TUMEUFUATILIA kwa karibu mgomo wa madaktari. Yapo madai ya msingi kabisa yanayohitaji uamuzi wa mapema na yako mengine, ambayo si madai, na haya yanaweza kupatiwa maelezo mbele ya safari.
Tunachokiona katika suala hili ni kwamba, kwa bahati mbaya sana, baadhi yetu wanashabikia mgomo huu. Inawezekana kwamba hawa mashabiki wa mgomo, kwa kipindi hiki cha mgomo, hawana wagonjwa walio mahututi, wanaopaswa kupata huduma ya haraka kitabibu.
Au, kama mashabiki hawa wa mgomo wanao wagonjwa wanaowauguza, basi wana uwezo mkubwa kifedha wa kuwapeleka wagonjwa wao katika hospitali binafsi au hata za nje, badala ya hizi za umma ambazo ndilo kimbilio la Watanzania wengi.
Hakika hii si mara ya kwanza kwa madaktari kugoma. Lakini ni wazi kwamba mgomo wa safari hii umekita sana, hiyo ikitishia kwa viwango ya juu kabisa haki ya kuishi ya Watanzania wengi. Na sote tunajua haki ya kuishi ni haki ya msingi, haipaswi kuhujumiwa, kwa sababu yoyote ile.
Ni kwa ajili ya umuhimu wa uhai wa kila Mtanzania tunasema kwamba kila pande husika za mgomo huu zimepeleka ujumbe uliokusudia na sasa umetosha. Tungependa, sasa, kuona suluhu ya jambo hili ikipatikana haraka iwezekanavyo.
Tunaamini kwamba wahusika wa pande hizi wanaweza kukaa na kuzungumza kwa nia ya kuepusha madhara zaidi, ambayo kimsingi, ni mauti, kwa umma ambao sasa umenaswa katikati ya pande hizi mbili usipate pa kukimbilia.
Hatupendi kuendelea kuona picha za magari ya wagonjwa yakirejea yalikotoka na wagonjwa mahtuti, kwa vile tu hao ambao wangewashughulikia wagonjwa hao hawakufika kazini. Hivi tunataka wafe wangapi ndipo tupate ushahidi kwamba mvutano huu hautusaidii sana?
Kadhia hii, polepole, inaelekea katika tafsiri ya kuwa huu si tu ni mgono dhidi ya Serikali, bali ni mgomo dhidi ya maisha ya wanyonge. Ukifika mahali ukawa ni mgomo dhidi ya wagonjwa, utakuwa umeweka doa la kudumu miongoni mwetu, na sisi tusingependa hali idhoofike hadi kufika huko.
Ndiyo maana tunahimiza kwamba pande husika ziendelee na njia za kutafuta mwafaka ikingali mapema, vinginevyo, jinsi muda utakavyopita, maafa zaidi yakatokea, wa kuwajibika wanafahamika.
Maoni ya Wasomaji
Hivi kweli nchi yenye uongozi
Hivi kweli nchi yenye uongozi thabiti inaweza kuacha watu wake kuendelea kufa? Tanzania inaongozwa na nani? Kama tuna rais aliyechaguliwa na wapiga kura, ambao miongoni mwao wameshapoteza maisha kutokana na yeye na serikali yake kushindwa kusimamia suala la madakrari wetu, basi atatue tatizo la madaktari MARA MOJA!
The value of life is
The value of life is extremely uncomparable 2 any thing pls watoto wanafundishwa kuongea basi wakubwa msijifunze kukaa kimya tulimalize swala hili kwa mazungumzo haraka so that we can save LIFE muhas medical student 1yr.
Kwa mara nyingine ombwe la
Kwa mara nyingine ombwe la uongozi limejitokeza kitaifa. Ndugu zetu wanakufa kama siafu, na huku watawala -serikali ya CCM na bunge letu la wachumia tumbo wako bize kulumbana juu ya posho ya makalio! Isitoshe Vasco da Gama hakuacha kuchukua kafursa ka kwenda kutanua Davos na Addis-kubadilisha hali ya hewa na suti. Hatuna viongozi ila tunatawaliwa kwa nguvu na watu waliojitawalisha kwa nguvu za dola na hela. Wanatudharau na hata tukifa hawapepesi kope. Kwa hali hii, ufumbuzi wa hili tatizo ni ndoto. Tumrudie tu Mungu ili atutayarishie makao mema huko kwake kwani wa kututibu hapa duniani Tanzania ili tusife haraka kwenda kwake wamenyimwa haki zao na serikali.
