Manchester United yatajwa kama klabu tajiri zaidi duniani kwa sasa

Manchester United imetengeneza fedha zaidi ya klabu yoyote ya soka duniani msimu uliopita, kulingana na taarifa iloyochapishwa na Deloitte, kampuni nguli ya ushauri wa fedha duniani.

United imeipiku Real Madrid – ambayo ilikuwa ikishikilia nafasi hiyo kwa miaka 11 mfululizo – baada ya kukusanya mapato ya jumla ya euro milioni 689 (sawa na shilingi trilioni 1.66) wakati wa msimu wa 2015 – 16.

Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza imeshuhudia mapato yake yakiongezeka kwa kiasi cha euro milioni 100 (sawa na bilioni 241).

Mauzo ya jumla ya klabu 20 tajiri zaidi katika kipindi hicho yamekua kwa kiasi cha asilimua 12, hadi euro bilioni 7.4 kwa jumla, ambayo ni rekodi mpya.

Ni mara ya kwanza kwa Manchester United kukaa kileleni mwa klabu tajiri duniani tangu msimu wa 2003-04.

Real Madrid imeanguka hadi nafasi ya tatu, nyuma ya mpinzani wake Barcelona, ambayo imebaki katika nafasi ya pili.

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich imepanda hadi nafasi ya nne na Manchester City pia imepanda hadi nafasi ya tano – baada ya kuwa na kipato cha eurp milioni 524.9 (sawa na trilioni 1.2) – kutoka euro milioni 463.5 wakati wa msimu uliopita.

Ni mara ya kwanza kwa Manchester City kuingia kwenye tano bora.

Timu nane  zinazoshiriki ligi kuu ya Uingereza zimeingia katika klabu 20 za juu.

Mabingwa Leicester City (ya 20) inaingia kwenye nafasi hiyo kwa mara ya kwanza.

Arsenal, Chelsea, Arsenal, Chelsea, Liverpool na Tottenham zimebaki katika nafasi za  saba, nane, tisa na kumi na mbili, wakati West Ham ikiwa katika nafasi ya 18.

Dan Jones kutoka Deloitte, alisema mapato ya Manchester United yalipatikana kutokana na ukuaji mzuri kibiashara.

Aliongeza, “Katika miaka ya karibuni, uwezo wao katika kupata wenza kibiashara kwa thamani ambayo inazidi ile ambayo wapinzani wao wanaweza kuipata imekuwa ni kitu muhimu katika kuiwezesha klabu hiyo kurejea katika uongozi wa ligi hiyo ya fedha.

“Baada ya kusema hayo, watakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa Barcelona na Real Madrid katika kubaki katika nafasi hiyo mwaka ujao, kutokana na kukosa Ligi ya Mabingwa Ulaya, na pia kushuka kwa thamani ya sarafu ya pound dhidi ya euro, wakati vilabu vingine vikiingia sokoni na kudai kupewa makubaliano kama yale ya United.”

Msimamo wa ligi ya Fedha ya Deloitte msimu wa 2015-16  – kumi bora

Timu (nafasi msimu uliopita)

Kipato kwa €m  (2015-16

Kipato 2014-15

1 (3) Manchester United

689 (515.3)

519.5 (395.2)

2 (2) Barcelona

620.2 (463.8)

560.8 (426.6)

3 (1) Real Madrid

620.1 (463.8)

577 (439)

4 (5) Bayern Munich

592 (442.7)

474 (360.6)

5 (6) Manchester City

524.9 (392.6)

463.5 (352.6)

6 (4) Paris St-Germain

520.9 (389.6)

480.8 (365.8)

7 (7) Arsenal

468.5 (350.4)

435.5 (331.3)

8 (8) Chelsea

447.4 (334.6)

420 (319.5)

9 (9) Liverpool

403.8 (302)

391.8 (298.1)

10 (10) Juventus

341.1 (255.1)

323.9 (246.4)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *