
Msiba wa Msanii maarufu zaidi wa filamu Tanzania Stephen Kanumba umekuja na kutuachia mshtuko kupita kiasi. Kutokea kwake katikati ya Ijumaa Kuu na Pasaka kwa kweli umefanya sikuu ya Pasaka (yenye kuadhimisha ufufuko) kuwa na maana ya pekee kwa baadhi yetu. Sisi wengine tayari tulikuwa tunaomboleza kuondokewa kwa aliyekuwa Inspekta Generali wa Polisi Mzee Harun G. Mahundi hatukutarajia mioyo yetu kuchomwa na msiba mwingine ndani ya muda huo. Lakini Mungu ni Mungu kwani nina uhakika wapo watu wengine wengi tu ambao walikuwa kwenye misiba mingine wakati huo huo na msiba wa Kanumba ukaja kama kidonda kingine.
Kilichoshtua wengi zaidi na hasa tuliopata habari mapema zaidi ni nini kilitokea. Taarifa za mwanzo kama ilivyotarajiwa zilikuwa na utata sana maana wengine walianza kusema ilikuwa ni ajali ya gari huko Mbagala wakati wengine wakitaja vyanzo mbalimbali. Lakini baada ya muda taarifa zikawa wazi zaidi kwamba kifo cha Kanumba kimesababishwa kwa namna moja au nyingine katika mazingira ya ugomvi wa kwenye nyumba (domestic conflict) ambao matokeo yake ni mmoja kufariki. Na kilichokuwa wazi mapema hiyo ni kuwa msanii mwingine maarufu Elizabeth Michael a.k.a Lulu alikuwa anahusika.
Mara moja hata hivyo baadhi ya watu walianza kueneza habari kuwa “Lulu kamuua Kanumba” na wengine kwenda mbali na kumuita “muuaji”. Niliwasoma wengine wakielezea kifo cha Kanumba kama “mauaji” bila ya shaka wengine wakishindwa kujua kuwa baadhi ya lugha wanayotumia ina maana ya kisheria zaidi. Kwamba Kanumba ametutoka hilo halina ubishi lakini ni mazingira gani yalisababisha hilo hilo ni suala la kitaalamu na la kisheria. Hapa ndio hoja ya Lulu kutendewa haki inapokuja kwa sababu tusipoangalia kutokana na maumivu tuliyonayo ya kupotelewa na mtu tuliyempenda mno basi tunapoteza macho yetu ya haki na tunajenda macho ya kisasi ambayo hayataki kuutafuta wala kuujali ukweli.
Niwashirikishe maneno yenye hisia hizo yaliyoandikwa na mmoja wa wanaForum wa JamiiForums.com akijaribu kuturudisha kwenye fikra za kujali haki bila kumuangalia nani atanufaika na haki hiyo. Yaani, badala ya kuangalia ni “Lulu” anahusika basi tumweke huyo “Lulu” kama ni mdogo wetu, binti yetu, rafiki yetu n.k na amefanya kitu ambacho pia kimemsababishia mauti ndugu, rafiki au jamaa yetu mwingine; je tungependa atendewe vipi? Ni wazi wengi tungependa atendewe haki; asionewe, asidhulumiwe au kupendelewa. Yaani, isije kuwa watu ambao walikuwa na chuki na Lulu kabla ya tukio hili ndio wanakuwa wa kwanza kupiga debe la “muuaji muuaji” kumbe wanathibitisha tu midomoni mwao kile wanachokiamini moyoni kutokana na chuki.
Mwanachama huyo aitwaye WomanofSubstance aliandika hivi katika mtandao huo na nimebandika hapa ili kutupa fikra na sisi wengine:
Naanza na kutoa Pole kwa watanzania wote, hasa ndugu jamaa na marafiki wa karibu wa Kanumba The Great (R.I.P) kabla sijatoa mchango wangu kuhusu hili jambo zito na nyeti ambalo limetawala maongezi katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka. Mengi yamesemwa na pia kuna mengi pia hayajasemwa, moja wapo likiwa "ujinai" wa Lulu katika kifo cha Kanumba.
