Hifadhi: Tahariri

Tanzania twendapi?

WIKI hii, Ikulu imetangaza orodha ya mabalozi wapya watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali ulimwenguni. Hili ni jambo zuri kwa sababu baadhi ya vituo vilikuwa havina balozi kwa muda mrefu sasa. Ni jambo la heri pia kwamba nchi yetu imetangaza kufungua balozi mpya katika nchi ambazo

Viva Fidel!

HATIMAYE, pazia la maisha ya aliyekuwa kiongozi wa Cuba, Fidel Castro Ruz, limefungwa rasmi. Kama ilivyo kwetu sote, naye amerejea kwa Muumba wake. Usiku wa kuamkia Novemba 26 mwaka huu; majira ya saa 4:29, moyo wa mwanamapinduzi huyu uliacha kupiga na dunia ikawa imempoteza mmoja

Wananchi walindwe mwisho wa mwaka

TOLEO lijalo la gazeti hili litatoka mwezi Desemba mwaka huu. Ni kwa sababu hiyo basi tumeona ni vema tuweke rai yetu mapema kabla mwezi huo haujafika. Kama ilivyo ada duniani kote, siku za mwishoni mwa mwaka watu wengi huzitumia kusafiri kwa ajili ya kupumzika na

Tuzijali afya zetu kama tunavyojali mali zetu

WIKI iliyopita, taifa letu limekumbwa na misiba ya viongozi takribani watano waliopoteza maisha katika kipindi cha wiki moja tu. Kwa namna ya kipekee, Raia Mwema linapenda kutoa salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa wote walioguswa na misiba hiyo. Wote waliofariki walipoteza maisha

Mabenki na taasisi za fedha zijitazame

KATIKA mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Rais John Magufuli, aligusia kidogo kuhusu matatizo yanayozikumba baadhi ya benki hapa nchini hivi sasa. Kwa ufupi, Rais alieleza namna baadhi ya benki na taasisi nyingine zilivyokuwa zikifanya biashara katika namna ambayo

Kila la kheri kwa Jenerali Waitara

RAIS John Magufuli wiki iliyopita alimteua Mkuu mstaafu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali George Marwa Waitara, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA). Waitara ambaye rekodi yake ya utumishi jeshini inaonyesha ni mtu mwadilifu na mzalendo, amepewa nafasi hiyo katika wakati

Hii ni hatua muafaka

JUMATATU wiki hii Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ilitoa maelekezo maalumu kwenda katika uongozi wa juu wa taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini kuhusu nia yake ya uhakiki wa wafanyakazi wa kitaaluma katika taasisi hizo. Taarifa hiyo ambayo pia ilisambazwa kwa umma kupitia

Bado tunauana kwa sababu ya Mumiani?

MWISHONI mwa wiki iliyopita, Watanzania walipata habari za kushtusha kuhusu vifo vya watu watatu waliouawa mkoani Dodoma kwa maelezo kuwa walidhaniwa kuwa ni mumiani (wanyonya damu). Waliouawa ni vijana wasomi waliokuwa wameenda mkoani humo kwa ajili ya shughuli za kitafiti ambazo kwa sehemu kubwa zingekuwa