Hifadhi: Makala

Tumechoka kuchezewa

TAIFA linapoingia katika vita ya kiuchumi kulinda na kutetea rasilimali zake, Watanzania na hasa vijana na wasomi wanatarajiwa kuchukua nafasi yao katika kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinabaki salama kwa manufaa ya vizazi vyake. Huu ndiyo umekuwa msingi wa Tanzania, wazee wetu waliposema tumeonewa kiasi

Tunavuna tulichopanda, nasimama na Rais wangu

KILA siku nashuhudia wananchi wenzangu wakikalamika. Natamani kujibu. Naacha. Natamani kuwakumbusha wananchi wenzangu. Naacha. Nasema mbona sisi ni wepesi wa kusahau? Natamani kuwakumbusha wabunge wenzangu. Naacha. Nasema name sasa nipo kwenye serikali. Ni mtunga sera, ni mfanya maamuzi, nikisema watasema huyu ni 'naibu waziri'. Lakini

Barua ya wazi kwa ndugu Muhingo Rweyemamu

Kwako ndugu yangu, Muhingo Rweyemamu. Salaam sana, natumaini kwa neema za Mungu unaendelea vyema, japo kupitia kwa wenzangu kwenye mtandao wa wahariri Tanzania yaani TEF nimefahamishwa kuwa unaumwa na muda mwingi upo nyumbani unapumzika. Nakuandikia waraka huu nikiwa Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo nipo kikazi. Naamini

Meremeta: Mradi wa kifisadi uliokomba dhahabu na kukwapua benki

JE, haikusemwa na Wahenga kwamba, ukishangaa ya Mussa, utastaajabu ya Firauni? Usemi huu una mantiki pia kwa zama zetu hizi kwamba; “Ukishangaa ya makanikia ya Kampuni ya Acacia, utastaajabu ya Meremeta”. Wakati Acacia walikuja na mtaji wao kuchimba dhahabu wakaparanganya mambo ili kutupora madini ya

Kama ningekuwa Rais Jacob Zuma, ningejiuzulu

IJUMAA iliyopita Rais Jacob Zuma alikuwa mgeni rasmi katika kumbukumbu ya Siku ya Mtoto wa Afrika, maadhimisho ambayo kwa Afrika Kusini yamepewa heshima kubwa na siku hiyo kufanywa kuwa siku ya mapumziko. Hii ni kwa heshima ya watoto ambao walipoteza maisha yao Juni 16, 1976,

Taarifa ya Twaweza na afya ya upinzani

SIJAWAHI hata siku moja kutamani kuishi katika Tanzania ambayo nguvu ya vyama vya upinzani inapungua kwa sababu naelewa athari za kukaa katika nchi ya ukiritimba wa chama kimoja na fikra za aina moja. Na ni kwa sababu hiyo, taarifa ya Twaweza iliyobatizwa, ‘Mwisho wa Mwanzo?

Usifungie, nenda mahakamani, bainisha kosa, ujibiwe

M SOMAJI atakumbuka kwamba nilipoanza mfululizo huu kuhusu kile Chachage alichokiita “collective imbecilization” niliijadili dhana pana ya “Baba,” toka ndani ya kaya zetu, makanisani, serikalini, hata mbinguni. Kuanzia “Baba Mzazi,”  kupitia kwa “Baba Mlezi,”  “Baba wa Taifa, ” kwenda kwa“Baba Paroko,” “ Baba Askofu” na

Siku Kagame alipopitishwa kugombea Urais

DAKIKA 14 baada ya Mwenyekiti wa chama cha Rwanda Patriotic Front (RPF), Paul Kagame, kupanda jukwaani na kuanza kuzungumza, mmoja wa waandishi wa habari walioketi jirani yangu alichana karatasi kutoka katika daftari lake la kumbukumbu (notebook) – na kilichofuata kimebaki katika kumbukumbu zangu. Karibu wajumbe