Bosi DAWASCO ametuchosha, Wizara ya Maji itusikilize

Mhariri, Kupitia gazeti lako tunaomba kufikisha malalamiko yetu, sisi wafanyakazi wa DAWASCO. Kwa muda mrefu sasa tumekuwa haturidhishwi na mwenendo wa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni yetu.

Kiongozi wetu huyo amekuwa na uhusiano na mmoja wa wafanyakazi mwenzetu kiasi cha uhusiano huo kuingilia utendaji wa wafanyakazi wengine na hata kupandikiza chuki.

Kutokana na uhusiano huo kumekuwa na upendeleo maalumu kwa mfanyakazi huyo mwenzetu ikilinganishwa na sisi wengine. Kumekuwa na hali ya wafanyakazi kufanya kazi kwa hofu kutokana na kauli za mara kwa mara za kutishiwa kufukuzwa kazi.

Hali hii iliwahi kutokea siku za nyuma na kusababisha takriban wafanyakazi 500 kuondoka na sasa umekuwa mwendelezo huo huo, watu wengine wanaacha kazi kutokana na kushindwa kuvumilia hali hiyo.

Tunapenda kuhoji; je, kufukuza na kuajiri mara kwa mara hali inayosababisha kampuni kukumbwa na kesi zisizo za lazima kuhusu masuala ya kazi na ajira ndiyo ufanisi unatarajiwa na Serikali Kuu? Tunasikika kutokana na ukweli kwamba, kwa sasa Dawasco ni kati ya kampuni zenye migogoro mingi tofauti na hali ilivyokuwapo awali.

Kupitia kwako Mhariri tunaomba Serikali kupitia Wizara ifuatilie kashfa hii iliyoko wazi katika ‘korido’ za Dawasco ili kutafuta ufumbuzi

6 thoughts on “Bosi DAWASCO ametuchosha, Wizara ya Maji itusikilize”

 1. mwanananchi mdadisi says:

  kiongozi mkubwa huyu anasikiliza majungu hasa ya mahawala zake,pamoja na watu wakabila lake,bila kuyatafakari kwa kina,anawatoa kazi watu bila ya sababu za msingi.mfano,mwezi wa 11 mwaka jana amewatoa kazi watu zaidi 5 bila ya sababu za msingi.sababu za ukweli ni kwamba kuna watu wa store ni nyumba ndogo zake,wezi na wanafahamika na shirika,wanajifanya wasafi,hawajui kazi,wala rushwa wakubwa,wana bifu na wastore wenzao hivyo wamepeleka majunu kwa mkubwa,kwa kuwa hajui afanyalo,amepokea majungu na kuwatoa kazi,akijua aliowabakisha ni wachapa kazi,waharibifu wa shirika na hata elimu hawana ni ile ya mngumbalu tu .pia kuna ndugu zake upande wa ufundi elimu yenyewe ni yeboyebo,hawataki hata kujiendeleza,wanaona nafasi za juu zote wanashika wasomi wakisasa ambayo ni haki yao kweli,sasa wao wanaona kama wanaonewa wanapeleka majungu kwa ndugu yao ili awape wao zile nafasi,bwana mkubwa huyu bila kutafakari haya aliwatoa kazi wataalam ambao walikuwa wanasifika na shirika na wateja kwa uchapaji kazi wao kwa majungu na fitina za ndugu zake pamoja na wale wasio jiamini na nafasi alizowapa kutokana na elimu zao kuwa chini wanaamua kufanya majungu na kuwapa mazingira magumu ya kazi wale wachapa kazi.
  Kiukweli kiongozi mkubwa wa shirika Dawasco anaburuzwa na;
  Nyuma ndogo zake,
  ndugu zake wasio na elimu kutaka madaraka,
  Jopo la watu mbalimbali wasio na elimu,akilifanyia kazi hili huenda akafanya vizuri.

