HABARI kutoka Bunge la Jamhuri zinaanza kutia matumaini kwamba wabunge wetu wameanza kushtuka kutokana na masuala kadhaa yanayowakabili, hasa wabunge wa Chama cha Mapinduzi.
Juzi wamekataa kumsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, alipotaka kufanya majumuisho ya semina iliyoitwa kuhusu mswada wa Nishati na Mafuta, wakiitaka Serikali kwanza wajadili masuala nyeti yanayoikabili wizara hiyo.
Aidha Spika wa Bunge, Sam Sitta, ameripotiwa kwamba amesitisha safari yake kwenda Marekani ili aweze kushiriki mjadala wa masuala hayo, ambayo awali alikuwa ameelekeza kwamba naibu wake asiyashughulikie hadi atakaporudi.
Sitta alikuwa amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba Naibu Spika, Anne Makinda, asije ìakakurupukaî kuyafanya masuala hayo yajadiliwe wakati yeye, Spika, hayupo. Sasa tunaambiwa kwamba haendi tena safari hiyo.
Labda huu ni mwanzo mzuri. Kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakiliangalia Bunge la Jamhuri kama mwendelezo wa chama tawala na Serikali yake, chombo cha kupiga mhuri kwa kila jambo inalotaka Serikali, liwe na manufaa kwa wananchi au la.
Kisingizio kimekuwa kwamba kutokubaliana na Serikali ni sawa na kuungana na Upinzani na kupunguza imani ya wananchi kwa serikali yao.
Sasa wabunge wa CCM wanaelekea kutambua kwamba wanapoteza heshima yao mbele ya raia wa nchi hii kwa kukaa kimya wakati mambo yanakwenda mrama, na hawako tayari tena kutumiwa kama mhuri.
Wanataka taarifa timilifu za masuala mazito ili wayajadili kwa kina, na hawako tayari kufumbwa macho na mawaziri wa Serikali. Mungu atupe nini?
Si tumeona jinsi ambavyo masuala mazito yanavyofunikizwa hadharani kwa wabunge wa chama tawala kujifanya ni sehemu ya Serikali badala ya kuwa sehemu ya uwakilishi wa wananchi?
Mfano mzuri ni wakati mbunge wa CHADEMA, Zitto Kabwe alipoleta hoja yake Bungeni kuhusu ëmkataba wa Buzwagií na wabunge wa CCM wakachachamaa kuivunja miguu hoja yake, kana kwamba Serikali haikuwa na mawaziri wa kutosha bungeni kuitetea.
Hivi, serikali yenye wabunge zaidi ya 60 ambao ni mawaziri inahitaji utetezi wa wabunge wengine? Hao 60 wanalipwa kufanya nini hasa?
Matokeo yake ni kwamba wabunge wa CCM wamempa Zitto umaarufu ambao labda hata yeye umemshangaza, kwa sababu hakuutaraji. Watu ambao hata yeye hakuutaraji. Wengi nchini wameliona Bunge lao kama haliwawakilishi bali linawakilisha maslahi ya watawala. Kama wabunge wa CCM wamelitambua hilo watakuwa wamepiga hatua muhimu katika kuimarisha sauti ya wananchi, na wanastahili pongezi.
Pia ni jambo jema kwamba Spika ameamua kufuta au kuahirisha safari yake ili asimamie mjadala huu muhimu. Haiyumkiniki kwamba wakati kuna jambo muhimu ambalo linahusu maisha ya Taifa letu bungeni, Spika anaondoka zake, kisha anamwambia msaidizi wake mkuu ëasikurupukeí kuendesha mjadala kwa niaba yake, kana kwamba msaidizi wake huyo ana tabia ya ëkukurupuka.í Angalau tushukuru kwamba na Spika naye amengíamua kwamba mjadala huu ni muhimu kuliko safari za ughaibuni. Sasa, twende kazini.
Bado kuna shaka kuhusu hatua ya Waziri Mkuu kuitisha ëcaucusí ya wabunge wa CCM (jana) kujadili masuala yanayohusu Benki Kuu na mkataba tata wa Richmond.
Punde tutajua nini kilitetwa katika mkutano huo, lakini isije ikawa mkutano huo uliitishwa ili kuwafunga midomo wabunge wa CCM. Wabunge hao wakikubali kufungwa gavana ili wasiisemee shauku ya wananchi, watakuwa wamekataa nini, wamekubali nini? Yatakuwa ni yale yale.
Ncheme nchicheme? Kama ningeweja kuchema ningechema hivi: Karamagi angemchaidia Laichi wake kwa kuchema bachi, naachia ngaji, kwani nini?
Toa maoni yako