Uhuru na maendeleo: changamoto ya miaka 50 ijayo

KUNA uhusiano wa moja kwa moja kati ya uhuru na maendeleo. Ni uhusiano kama wa yai na kuku kwamba huwezi kuwa na yai bila kuku na huwezi kuwa na kuku bila yai. Siyo maoni yangu hayo bali maoni ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.

Mazingira: Tutokako, tuliko na tunakokwenda

Imekuwa miaka saba sasa tangu sheria iipe NEMC meno, na matukio ya uchafuzi na uharibifu wa mazingira ndiyo yanaonekana kuongezeka. Kuna wengi sasa wanaojiuliza: Kulikoni? Makala haya yanachambua historia, harakati na nini kifanyike kagtika kutunza mazingira. UHIFADHI wa mazingira Tanzania, kama ilivyo kwa nchi za

Sir George, muasisi mkimya wa harakati za uhuru

MSEMO wa Kiswahili usemao, “kimya kingi kina mshindo mkuu, ni sahihi kwa mujibu wa mwenendo wa kisiasa aliokuwa nao mwanasiasa mkongwe wa nyakati zote, aliyeingizwa kimyakimya katika harakati za kudai uhuru wa iliyokuwa Tanganyika miaka kadhaa kabla ya nchi kujitawala. Clement George Kahama, al-maarufu Sir.

TFA: Serikali itoe uhuru kwa mkulima kuuza mazao yake popote

Hivi karibuni Mwandishi Wetu wa Kanda ya kaskazini   Paul Sarwatt alifanya mahojiano na Mwenyekiti wa Chama Cha Wakulima nchini Tanganyika Farmers Association (TFA),  Elias Mshiu. ifuatayo ni sehemu ya mahojiano hayo. Swali: Wasomaji wetu wangependa kufahamu historia fupi ya TFA. Je unaweza kuwaleza kidogo?

Miaka 50 ya uhuru na uzalendo unaotoweka

SIKU chache kabla ya Uhuru, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliandika kwenye Gazeti la “The East Africa and Rhodesia”, lililokuwa likichapishwa mjini London. Aliandika kwamba: “Maisha yetu yote yamekuwa yakidhibitiwa na watu ambao mtazamo wao wa maisha wa kigeni kwetu; ni watu wenye

Nyerere nabii wa kisiasa

MCHAKATO wa kumtangaza mwenye heri Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ulioanzishwa na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es salaam, una kila dalili za kutekelezwa kwa hiyo basi inahitaji kuchangiwa maoni. Wastahiki wa kutoa maoni hayo ni kila mtu awezaye kuanisha kwa vigezo,

Kwa nini mkulima Mwamwindi alimpiga risasi RC Dk. Kleruu?

IRINGA ina historia ndefu ya harakati za mapambano ya kudai uhuru. Harakati za kijamii, kisiasa na kiuchumi. Wakati huu nchi yetu ikielekea kwenye kuadhimisha miaka 50 ya uhuru si vibaya tukakumbushana tulikotoka ili tuweze kuelewa tulipo sasa na tunakokwenda. Hakika, simulizi ya Mkulima Saidi Mwamwindi

Uhuru wetu ulikuwa mwanzo wa safari yetu

SIKU kama ya leo miaka 50 iliyopita ilikuwa ni ya kihistoria  kupindukia. Kwani siku hiyo ndipo Tanganyika ilipopata Uhuru wake na kukomesh ukoloni wa Waingereza.  Kwa tuliokuwapo, hakika ilikuwa ni siku adhimu sana. Wakoloni, hasa wa Kijerumani  na Kiingereza,  walitutawala kwa takriban miaka 70. Ndani