Amir Jamal na Ujamaa

MAADUI wa Afrika ya Mashariki lazima waelewe kwamba Tanzania iliikata mirija ili kuinua uchumi wa umma. Ilitaka njia zote za uchumi ziwe mikononi mwa umma. Makabaila wa shirika la Association of East African Industries waelewe kwamba kabla hawajaleta mitaji yao katika Afrika ya Mashariki, nchi zetu tatu zilikuwa zikishirikiana katika kila jambo. Ushirikiano huu, hata kama makabaila hawa wakitia maneno yao chumvi, utaendelea kudumu watake wasitake. Sisi tunalojua ni kwamba siasa inayoifaa Afrika ya Mashariki pamoja na bara zima la Afrika ni siasa ya Ujamaa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *