Kuuawa kwa Osama Bin Laden; Tafsiri yangu

"ANAYEOGELEA baharini haogopi mvua," alipata kusema Osama Bin Laden. Naam, habari zimetufikia kuwa Kikosi Maalumu Cha  Makomandoo wa Marekani kimeendesha operesheni maalumu iliyowezesha kuuawa kwa Osama Bin Laden nchini Pakistani usiku wa kuamkia Jumatatu. Ndio, anayeogelea kwenye bahari yenye kina kina kirefu yumo katika hatari

Somo kutoka Marekani: Taifa haliwezi kutekwa nyara

UKURASA wa mtandao wa intaneti wa Taasisi ya Upelelezi Marekani (FBI) imepambwa na picha na taarifa ya kuwa Osama bin Laden, mmoja wa watu kumi waliokuwa wakitafutwa sana duniani na taasisi hiyo amekufa. Kabla ya hapo ukurasa wa taasisi hiyo ulikuwa na bango kubwa lenye

Lini Wazanzibari wa Afrika Kusini watarejea kwao?

TEMBELEA mji wa Durban nchini Afrika Kusini, utakuta wakazi wanaojulikana kama “Wazanzibari”; kwa maana ile ile ya Uzanzibari wa Visiwa vya Unguja na Pemba, ingawa hawaishi Zanzibar wala si raia wa Tanzania. Inawezekana usiamini hili na kujiuliza maswali mengi: “Je, Wazanzibari hawa ni wazawa wa

Buriani Balozi Andrew Tibandebage

BALOZI Andrew Kajungu Tibandebage, hatunaye tena. Alizikwa nyumbani kwake Kihanga, Karagwe, Ijumaa ya Aprili 29. Taifa lemempoteza mzalendo na mpambanaji, Karagwe wamempoteza mshauri wao mkuu, ukoo wa Bakaraza umepoteza nguzo muhimu na familia yake imempoteza baba na babu mwenye hekima, busara na upendo wa kupindukia.

Hata waandishi tuna ‘gamba’ la kujivua!

JANA, Jumanne, Mei 3, dunia iliadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. Mjini Dar es salaam, waandishi wa habari waliiadhimisha siku hiyo kwa kuwatuza wenzao waliofanya vyema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Niitumie fursa hii kulipongeza Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kuratibu

Ya Obama, Kikwete na Usalama wa Taifa

VUGUVUGU la kuwania nafasi ya urais wa Marekani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani limenza kupamba moto.Wakati hadi sasa hakuna majina yanayotajwa kuchuana na Rais Barack Obama katika kinyang’anyiro cha kupitishwa kuwa mgombea kwa tiketi ya chama cha Democrats, hali ni tofauti kwa chama cha Republicans.

Chonde, tunahitaji Bunge si vituko

HIVI karibuni, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila, alizungumzia mwenendo wa wabunge na hasa viashiria vilivyogharimu, vinavyogharimu na vitakavyogharimu hadhi ya Bunge