 2. KICHUMU says:

  Hayo mambo ya Dawasco sio kwa wafanyakazi hata kwa sisi wateja wa KINONDONI MKWAJUNI tunapata tabu na huyu Meneja wa sasa ambae kwa kushirikiana na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM ameamua kukata maji kwa wateja wa muda mrefu na kuweka hudumahiyo kwa hao wajumbe ili aifanye serikali ichukiwe kwa upuuzi wa watu wachache mmoja wapo ni huyu Meneja wa DAWASCO KINONDONI na huu ndio mpango maalum aliouweka ili kwa namna moja au nyengine ahujumu mapato ya shirika maana anpingana na SERA ya maji isemayo ‘MAJI NI UHAI KWA KILA KIUMBE’ sasa inakuwaje kuondoa huduma kwa wateja wengi na kuweka kwa wajumbe wa nyumba kumi tena bila taarifa

 3. Msomaji wetu says:

  Jamani mimi naomba wizara ya ajira iwe inafanya ukaguzi kwenye hayo mashirika.kwa sababu wafanyakazi wa dawasco hawana lugha nzuri kwa wateja hasa mapokezi pamoja na wasoma mita, ina bidi serikali iwemkakati wa kuhakikisha wanalipwa mishahara yao kutokana a bili za wateja la sivyo wataendelea kuwa na viburi katika kazi na kuipatia serikali hasara.

 4. Msomaji wetu says:

  kafanya viuri

 5. Msomaji wetu says:

  Wizara ya maji tunasikitika sana- Mbunge achinja ng’ombe

  17 April 2015
  KATIKA kile kinachoweza kuelezwa kuwa changamoto ya viongozi wa kisiasa na wananchi kutambua majukumu na dhamana za viongozi wa kuchaguliwa, Mbunge wa Jimbo ……………….., amekuwa akiwafanyia sherehe wananchi wa kila kata katika jimbo hilo kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake za uchaguzi.
  Wakati maji ya kunywa ngombe/matumizi ya nyumbani kwenye Lambola Ibindo hakuna ,Cha kusikitisha Halmashauri kwimba ili ingia mkataba na Mkandalasi asiye na uwezo au makusudi ambaye alipewa kazi ya kutoa matope kwenye Lambo la Ibindo kwa kiasi cha sh.120 millioni , badala yake akalitoboa tuta la kukigia maji akashindwa kulitegeneza matokeo yake mvua imenyesha tuta limetoboka na maji hayakaliki, tunaomba serikali itupe jibu kuhusu maji katika kijiji cha Ibindo ambapo mpaka sasa hakuna uvunaji wa maji mwaka huu ,hivi nani atatuletea maji wakati wa kiangazi? tunaomba serikali ichukue hatua kama wizara iko makini.
  Mmoja wa wananchi wa jimbo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Manoni anasema kitendo hicho ni sawa na kuwakejeli wananchi kwa kuwa kuwafanyia watu sherehe si sehemu ya majukumu ya mbunge sisi tunataka maji na siyo kula nyama.

 6. stephen says:

  Na mimi leo naingia uwanjani kueleza yanayotusibu wakazi wa Mbezi kwa Msuguri. Kwetu maji hawatufulii kabisa. Na inaonekana kuna hujuma za makusudi kuharibu miundo mbinu ya mabomba ili tusipate maji haya hata siku moja kwa juma kulingana na mgao uliopo. sisi mgao wetu ni siku ya jumanne. Meneja huyu inaonekana ana mkakati wa kutuuzia maji kupitia magari ya maji, maji yenyewe yanasafirishwa kupitia matanki machafu. Alafu kwanini tuuziwe maji kupitia ktk magari na sio kupitia mabomba tuliyoungiwa kwa gharama kubwa ya kiasi cha laki tano na ushee?. Meneja huyu ameshindwa kazi , hivyo atumbuliwe mapema ili vifo visitokee kwa kunywa maji amabayo usalama wake una mashaka, maji yanayosafirishwa kupitia magari hayo.Natanguliza shukrani zangu kuwa kilio chetu kitasikiwa haraka.

   

   

  Na

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *