.
Kuhusu madiwani alisema kutakuwa na chaguzi ndogo za madiwani katika kata nane zilizopo katika halmashauri mbalimbalki nchini.
Alitaja Kata hizo kuwa ni Temeke vijibweni, Bagamayo Kiwangwa, Kirumba Mwanza, Bariadi Longangambilili, Dodoma Changómbe, Lizaboni Songea, Msambweni Tanga,Rungwe Kiwira.
Alisama wagombea udiwani watatueliwa machi 5 mwaka huu na kufuatiwa na kampeni Machi sita hadi machi 31.
Alisema NEC itaweka orodha ya wapiga kura katika vituo vya kupigia kura kwa muda wa siku saba kuanzia Machi 25, 2012 hadi 31.
Toa maoni yako