Hifadhi: Tahariri

Tunataraji uchaguzi salama na wa kistaarabu

JUMAPILI hii, Watanzania wanatarajia kupiga kura katika chaguzi ndogo za ubunge na madiwani katika maeneo mbalimbali Tanzania Bara na Visiwani. Huu ni uchaguzi wa kwanza kufanyika nchini baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kama sote tunavyofahamu, hususani kwa wenzetu wa Zanzibar, bado machungu ya

Tunahitaji tafakari nzito kuhusu elimu yetu

HII ni wiki ambayo shule nyingi za msingi na sekondari hapa nchini zimefunguliwa tayari kwa mwaka mpya wa masomo. Kwa wazazi wengi, hii ni wiki yenye changamoto za kipekee. Tanzania ni taifa kijana kwa sababu zaidi ya nusu ya wananchi wake wana umri wa chini

Ahsanteni kwa 2016, mambo mapya 2017

HILI ni gazeti la mwisho la Raia Mwema kutolewa kwa mwaka 2016, labda tu kama litatokea tukio lisilotarajiwa litakalolazimu kwamba tuingie mtamboni na kuchapa toleo lingine. Kwa vyovyote vile, mwaka 2016 ulikuwa na changamoto zake za tofauti na miaka mingine yote iliyopita. Tunataraji kwamba mwaka

Diplomasia ya Uchumi itazame DR Congo

KUNA dalili za kuamini kwamba hali inaweza kuchafuka na kuwa mbaya zaidi katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Tatizo lililopo ni kwamba taifa hilo lilitakiwa kufanya uchaguzi wake kwa mujibu wa Katiba yake mwaka huu, lakini kwa sababu ya kile ambacho

Watanzania waelimishwe kuhusu hisa

KATIKA Robo ya Kwanza ya mwaka ujao, Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) linatarajiwa kushuhudia ongezeko kubwa la thamani baada ya makampuni ya simu ya Tanzania kuanza kuuza hisa zake. Kampuni ya Vodacom, kwa mfano, ambayo inaonekana itakuwa ya kwanza kuanza zoezi hilo

Tanzania twendapi?

WIKI hii, Ikulu imetangaza orodha ya mabalozi wapya watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali ulimwenguni. Hili ni jambo zuri kwa sababu baadhi ya vituo vilikuwa havina balozi kwa muda mrefu sasa. Ni jambo la heri pia kwamba nchi yetu imetangaza kufungua balozi mpya katika nchi ambazo

Viva Fidel!

HATIMAYE, pazia la maisha ya aliyekuwa kiongozi wa Cuba, Fidel Castro Ruz, limefungwa rasmi. Kama ilivyo kwetu sote, naye amerejea kwa Muumba wake. Usiku wa kuamkia Novemba 26 mwaka huu; majira ya saa 4:29, moyo wa mwanamapinduzi huyu uliacha kupiga na dunia ikawa imempoteza mmoja

Wananchi walindwe mwisho wa mwaka

TOLEO lijalo la gazeti hili litatoka mwezi Desemba mwaka huu. Ni kwa sababu hiyo basi tumeona ni vema tuweke rai yetu mapema kabla mwezi huo haujafika. Kama ilivyo ada duniani kote, siku za mwishoni mwa mwaka watu wengi huzitumia kusafiri kwa ajili ya kupumzika na