raiamwema tunasubiri siku
raiamwema tunasubiri siku mtakuwa na gazeti la kila siku,redio na Tv hapo mtaweza kuwafikia watu wengi zaidi
Inasikitisha kuona vifo vya
Inasikitisha kuona vifo vya wenzetu watanzania wasio na hatia maishani kwa mgomo wa madaktari. ila tu mkumbuke anae sababisha vifo hivi ni serikali ambayo inakiongozi mwenye kutoa amri ya mwisho.
huwa nacheka nikisikia serikali inasema haina pesa. ivi ni nani wanafikili asiye jua nini kinapatikana kutokana na migodi ya hapa tanzania. naomba niwataarifu watanzania wenzangu madini ,mbuga za wanyama na bandari bila kuisahau T.R.A kwa kweli kuna mapato mpaka huwa fedha nyingine zinatumika kwa matumizi yasiyo na kichwa wala miguu.
kama mtakumbuka ndege iliyotaka kutekwa na majambazi mmoja aliuliwa wakiwa na nia ya kuiba ile gold iliyokuwa inasafirishwa na wazungu KWENYE NDEGE, kwa ufupi ilikuwa ni TANI MOJA YA GOLD AMBAYO NI SAWA NA KILOGRAM 1000. JE KAMA GRAM MOJA NI SHILINGI ELFU 70,000 ,KILO MOJA INA GRAM 1000 AMBAZO NI SHILINGI MILIONI 70 YA KITANZANIA. KWA MAANA IYO TANI MOJA NI BEI YA KILO MOJA MARA KILO 1000. AMBAYO ITAKUWA 70,000,000 X 1000 = 70,000,000,000/=. JAMANI IVI HIZO BILIONI 70 ZINASHINDWA HATA KUTAWANYWA KWA MADAKTARI WA TANZANIA. KAMA KIKWETE INCHI IMEMSHINDA BORA AJIUZURU MAANA MAPATO KAMA HAYA ANAYAACHA YANAZOLEWA TU NA WAZUNGU MI SIONI UMUIMU WAKE .
NIJE KWENYE MBUGA ZA WANYAMA KWA YEYOTE ATAKAE WEZA EMBU NAOMBA UKAKAE GETI LA MBUGA YA MANYALA NA KISHA UULIZE MZUNGU MMOJA ANAINGIA KWA SHILINGI NGAPI KISHA HESABU GARI NGAPI ZITAINGIA SIKU IYO NA WAZUNGU WANGAPI KISHA PIGA HESABU YA MAPATO KWA MWEZI. HUU NI UCHIZI NINAPOSIKIA SERIKALI INASEMA HAINA PESA YAKUWALIPA MADAKTARI.
KAMA HAITOSHI NAOMBA WATANZANIA MFANYE UTAFITI PALE BANDARI BEI YA KONTENA IKILALA BANDARINI IKISHA PITA SIKU SABA TANGU ISHUSHWE HUWA INATOZWA SHILINGI NGAPI KWA SIKU, KISHA OMBA AMA KISIA IDADI YA KONTENA UNAZOZIONA KWA MACHO KWAKWELI NI VICHEKESHO SERIKALI IKISEMA HAINA PESA.
T.R.A JAMANI EEH IVI TUANZE TU KODI KWA MWAKA ZA BAJAJI NA PIKIPIKI, KISHA DALADALA, MABASI YA MKOANI, MAFUTA IKIWEMO DIESEL,PETROL,MAFUTA YA TAA, BADO MAGARI YA WATU BINAFSI, HOTEL, GUEST HOUSE, MADUKA , MAGARI YANAYOTOKA NJE YA NCHI NA KUINGIA YENYE BIDHAA NA YALE YA WATU BINAFSI....NA MENGINEYO, JAMANI KWA KWELI MI NAONA KIKWETE AENDE TU AKAPOTELEE ULAYA KAMA BALALI TUJUE AMEKUFA MAANA NI UJINGA SI UJINGA UPUUZI SI UPUUZI YANI KWAKWELI NI INASIKITISHA SI MASWALA YA KUCHEKA KABISA.
MI NAISI UYU JAMAA KATUMWA KULETA VITA TANZANIA SIUELEWI UONGOZI WAKE.