Katika mukatadha wa sheria, tunaona kwamba Tanzania ni moja ya nchi zenye kuuweka uwajibikaji kijinai kuwa chini ya UMRI wa miaka 18 kwa kuweka miaka 10 kama umri ambapo mtu anaweza kushtakiwa kwa kosa la jinai. (Linganisha na Kenya miaka 8, Zimbabwe -7,Zambia 8,Africa Kusini 10) n.k. Ina maana kwamba mtu (mtoto) aliye chini ya umri huu hawezi kushtakiwa labda ithibitishwe kuwa alikua anajua kabisa anachokifanya. Lulu hafit kwenye kundi hili hata kama ana umri wa miaka 17 kama ambavyo Mh Halima Mdee ame tweet leo baada ya kumtembelea LuLU Oysterbay Polisi.
Tukiacha sheria na matakwa yake, kwa kuzingatia yale yanayosemwa kuhusu mkasa huu wa kifo cha Kanumba (R.I.P), inatupasa tuone kuwa kila hadithi ina pande mbili. Hadithi ya Kanumba ambaye kwa sasa hayupo kuelezea, na hadithi ya Lulu aliye mahabusu. Inasikitisha sana kwamba kifo kimetokea katika mazingira ya kutatanisha. Kifo hiki kimesikitisha watu wengi na kufanya udadisi wa kutaka kujua ukweli ulio objective iwe vigumu. Watu wamebakia kushusha lawama ZOTE kwa Lulu tu bila kutaka kujua haswa ilitokea nini hadi kifo hicho kikatokea.
Kama watanzania wengine napenda niseme kwamba , nahuzunika kama wengine kumpoteza Kanumba na pia kuona ndoto zake kama msanii zikizimwa ghafla. Aidha wapenzi wake wamekatishwa ile raha ya kuendelea kuburidika na filamu zake. Pamoja kuwa na huzuni kuu, pia najaribu kuangalia upande wa pili – Lulu! Huyu binti wa miaka 17/18 kijamii bado ni msichana mdogo japo kisheria hasamehewi kuwajibishwa kijinai. Lakini uwajibishwaji huo utakuja pale upelelezi utakapokamilika. Kufuatana na waliobahatika kumuona huyu binti, ana majeraha kuashiria kuwa alipigwa na kuumizwa na marehemu. Ingekuwa marehemu hakufa, basi nadhani kesi hii ingekuwa ya aina yake kama ingefika kunakohusika. Wote walijeruhiana. Lakini mazingira ya kujeruhi huko ni yepi?
Tumeambiwa na hata kusoma kwamba:
- Lulu alienda kwa Kanumba usiku mkali mishale ya saa 6, kusudi watoke kwenda kucheza muziki kwa msanii Chaz baba – Mashujaa band ( Kanumba alishapiga simu kutaka andaliwe viti na sehemu maalum ya kukaa yeye na marafiki zake na pia akiomba hata wimbo maalum atakapofika)
- Lulu alitoka nje kusikiliza simu – Kanumba akamfuata na kumrudisha ndani ili aeleze anaongea na nani.( Hapa tunaona kabisa Kanumba akianzisha shari yeye mwenyewe badala ya kuepuka shari)
- Kanumba alimfungia Lulu ndani wakawa wanagombana. Aggressor hapa ni Kanumba na siyo Lulu.Kelele za ugomvi ziliashiria vurugu na kwa vile mlango ulifungwa na ufunguo, ilikuwa vigumu Lulu kukimbia tena au hata watu nje kuja kutoa msaada.
- Lulu alitoka nje kwenda kumwita Seth na kumwambia Kanumba kaanguka.Lulu alikimbia akiwa na majeraha.Hii haionyeshi kuwa Lulu aliua vinginevyo angetoka kimya kimya akatokomea.
Sasa ndugu zanguni, kwanini Lulu anaonekana alifanya mauaji ya kukusudia? Ikiwa Kanumba alianguka katika purukushani na kuponda kichwa na kufa, Lulu kaua vipi? Kukamatwa na polisi na kushikiliwa ili kusaidia uchunguzi ni utaratibu wa kawaida sana. Nimewahi kushuhudia mtu kajiua, ndugu yake na mkewe waliomgundua kajining’iniza walikamatwa wakakaa ndani ili wasaidie uchunguzi Ilahali mtu kajiua mwenyewe. Ilisikitisha sana kwa maana wafiwa walitiwa misukosuko kwa kifo ambacho marehemu alijiletea kwa kujitundika. Walikaa masaa kadhaa kabla ya ndugu kwenda kuwatetea na kushinikiza waachiwe!
Kwenye hii kesi ya Lulu, bahati mbaya sana Lulu ana sifa mbaya kwenye jamii kiasi kwamba hakuna mtu anathubutu kumtetea na kumsaidia angalau aweze kujipanga kukabiliana na siku za kusubiri hatma baada ya upelelezi. Kibaya zaidi kuna statements za watu wazito ndani ya jamii, statements ambazo zenyewe tu zimeshapasisha kwamba Lulu ndio muuaji. Kibaya zaidi, unyeti wa hali inayozunguka msanii maarufu kipenzi cha wengi utaathiri hata mwenendo mzima wa upelelezi na kitakachojiri to the detriment of Lulu…
WoS
Sasa WoS amechokoza mjadala huu kwa kuangalia mtazamo wa kisheria na mjadala huu ulipamba moto sana na unapatikana kwenye Jukwaa la Sheria la mtandao maarufu zaidi wa mijadala ya Watanzania Duniani wa Jamiiforums.com Swali ambalo tunakabiliwa nalo ni kuwa je Lulu anaweza kweli kutendewa haki? Je, hata kama ushahidi utaonesha kuwa Lulu alikuwa anajihami au anajitetea je tuko tayari kulikubali hilo na kuona kuwa ni ajali mbaya? Je, kuna uwezekano wa Lulu kuweza tena kufanya kazi ya usanii endapo ataonekana hakuwa na hatia wala kukusudia kusababisha mauti ya mtu tuliyekuwa tunampenda? Lakini pia upande mwingine ni je kwa vile ni kifo kinachomhusisha mtu maarrufu yawezekana Lulu akahukumiwa vikali zaidi kuliko mtu mwingine kwenye mazingira yale yale? Fikiria kwa mfano viongozi kadhaa ambao wameendelea kuwa huru licha ya kusababisha vifo vya watu na hawakushikiliwa jela kwa muda ambao Lulu ameshikiliwa. Kama yule Mbunge aliyesababisha vifo vya kina dada wawili katika bajaji! Kweli, Lulu anaweza kuwa na hatia zaidi kuliko yule au kwa vile wale kina dada hawakuwa watu maarufu kihivyo?
Ndio maana natoa wito binti huyo atendewe haki na siyo tu atendewe haki bali pia haki ionekane inatendeka. Lakini wakati huo huo marehemu atendewe haki yake vile vile kwa sababu yawezekana wakati tunafikiria suala ni “Lulu” na Kanumba kumbe kuna watu wengine wanahusika!
Maoni ya Wasomaji
Uchambuzi makini sana huu
Uchambuzi makini sana huu nilikuwa naongejea gazeti hili kwa hamu nikijua litakuja na angle mpya, kulinganisha na magazeti yote niliyosoma tangu kifo cha msanii, na nachelea kusema makala hii imejibu maswali mengi yalikuwa hayasemwi kwingineko.
Na niimani yangu kuwa utaendelea kutujulisha kadri kesi hii inavyoendelea.
Lakini ninawasiwasi mkubwa kuwa Lulu hatapata fair trial kwani tayari amehukumiwa sio tu na vyombo vya habari bali pia serikali, kwa serikali kuonyesha waziwazi uwepo wake kwenye kifo cha utata kama hiki inatia petroli kwenye vyombo vya habari na pia shinikizo kwa jaji au juries.
Hivi kulikuwa na umuhimu kwa mkuu wa nchi kwenda in personal? Na kukatiza safari nje ya nchi au hata kama ingekuwa ndani bado ni ya kitaifa. Kwanini wasitume salamu kimya kimya kuwafariji wafiwa katika kipindi hiki kigumu.Endelea kutupasha.
Huyu binti atendewe haki
Huyu binti atendewe haki,Inaonyesha kabisa kuwa alikuwa anajihami kutokana na kipigo,pamoja na udharirishaji wa kuburuzwa ili arudi ndani ajibu nani alikuwa anaongea nae.
Lakini pia ni muhimu kwa vijana wetu wa sasa kujifunza kuwa kupokea simu ni uhuru wa mtu,
Na hivyo basi,marehemu hakuwa na haki ya kuingilia maongezi ya binti huyu hata kama alimununulia simu hiyo yeye,Ni ulimbukeni wa kufikiri kuwa kumzuia mtu kupokea simu ndo mapenzi hayo!!
Naona hata utetezi wake kama anyo majeraha ni rahisi sana,tena haitaji hata Wakili wa kumsaidia.
Kwa vyovyote vile,binti huyu jamii itashindwa kumpokea kwa sasa,ila kadri muda unavyopita atatafuta kazi nyingine ya kufanya na si lazima afanye maigizo
LULU alitengenezwa ili awe
LULU alitengenezwa ili awe mhalifu.............Tasnia ya filamu imejaa tabia chafu..........watu walikuwa wapi mpaka Lulu afikwe na mambo haya....................Kanumba alichagua maisha yake mafupi ya usanii. He decided earlier his destiny but as a human being am very sorry and let him rest in peace.
kwenye kuliendea hili vipo
kwenye kuliendea hili vipo vitu vingi saan vya kuangalia ktk kutoa maamuzi,labda niseme kitu kimoja kwamba siingilii mwenendo wa case bali haiyumkini kwa mtu kama kanumba alivyo na lulu alivyo then kanumba hakuwa na alama ya kuchomwa kisu wala kunyweshwa sumu then iwe lulu alimuua,sijui wanaocomment hivi wangetuambia tendo ambalo wanadhani ndili alilolifanya kumuua ni lipi? kama ni kweli alimsukuma na kanumba akaanguka kwann tusi-doubt kwamba huenda alimsukuma kwa kujitetea baada ya kipigo ambaccho kimethibitishwa wmilini mwa lulu? mbona swala la kuwa kanumba alikuwa melewa whisky halizungumzwi kwamba huko kudondoka kwake kirahisi lkumetokana na kulewa? hv kweli kanumba yule kwa mazoezi yale anawza akasukumwa na mtu kama lulu akaanguka kama mzigo? jamani tusiwe so optimistic ,let us see haki ikitendeka na kama una personal differences na lulu basi uwe wazi tu kuwa wewe una biff na lulu lkn kama utatoa mawazo yako ni bora ukaangalia tukio lilivyo na jinsi mazingira yake yanavyozungumzwa hasa na huyo seth bosco ambae pamoja kuwa hata yy hawezi kuwa shihidi mzuri kwakuwa hakuwepo chumbani lkn angalau alikuwa jirani na tukio.
kwanini wametumia kifungu
kwanini wametumia kifungu namba 196 katika penal code kinachoonyesha kuuwa kwa kukusudia badala ya kifungu kingine?
All in all , Lulu anamatatizo
All in all , Lulu anamatatizo matatizo,Mtoto wetu, dada yetu Mdogo wetu
Kwanza poleni sana wana dar es salaam,Tanzania, africa mashariki kwa msiba mkubwa ambao wote kwa ujumla umetugusa kwa namna moja au nyingine
Wana Haki za binaadam wanasheria tujitokeze kwa hili tuone jinsi ya kumsaidia hili,tuingilie hili swala Tuone kuwa lulu mbali ya yote anastahili kuishi na maisha yake yanabidi yaendelee tuone anatendewa haki kama watu wengine
Natumaini ndugu zangu
Natumaini ndugu zangu watanzania na mataifa mengine mu wazima na nawaombea uzima na afya njema. Kwa kweli napenda kuanza kwa kumtakia ndugu yetu mpigananji wa bongo movies aliebeba bendera ya Tanzania kuintangaza ndani na nje ya nchi tasinia ya filamu Tanzania awekwe mahari pema peponi,Mungu ametwaa na jina lake litukuzwe. Sasa nachangia mada ya mkasa kama ifuatavyo,naungana na baadhi ya wachangiaji hapo juu kuwa kulingana na tukio kuwa halieleweki kwa ufasaha,haina haja ya watu kuanza kuongea kwa uthibitisho kuwa LULU kamuua Kanumba. Nijuavyo mimi matamshi kama hayo kisheria yana maana kubwa na yanaweza kukuweka pabaya kama huna huo uthibitisho,watu wengi wanapenda kudakia mada na kutoa walichonancho bila kusubiri kupata uhakika wa nini ni nini na kilikuwaje,habari za kusikia tu na wewe unaanza kusambaza bila kuwa na uhakika ndo yanayoponza watanzania wengi.Hapa sasa vyombo vya sheria na polisi bado wako katika hatua za mwanzo kabisa za uchunguzi hapohapo watu walishahukumu tayari,tutafika kweli,nini umuhimu wa uchunguzi?hatukatai kama mtu ana habari yeyote inayoweza kusaidia katika uchunguzi aende polisi awape vielelezo hivyo kuliko kuongelea mitaani.Nilikuwa nawaambia rafiki na jamaa huku nilipo kuwa Kanumba katutoka ila mtasikia mengi kuhusu marehemu na kilichomuua mpaka mtachoka,na kweli yamesemwa nafikiri yamefika gunia,nimesoma magazeti mengi toka amefariki Kanumba,nayo hayaeleweki,mara yanasema hivi mara hivi tena,kwa kweli nayo yanachanganya tu watu,mara ilikuwa hivi mara hivi,mpaka watoa maoni wengine waliona hilo pia kuwa sababu ya kifo chake hakijajulikana ila watu wanaongea sana wakati hawajui what happened zaidi ya rumours.Kwa wafuatiriaji wazuri wa kusoma na kufatilia vyombo vya habari wanweza kuwa pamoja nasi juu ya tunachokiongea hapa,utata wa sababu ambao haujajulikana,na mlolongo wa matukio kabla na baada ya masiba kutofautiana muda baada ya muda. Cha msingi watu wawe na subira serikali kupitia vyombo vyake (polisi na mahakama) wafanye kazi kwa haki ili haki itendeke kwa mtuhumiwa lulu kuliko kumuhukumu bila ya vigezo vya msingi
Da MWANANZELA big up maana
Da MWANANZELA big up maana umeiweka mada hii kishule zaidi. Tunawataka sana watu kama nyie kwa kuonyesha msimamo kulingana na unavyoweza kuufikirisha ubongo wako na utumizi wa elimu uliyo nayo.Yaani nimekuelewa vizuri sana.Ni kweli Tanzania mtu masikini kifo chake hakithaminiwi hata kama kavunjiwa haki zake kama vile kifo cha KIBONDE deleva wa daladala Dar.....wale wa bajaji na wengine wengi.Kama ulivyoseema kama kweli LULU hakubaliki ktk jamii kwa tabia zake sawa lakini si ktk hili mbona watu wanaenda mbali sana kwa kumuhukumu?!!!!!! HAKI ITENDEKE KTK HILI BILA KUJALI KANUMBA ALIKUWA JEMBE LETU.
Tunataka tumsikie yeye
Tunataka tumsikie yeye mwenyewe Lulu akitamka kilichotokea kati yake na Kanumba, sio leo ilikuwa hivi mara hivi. Msichukulie kifo cha Kanumba kirahisi rahisi tu au bahati mbaya, aseme mwenye Lulu tumsikie, na kama ana hatia basi ahukumiwe, Lulu ni mtu mzima ndio maana aliweza kwenda kwa Kanumba usiku na walikuwa na mpango wa kutoka na si ajabu angerudi kulala kwake, hapo hakuna udogo, hiyo simu kwa vyovyote vile ilikuwa haina jambo jema ndio sababu ya ugomvi, kwa nini aliizuia? inawezekana kabisa kipondo alikipata baada ya marehemu kugundua anamdanganya.
