Quotes

Kennedy na taifa oga

TAIFA ambalo linaogopa  kuwapa wananchi wake fursa ya kupembua hadharani kujua ukweli  ni upi na uongo ni upi, ni taifa  linalowaogopa wananchi wake wenyewe

Nyerere na haki na usawa

LAKINI chama chetu (CCM)  hakitaweza kuisaidia serikali yetu kutimiza wajibu wake wa kulinda utulivu na  umoja wetu  ikiwa kitasahau, au  kitaonekana kinaanza kusahau, misingi ya utulivu na umoja huo. Bila Azimio la  Arusha, wananchi wanyonge wa Tanzania watakuwa hawana matumaini ya kupata haki  na heshima