Ndugu mhariri, imetangazwa
Ndugu mhariri, imetangazwa jana bungeni kwamba mgomo umeisha, sasa huu ujumbe wako unamanisha bunge lilidanganywa?
Kilio cha madaktari kimekuwa
Kilio cha madaktari kimekuwa cha muda mrefu sana.Udaktari siyo laana.wanastahili kulipwa
hakizao, na maisha bora ya kazi.Hawapaswi kulaumiwa kabisa.Wananchi wanapaswa kujilaumu
wenyewe kwa kuichagua serikali isiyo sikia.
JOHN BWIRE unapaswa kuwaomba msamaha MADAKTARI na wasomaji wa Raia Mwema kwa kuupotosha umma.
Vita vya panzi furaha ya
Vita vya panzi furaha ya kunguru!!!!!!!!!!!!
Hapa hakuna utawala bora wala uongozi bora, wa kuchimba mizizi ya tatizo mbali ya wahusika wa kwanza, yaani Katibu Mkuu Wizara ya Afya kutaka kuonyesha ubabe tu. Kiongozi anayejiamini huwa hatishi tishi, hutafakari pia jambo bila jazba.
Mbona hatujaona maneno makali toka kwa Wabunge kama waliotowa kwa Magifuli?, mbona hatujaona maneno ya kupoza yaliyotolewa na raisi kwa Magufuli alipotaka kusafisha maeneo kando ya barabara. Huu ni unafiki na si uongozi bora.
Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni!!!!!!!!!!!
KUGOMA NA MAADAMANOSIYO NJIA
KUGOMA NA MAADAMANO
SIYO NJIA YA KILA MTU KUPATA HAKI
WANANCHI WAFIKIRI ZAIDI
NA BONIFACE MAZIKU:
INATAKIWA KILA BINADAMU KATIKA NAFASI YAKE AFIKIRI NAMNA YA KUCHUKUA HATUA KUPATA HAKI YAKE IKIPOTEA.
KUGOMA SIYO NJIA NZURI KWA DAKTARI KUPATA HAKI ZAO HATA KIAPO CHA KAZI YAO KINAKATAZA
Je mama akigoma kujifungua mototo ili apate haki zake kwa mme wake, itakuwa ni dhambi ya baba au mama? Aliyeua ni mama aliyegoma kuzaa na kuuwa au ni baba ambaye kachelewesha huduma kwa mama? Tutafakari zaidi.
KUGOMA KUTIBU SI NJIA NJEMA KWA DAKATARI KUDAI HAKI ZAKE:
Madakari wakumbuke wamekiuka kiapo cha ajira pia wamevuka misingi ya uwema au miiko ya binadamu ya kufuata ili atende mema.
Kila tendo jema analotenda binadamu lazima awe nia au lengo zuri, njia atakayoamua kutenda ili afikie lengo lake iwe nzuri na mazingira ya pale anapotendea kitendo hicho yaruhusu.
Sasa dakatari ana haki ya kupata maslahi yake na anayo haki ya kudai maslahi yake lakini akitumia njia ya kugoma na kuuwa wagonjwa njia hiyo inafanya kitendo chake kiwe kibaya hakikubaliki katika jamii na ni dhambi kwa Mungu.
KUTANGAZA KWA NGUVU KATIKA JAMII HAKI ZA MADAKTARI KUNAINUA VURUGU NCHINI NA KULETA LAWAMA KWA WATU WASIOHUSIKA NA KUWAUWA WAGONJWA MAHOSPITALINI
Sasa madkatari wamegoma na kutangaza mbele haki zao na kwa kuwa ni haki halali wamepofusha jamii ibaki inawapa hongera kudai haki zao na kusahau kujadili kwamba njia waliyochagua kudai haki yao si nzuri na ni njia ya kiuaji. Zaidi ya hayo wanazidi kusema uongo kuwa wamerudi kazini na huku hawajarudi kutoa huduma hii inatoa picha kuwa tuna watumishi wa serkali ambao wako makini kusema uongo halisi uongo ambayo unafanya wangonjwa wengine waende kupata huduma zao huku kumbe hawajaanza kutibu na watu hao wengine wanazidi kufa. Uongo huu sasa kuzidi kuuwa unazidi kuinua hasira ya jamii na matokeo yake ni kuleta vurugu nchini na kuvunja amani wafe watu wengi katika vurugu.
OMBI KWA MADAKATARI NA WABUNGE
Tunaomba madaktari wajirudi kuacha mgomo ni dhambi na ni kinyume cha misingi ya maadili mema, kugoma kwa mwanafunzi wa shule ya msingi na kugoma kwa daktari ni vitu viwili tofauti ni sawa na kumuona piloti wa ndege yuko hewani anaamua kugoma ili alipwe mshahara asipolipwa haraka basi ndege inaanguka nay eye mwisho atakufa.
Tuna omba nao wabunge wakubuke kuwa kutokuwa na kauli ya wazi kuhusu posho zao kuziongeza, inabidi wakubali wazi kuwa wako tayari kutoongeza posho zao maana hali ya nchi ni duni, na majanga ni mengi yanayojitokeza ambayo yanadai nchi izidi kulipia au kufidia vitu ambavyo ni vya dharura. Pasipo kutoa kauli ya wazi wabunge watazima tatizo la madakatari na watainuka kundi jingine maana wanajua kuwa pesa ipo kama wabunge wanajipa posho kubwa.
KUNA HATARI KAMA TAIFA HALITOI MWONGOZO WA OMBI LA MADAKTARI NA POSHO ZA WABUNGE KUONGEZEKA JAMBO HILI:
Wasipotoa kauli ya msimamo wa kimaadili wabunge pamoja na madatari, watawakwaza wananchi wa kawaida na matokeo yake fujo zitakuwa nyingi kwa kwakuwa si kila mtu anao uwezo wa kutafakari mambo haya kwa uangalifu panapokuwa na dharura za mauaji. Ndiyo maana wengine wanaenda kuandamana bila kudadisi kiasi Fulani kosa la madaktari.
WITO KWA WOTE:
MWISHO NI WITO WANGU KUWA VIONGOZI WAKAE KATIKA KWELI NA WATUMISHI WOTE NA RAIA WAJALI KUISHI KWA KUTENDA MEMA AMBAYO NDIYO MILA NA DIRA YA MAISHA YETU TANGU UTAMADUNI WETU WA KITANZANIA HASA WA KIJAMAA, TUSIYUMBISHWE NA WAGENI KUINGIA KUDAI HAKI BILA KUJALI USALAMA AMBAYO TUKIUPOTEZA SI RAHISI TENA KUURUDISHA, NA HASA WATU WAZIMA WAWAONGOZE WATOTO WASIPENDE KUDAI HAKI NA DEMOKRASIA BILA KUWA NA MIPAKA.
TUNAOMBWA KILA WAKATI
TUZIPIME HAKI KAMA NI ZA KWELI NA TUPIME NJIA BORA ZA KUTUFIKISHA KWENYE HAKI KWELI
Mfano wageni wanatuingiza katika kudai haki bila kuwa na mipaka ya heshima na nidhamu ya maadili yetu. Tunapoambiwa watu wa jinsia moja kujamiiana ni haki, hii si haki wala si sawa katika imani , na mafunzo ya maadili au maumbile ya binadamu. Mtu anapofanya kitendo hicho ni makusudi anaharibu afya yake na anatakiwa achukuliwe hatua, mbona watu wakikeketwa tunawachukulia hatua, au mtu akiamua kujinyonga akipona tunamchukulia hatua, kwanini mtu anapoishi kwa kinyume cha kujamiiana hatuchukui hatua, ni kwa sababu Mzungu kasema au ni kwa sababu tumefungwa kwa pingu za kiuchumi.
Tutafakari sana mambo haya, hasa watu wazima tusiache vijana wadai haki bila kujua wajibu wao wa kuchunguza na kuona njia bora ya kupata haki zao ni nzuri pia wanatakiwa kujiuliza kama hicho wanachodai ni haki ya kweli. Maana mtu anayedai ndoa na mtu wa jinsia sawa na yake inabidi ajiulize kama ni haki yake kweli, siyo swala la viongozi kubaki wanasema ni haki ni haki, haya mambo ni mabaya ndiyo yamepelekea kuleta maafa katika nchi nyingi za Africa , mfano Misri, Libiya nk. Vijana na viongozi tuwe macho panapotakiwa kukemea na kuchukua hatua tufanye haraka.
Ni mimi raia mwema anayependa taifa lake
Mr. BONIFACE MAZIKU
Mwenye kiti wa shirika la hiarai (TADESO)
Tabora Voluntary Development Society
P.O. BOX 1646 TABORA
P.O BOX 32345 DAR ES SALAAM
Email : bonigema@yahoo.com
B