Kabla hata hatujaangalia
Kabla hata hatujaangalia Kanumba kafaje hebu tumwangalie aliishije? Hivi kweli wewe kama mzazi Kanumba ni mtu ungeweza kumkabidhi mwanao (hata wa kiume) asafiri, aishi naye au amlee? Kama ungeweza basi wewe ni mzazi wa hovyo kabisa kama walivyo wazazi wa Lulu.
Najaribu kufikiria hivi Mwalimu wakati wa Uraisi wake, angehudhuria mazishi ya mtu aliyeishi hovyo na kufa katika mazingira ya kufedhehesha hivi? Hata Mkapa sidhani angehudhuria. Kwa nini Ikulu imevia hivi? Hivi Kanumba na kina Mzee Jongo, Hamisi Tajiri, Mzee Kipara na wengineo nani alielimisha jamii zaidi? Mbona Raisi hakwenda kwenye mazishi yao? Kuna siku Raisi atahudhuria harusi ya waigizaji wa Bongo Dar Es Salaam!
Viongozi wetu wanapaswa kujiheshimu na kuheshimu ofisi tulizo wakabidhi. Utamaduni huu ulianza kitambo kidogo eti Waziri wa Michezo alikwenda kumpokea Mrisho aliyetoka Big Brother Africa! Mtu katoka kuonyesha uchafu hadharani anapokewa na serikali?
Haya matokeo ya kutupa miiko ya uongozi. Huwezi kuwa kiongozi wa kitaifa halafu tunakuona unatenda mambo yanayowiana na mitaa ya Ohio!
Raisi angekwenda Arusha, Songea na kwingineko wananchi walipouawa na vyombo vya dola tungeamini anajua wajibu wake! Haya ya mazishi ya watu wa aina ya Kanumba awaachie wasanii!
<p>Kabla hata hatujaangalia
Kama Huyo Lulu alimsukuma
Kama Huyo Lulu alimsukuma Kanumba na kuanguaka je?
Inawezekana huyo Lulu alimsukuma Kanumba naye akaanguka na kusababisha kifo chake. Hilo hamlioni au mnataka tu kumtetea huyo Lulu. hayo yote ni matatizo ya wasanii wetu wengi hawana shule. kama huyo mdada aliyekimbia shule.
Msichezee watoto, wetu Mungu
Msichezee watoto, wetu Mungu anawaona!!...
Nadhani kwa sasa si vema
Nadhani kwa sasa si vema kumlaumu Lulu kwa yaliyotokea tuwe na subira tusubiri maamuzi ya Kisheria. Nina imani vyombo vya dola vitatenda haki.
jamani mie hapo kwakweli
jamani mie hapo kwakweli sioni kama kweli LULU ana makosa, kulingana na uchunguzi wa madaktari bingwa uliofanyika inaonyesha kuwa hilo tatizo la Kanumba lililomuua halikuanza siku hiyo bali kutokana kuwa na tatizo hilo kile kitendo cha kuanguka na kuutikisa ule ubongo ambao ulikuwa na tatizo before ndo ulipelekea kifo chake, na haya kama kweli lulu alimsukuma nae alikuwa katika kujihami maana kumbukeni walikuwa katika ugomvi hata kama ingekuwa wewe au mimi lazima mtu unajitahidi kujiokoa hauwezi ukakaa tu huku unapigwa, kwakweli sheria imtendee haki binti huyo mdogo, kwanza tukiangalia bahati nzuri marehemu Kanumba angepona nae ingebidi afunguliwe mashitaka kwa kuwa katika mapenzi na mtoto mdogo ambaye aja-turn hata 18
Its true hata katika hali ya
Me naona MUNGU alipanga
Me naona MUNGU alipanga kumuumbua lulu kutokana na aliyokua akiyafanya nbali na umri wake huo mdogo.Kwa upandr mwengine ni siku ya kifo cha Kanumba ilifika cuz angeweza dondoka na kupoteza fahamu tu,tusimlaumu sana Lulu.What if angekufa Lulu?until now no body know what happened behind the scene,thus we should not blame anybody.Hata hivyo huyu mtoto anahitaji Guidance and councelling bcause she is deliquent...Mahakama ifanye kazi yake na likiwezekana apate msaada wa KISAIKOLOJIA.