NI wapi ulipata habari kwamba niliwahi kusema kuwa Ujamaa ulishindwa vibaya Tanzania? Katika miaka ile ya sabini, nchi kadhaa zilisambaratika kiuchumi na hazikuwa zikijenga Ujamaa. Najua hivi sasa inahitaji ujasiri kuuzungumzia Ujamaa, lakini lazima uelewe manufaa ya maadili ya kijamaa tuliyokuwa tunajaribu kuyajenga nchini mwetu