Quotes

Tshala Muana na ndoa

SIPENDI kumtembelea mama yangu mjini Kinshasa kwa sababu bado sijapata mume wa kunioa. Kila ninapokwenda kumwona mama huniuliza swali lile lile: ‘Umekuja tena peke yako? Tulidhani safari hii ungekuja na mume wako kumtambulisha kwetu.’ Huwa nasononeka kuambiwa hivyo, lakini nifanyeje – huyo ni mama yangu

Clinton na penzi la Lewinsky

NILIKUWA na mahusiano na Monica Lewinsky ambayo hayakustahili. Kwa hakika, hayakuwa mahusiano yanayofaa, na yalitokana na uamuzi wangu mbaya ambao uliniponza. Ninawajibika binafsi kutokana na uamuzi huo mbaya Hata marais huwa na maisha yao binafsi na ya siri

Lamwai na njama za mauaji

SASA tunawaambia (waandishi) kuwa tunao ushahidi kamili wa vikao vilivyofanyika Ikulu ambavyo viliamua kuwa viongozi wachache wa NCCRA-Mageuzi wawe eleminated (wauawe)

Nyerere na shabaha ya uhuru

KULE mwanzo tulimuomba kila mwananchi kushirikiana na wenzake kuondoa umaskini. Swali ambalo hatuna budi tujiulize ni hili: Tunamwomba kila raia kufanya kazi kwa bidii ili tuondoe umaskini wa nani? Umaskini wa viongozi wa TANU? Au wa watumishi wa serikali? Au wa watu wachache wenye elimu,

Sir Isaac Newton na ukweli

AMICUS Plato amicus Aristotle magis amica verita (Plato is my friend, Aristotle is my friend, but my greatest friend is truth ).

Simpson na thamani ya ardhi

ARDHI ni chanzo cha utajiri wote. Kutokana na ardhi tunapata kila kitu tutumiacho chenye thamani – iwe chakula, mavazi, nishati, makazi, vyuma au vito. Matumizi yote ya thamani yanatokana na ardhi – yawe chakula, nguo, mafuta ya kuendeshea mitambo, hifadhi, chuma au mawe ya thamani

Warioba na kung’atuka

UNAJUA hii ndiyo concept (dhana) ya kung’atuka. Ukishakuwa katika madaraka na kisha madaraka yale ukayaacha, njia moja ya kuisaidia nchi yako ni kutojiingiza sana katika utendaji. Unabaki mshauri na unashauri. Unapohitajika unaombwa ushauri. Unapoona inafaa, unatoa ushauri na si kungoja mpaka uombwe

Nyerere na ujira wa mawaziri

TUNATAKA mawaziri wetu walinganishe mishahara yao na wale vibarua wanaopata Sh. 71.50 kwa mwezi, na watambue kuwa ni mikubwa. Hatutaki waziri wetu awe na tamaa ya kupunguza tofauti ya pengo kati ya mshahara wake wa Sh. 3,000 kwa mwezi na mshahara wa Permanent Secretary (mzungu)