Magufuli: Ruksa kuoana bila cheti cha kuzaliwa

RAIS John Magufuli leo amefuta agizo la Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe, la kutaka wanandoa wawe kwanza na cheti cha kuzaliwa kabla ya kuoana.

Akizungumza na wandishi wa habari katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Magufuli alisema kwa sasa idadi ya Watanzania wenye vyeti vya kuzaliwa ni ndogo sana kiasi kwamba kuweka sharti hilo kwa wanandoa kunaweza kusababisha usumbufu mkubwa.

Alisema mpaka sasa, Watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa hawazidi asilimia 20 na wengi wasio navyo ni wale walio vijijini ambako upatikanaji wa huduma hiyo bado hauridhishi.

" Kwa hiyo, ndugu zangu Watanzania, msiwe na wasiwasi wowote. Endeleeni na utaratibu wenu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na kama kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na cheti za kuzaliwa ndipo aoe au kuolewa, nitamuelekeza waziri Mwakyembe apeleke bungeni kikarekebishwe, alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *