Mwaka mwingine wa uhuni na vurugu chama tawala

HAUHITAJI kuwa nabii kugundua kwamba mwaka huu utakuwa na mivutano na misuguano mingi ya kisiasa. Hili ni jambo linaloeleweka hata kwa wale tunaoweza kuwaita mbumbumbu-mzungu-wa-reli katika masuala ya kisiasa. Mwaka huu zitafanyika chaguzi nyingi na za ngazi mbali mbali ndani ya CCM, chama-tawala, kuanzia ngazi

Ufisadi walitesa Jiji la Mbeya

MWAKA 2011 umeisha huku uongozi wa Jiji la Mbeya ukigubikwa na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, mtuhumiwa mkuu akiwa ni Meya wa jiji hilo

Kwa nini mkulima Mwamwindi alimpiga risasi RC Dk. Kleruu? V

UKIMWONA kwenye mitaa ya Iringa bado anatembea  kwa hatua za kijeshi. Ni Mzee David Butinini. Alipata kuwa askari polisi na alishuhudia kwa macho yake, siku Mkulima Said Mwamwindi alipofika kituo cha Polisi Iringa akiwa na mwili wa marehemu Dk. Kleruu kwenye gari aliloendesha. Dk. Kleruu

Nauli Kigamboni: Magufuli futa kauli yako, waombe radhi Watanzania

WAZIRI wa Ujenzi Dk. John Magufuli amenukuliwa na watangazaji wa habari akitamka:  "Na atakayeshindwa kulipa nauli mpya Dar- Kigamboni na apige mbizi au azunguke Kongowe." Kauli hii ya Magufuli inaingia kwenye rekodi kwa kuwa ni ‘ mchemsho’ wa kwanza kwa mwaka huu wa 2012  kutoka

Waliwapuuza Jaji Nyalali, Kisanga, kwa nini tusiwatilie shaka sasa?

NOVEMBA mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete alisaini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011. Pamoja na kusaini, taarifa ya Ikulu ilisema: “…kwa mwananchi yeyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha sheria hiyo, ajisikie yuko huru kutoa maoni yake na Serikali

Tumewavumilia, imetosha

NCHINI, kuna mambo mbalimbali ambayo kama ilivyo kwa Watanzania wengi, nasi Raia Mwema, tusingependa kuyashuhudia yakiendelea mwaka huu, kama ilivyo mazoea kwa miaka iliyotangulia.

Hongera, Balozi Sefue, lakini kazi unayo!

Ni uungwana kuwapongeza wale miongoni mwetu wanaopata bahati ya kuteuliwa kushika madaraka. Pongezi hutokana na kuelewa kwamba aliyeteuliwa kateuliwa kwa sababu aliyemteua ametambua sifa kadhaa za mteuliwa ambazo zinamfanya afae katika nafasi aliyoteuliwa kuishika