Quotes

Diana na kutenda mema

USINIITE Princess Diana, niite Diana. Fanya matendo mema mengi hapa duniani bila kutarajia malipo au zawadi yoyote. Fanya matendo mema mengi ukiwa na matumaini kwamba siku moja na wewe utafanyiwa matendo mema

Papa na Walutheri

MARTIN Luther? Huyo Martin Luther hakuwa mtu mbaya kiasi hicho. Hakuwa na lengo la kuligawanya Kanisa. Alikuwa na lengo la kupambana na vitendo vya ufisadi ndani ya Kanisa

Dk. Stirling na Wahindi

KATIKA uchaguzi huo iliwabidi TANU kupata pia msaada wa Wahindi katika majimbo mengine. Mojawapo lilikuwa jimbo la Lindi ambaye yule waliyemtaka huko alipingwa sana na majirani zake. Wahindi watatu walikuwa wanagombea, ilibidi mimi na Sijaona (Lawi) twende huko kumsaidia Mhindi kwenye kampeni Mhindi tuliyemtaka

Nyerere na CCM ovyo

CHAMA chetu (CCM) hakiwezi kuikubali tofauti hii ya pili na kikaendelea kuwa CCM, na wala kisitazamie kuwa wananchi watakikubali. Maana tukianza kuzikubali tofauti hizi haramu zinazoongezeka katika jamii yetu kuwa ni jambo la kawaida, basi amani ya taifa letu na utulivu wa kisiasa tulionao vitakuwa

Mahatma na chuki binafsi

NIMEGUNDUA kuwa kuna chuki kubwa kati ya watu wetu na Waingereza. Watu wetu hawatenganishi kati ya Waingereza na Ubeberu wa Kiingereza. Kwao, yote mawili ni sawa. Chuki hii huwafanya wawe tayari hata kuukaribisha ukoloni wa Kijapani. Ni lazima tuishinde chuki hii. Mapambano yetu si dhidi

Mohd Yunus na fikra mgando

KUBADILISHA mitazamo (mindset) na fikra mgando za watu ndiyo changamoto kuu ninayopambana nayo maishani. Mitazamo na fikra mgando wakati mwingi hutuzubaisha na kutukwaza. Hufanya tuyaone mambo kwa namna mitazamo hiyo inavyoelekeza macho kuyaona

Amir Jamal na Ujamaa

MAADUI wa Afrika ya Mashariki lazima waelewe kwamba Tanzania iliikata mirija ili kuinua uchumi wa umma. Ilitaka njia zote za uchumi ziwe mikononi mwa umma. Makabaila wa shirika la Association of East African Industries waelewe kwamba kabla hawajaleta mitaji yao katika Afrika ya Mashariki, nchi

Nyerere na kupenda utajiri

IKIWA serikali ya TANU itachukua hatua za kuzuia tofauti iliyopo sasa kati ya watu wa juu na watu wa chini, sina shaka watu wote walio juu hawatapenda. Hata mimi ninayeandika maneno haya sitapenda; kwani hata mimi napenda kuwa tajiri. Lakini kitakachotuwezesha kujenga nchi safi siyo