Regia Mtema katuachia mfano wa kuwajibika kwa wapiga kura

KIFO cha Mbunge wa Viti Maalumu, Regia Mtema (CHADEMA) kilichotokea Jumamosi iliyopita kimeacha pengo kubwa katika maisha na fikra za watu wengi ambao walikuwa wanamfuatilia na kumfahamu. Kwa hakika kimeacha pigo kubwa kwa familia yake na kuacha ombwe lisiloweza kuzibwa. Wakati wazazi wake, ndugu, jamaa

Regia ameondoka, ametuachia daraja

JUMATANO ya leo hii kuna mkusanyiko mkubwa wa watu kule Ifakara. Ni Watanzania wanaoshiriki kumsindikiza kwenye safari yake ya mwisho, ndugu yetu mpendwa, Regia Estelatus Mtema. Ni Jumatano hii ya leo, Watanzania kwa mamilioni, nao, kwa kuelekeza fikra zao kwa Regia wanashiriki kumsindikiza ndugu yetu

Kujitolea kuko wapi au tuseme wanajitolea kuvimbiwa?

‘Dunia imebadilika dada. Wazee wanauza mashamba ili watambe kilabuni kwa hiyo sisi lazima tutafute njia ya kujikimu. Sasa mimi naenda kwenye biashara zangu, ghafla naambiwa nilime barabara

Kuna nini kwenye siasa zetu?

KATIKA moja ya makala za ndani ya toleo la wiki hii tumechapisha mahojiano na mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Jaji Joseph Warioba, akizungumzia, pamoja na mambo mengine, matatizo ndani ya vyama vya siasa

Kwa nini mkulima Mwamwindi alimpiga risasi RC Dk. Kleruu? VI

NIPO katika mgahawa wa Neema Craft mjini Iringa. Mzee David Butinini na mimi tumepanga tukutane mahali hapa kwa chakula cha mchana na mazungumzo kuhusu alichokishuhudia miaka 40 iliyopita. Inahusu tukio la mkulima Said Mwamwindi kumpiga risasi aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Kleruu. Zikiwa

Ukamilifu wa ubinadamu wetu utathibitishwa na fikra zetu

WIKI iliyopita nilianza safu hii kwa kuibua upya mjadala kuhusu changamoto kuu zinazotukabilia katika kujitambua, kujikomboa na kujipambanua kama binadamu tunaofikiri sawa sawa. Nilihitimisha kwamba sifa kubwa inayomtofautisha kimsingi binadamu kamili na hayawani ni kule kufikiri kwake, ambako humwezesha kutaka kujua zaidi na kujikuta akikusanya