Hifadhi: Makala

Hapo komesha tu!!

Uzitoni Street, Bongo. Mpenzi wangu wa moyo, Yaani mpenzi, nakuwazia kila saa. Napenda kujua unafanya nini, unajisikiaje, umweza kupika nini (tehe tehe), maisha yako kwa ujumla … kila kituNatamani kuwa na wewe tuweze kugawiana mawazo yetu, mioyo yetu, raha zetu na hata taabu zetu. Ujue

Buriani ‘Mnyakaya’ Askofu Isuja, mbegu ulizopanda zitastawi

DHAMIRA na utashi wa kujitegemea ndiyo hazina na urithi wanaobaki nao wananchi wa Dodoma kutoka kwa Askofu mstaafu wa jimbo hilo, Hayati Mathias Isuja, watakapokuwa wanampumzisha Jumatano hii katika nyumba yake ya milele. Hayati Askofu Isuja (86) aliyefariki dunia wiki iliyopita katika Hospitali ya Mtakatifu

TCRA ijisafishe na kusimamia sheria, hali mbaya Instagram

MAJUZI nilibandika habari mbili kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook zilizohusu ufisadi na umasikini. Habari moja ilihusu taarifa za vyombo vya habari kwamba wabunge wameshtushwa na ripoti inayoonyesha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetumia shilingi bilioni 18 kwa ajili ya mafunzo, semina na warsha. Niliambatanisha

Acheni kumwomba Samatta ‘selfie’

UMEWAHI kupitia akaunti za mitandao ya kijamii ya baadhi ya mastaa wetu wa soka nchini kila Mbwana Samatta anapofunga bao katika klabu ya Genk? Kama hujawahi jaribu kuzifuatilia. Kuna kitu utakiona. Akaunti nyingi zinavutia kuzisoma. Inafika muda unatamani kila leo Samatta, afunge ili uzipitie akaunti

Ya Mwajuma na kina Msekwa

KATIKA uhai wangu nimekutana mara moja tu na Pius Chipanda Msekwa. Sijui kama yeye anakumbuka. Kwa hakika, hana sababu ya kwa nini akumbuke au anikumbuke ingawa pengine hatopasahau nilipomkuta Jumatatu ya Machi 11, 2002 jua lilipokuwa limekwishatua. Ama mimi siwezi kusahau mahala tulipokutana. Wala siwezi

Ndugai, Majaliwa matatani

WABUNGE wamepania kuwaweka kikaangoni Spika wa Bunge, Job Ndugai na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kwa sababu tofauti katika Mkutano wa Bunge ulioanza Jumanne wiki hii, Raia Mwema limeambiwa. Wabunge hao wanatarajiwa kumbana Ndugai kutokana na kile kinachodaiwa kuwa “amekuwa upande wa serikali kuliko wabunge” katika

Nchi ilivyotafunwa mbele ya Kikwete

RAIS Dk. John Magufuli ana kazi kubwa ya kukabili kundi la ubia wa wanasiasa na watendaji, matajiri wakubwa, walionufaika na mfumo wa hovyo wa wizi na ‘dili’ ulioshamiri wakati wa utawala wa Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete. Raia Mwema limeambiwa ya kuwa awamu

Kwenye hili, tujiulize tumefikaje hapa

KWENYE toleo hili la gazeti la Raia Mwema, kuna habari kuu inayoeleza namna wanasiasa na watumishi wa umma walivyoingia ubia katika kufisidi mali ya umma. Ni habari ya kusikitisha inayoeleza kuhusu uozo ambao nchi yetu ilikuwa imefikia. Picha inayojitokeza ni kwamba uongozi na utumishi wa