NILIWAHI kusikia minong’ono kama hii kwa baadhi ya wabunge wa CCM wakisema Rais (Kikwete) amekuwa soft sana na hivyo uhuru ubanwe kidogo. Watu wa aina hii hutumia maneno ‘uhuru una mipaka’. Uhuru ni uhuru na mipaka ni mipaka. Madikteta wa kisiasa wasio na uvumilivu kukosolewa hupenda sana maneno haya ‘uhuru una mipaka’.