Hifadhi: Makala

Lindiwe Sisulu anapoitabiria ANC kuanguka 2019

JINA la Walter Sisulu ni maarufu sana ulimwenguni kote. Huyu alikuwa mpigania uhuru wa Afrika Kusini ambaye harakati zake zilimfanya awekwe gereza moja na mzee Nelson Mandela huko katika kisiwa cha Robben kilichopo Cape Town hapa Afrika Kusini. Walter Sisulu alifariki mwaka 2003 na kuacha

Wazazi wana wajibu kuboresha Shule za Kata

MSOMAJI wa safu hii kutoka mkoani Mwanza aitwae Joseph, wiki iliyopita aliniandikia ujumbe  mfupi wa simu (SMS) akinitaka niwe pia nazungumzia masuala ya kitaifa kuliko yale ya Mkoa wa Kilimanjaro tu kila wiki. Baadaye nilimpigia simu na kumweleza kuwa mwandishi wa habari anayejikita kwenye uandishi

Mfalme akitinga utupu hadharani, ni uhaini kutosema yuko uchi

HAIKUWA kwa bahati mbaya wala kutotarajiwa, bali kwa stahiki yake na haki; pale mheshimiwa Mikogo Mingi, mwana wa Mfalme Mingi Mikwara, aliposhika kiti cha ufalme kumrithi baba yake aliyeitwa na Mungu katikati ya mwezi Machi mwaka huo. Mfalme huyo kijana ambaye kabla ya hapo hakujisumbua

Kama mnataka ‘Ukawa’, wakati ni huu

MWAKA 1995, Tanzania ilifanya Uchaguzi Mkuu wa kwanza tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi. Wakati huo, ‘kizazi cha dhahabu’ cha upinzani kilikuwa tayari kwa mapambano. Nakiita kizazi cha dhahabu kwa sababu naamini wengi wa waliokuwa vinara wake walikuwa watu ambao ama walikuwa wamepigania upinzani

Madaraka yametafuna unyenyekevu wake?

MKONO mmoja huosha mkono mwingine, hii ni busara inayopatikana katika msemo wa kilatini “manus manum lavat”. Nitatumia dhana ama busara hii kujadili uongozi wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli, ikiwa ni takriban miezi 20 tangu nikutane naye na kufanya mahojiano katika Hoteli

Rais Magufuli ameishiwa pumzi ya kutumbua majipu?

NIANZE makala hii kwa kutoa salamu za rambirambi kwa familia za askari wanane wa Jeshi la Polisi waliouawa kinyama wiki iliyopita, wilayani Kibiti, mkoani Pwani. Huu ni msiba wa kitaifa, japo hakuna maombolezo ya kitaifa – sijui kwa vile hatuthamini uhai wa Watanzania wenzetu au

Rais Zuma ataweza kuruka kihunzi hiki?

WIKI tatu zilizopita zimekuwa ngumu kwa Rais Jacob Zuma kutokana na kuandamwa na shinikizo kutoka ndani na nje ya chama chake cha African National Congress (ANC), ndani na nje ya serikali, na pia ndani na nje ya Afrika Kusini kutokana na mabadiliko ya baraza lake

Tazama tulichoifanyia dunia

KWA kitambo cha pungufu ya dakika saba, Michael Jackson, kwa ufundi na usanii mkubwa, anatueleza na kutuonyesha uovu dhidi ya mazingira. Ni katika wimbo na filamu “Earth Song” ya mwaka 1995. Kwa dakika hizi chache, mtazamaji hupelekwa sehemu tatu tofauti – Ulaya, Afrika na Amerika