Tujiandae na changamoto mpya za Muungano

LEO, Aprili 26, 2017, Muungano wa Tanzania unatimiza miaka 53 tangu ulipoasisiwa. Kwenye miaka yake hiyo 53, Muungano huu umepita katika mengi, ya kujivunia na yasiyo mazuri. Muungano huu umeboresha na kufungamanisha uhusiano wa muda mrefu uliokuwepo kati ya wananchi wa nchi hizi mbili. Ni

Naahidi, Mto Ruaha Mkuu utakuwa mkuu tena

PICHA hii niliopiga hapa haivutii. Nimesimama katika bonde la Mto Ruaha Mkuu ambao unaelekea kukauka. Kabla ya mwaka 1993, hakuna binadamu aliyewahi kusimama hapa niliposimama wakati napiga picha hii kwani kote hapa kulikuwa kunafurika maji. Kabla ya mwaka 1993, Mto Ruaha Mkuu haukuwahi kukauka maji.

Kwa hali hii, askari wastaafu wafuge kuku na samaki tu?

NI wazi kuwa yako maeneo hapa nchini kwetu ambako hali ya kiusalama si nzuri kama ilivyokuwa zamani. Kila siku tunasikia kuhusu mauaji yanayoendelea mkoani Pwani; yakiwa yameelekezwa kwa viongozi wa serikali na watumishi wa vyombo vya dola. Na hili haijaanza leo. Kwa takribani miaka minne

Wahitimu wanavyoiingiza mjini Bodi ya Mikopo

KAMA kuna jambo limewahi kufanywa na serikali ya nchi hii katika harakati zake za kuboresha elimu, basi ni uanzishwaji wa Bodi ya Mikopo ambayo tayari imekwishanufaisha maelfu, kama sio malaki ya wanafunzi, na hasa wale wanaotoka katika familia masikini. Mikopo hii imesaidia nchi kupata wataalamu

Namna anavyonasa katika kitanzi cha nia njema

WIKI iliyopita katika safu hii ya Dokezo la Wadau nilianza kuchambua kuhusu uongozi wa Rais Dk. John Magufuli kupitia dhana ama busara ya msemo wa kilatini “manus manum lavat” yaani mkono mmoja huosha mkono mwingine. Kwa sehemu kubwa, makala yangu ya kwanza katika mfululizo wa

Tunamuhitaji Magufuli mmoja kwenye soka

ULIKOFIKIA Mpira wa Tanzania, tunamuhitaji Rais ajaye wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) awe na vinasaba vya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, kuondoa uozo uliokithiri kwenye mchezo wa soka pale viunga vya Karume. Tunamuhitaji sana mtu wa aina