Muungano waundwa kumwondoa Mugabe madarakani

Robert Mugabe, 93, amekuwa madarakani tangu Zimbabwe ipate uhuru mwaka 1980 kutoka kwa Uingereza

Harare, Zimbabwe

WANASIASA maarufu katika siasa za upinzani nchini Zimbabwe wamekubaliana kuunda umoja kwa ajili ya kupambana na Rais Robert Mugabe wakati wa uchaguzi mkuu nchini humo mwaka ujao.

Mpinzani wa muda mrefu dhidi ya Mugabe, Morgan Tsvangirai na aliyewahi kuwa Makamu wa Rais Joice Mujuru wamesema watafanya kazi pamoja katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2018.

Hata hivyo, bado haijafahamika ni yupi kati yao atagombea urais katika uchaguzi huo.

Mugabe, 93, amekuwa madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1980 na tayari ameshatangaza kwamba atagombea katika uchaguzi mkuu ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *