KWA nini tunazungusha maneno? Tuseme ukweli tu kwamba endapo Muungano utavunjika wa kulaumiwa si Wazanzibari bali ni Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimeshindwa kuonyesha uwezo wa kuutetea Muungano kwa hoja maridhawa na mikakati ya makusudi na badala yake kuendeleza imani ya kuzima hoja za kupinga Muungano kwa mtutu wa bunduki, vitisho, na mabavu.
Ni wakati wa utengano sasa
Tanzania kama nchi ina mambo mengi sana ya kuhangaika nayo ili kuweza kuwainua watu wake kutoka katika laana ya umasikini wa kudumu. Tuna mambo mengi ya kufanya ili kuweza kuwaongoza watu wetu kuelekea uhuru wa kiuchumi na maendeleo yenye kutoa nafasi kwa kila mtu kufanikiwa.
Haiwezekani katika wakati kama huu tuanze kuhangaika na utetezi wa Muungano. Suala la Muungano lilitakiwa liwe limemalizwa miaka 20 iliyopita. Kutokana udhaifu na uongozi mbovu wa CCM leo hii tumefika kwenye ukingo wa kutengana (a precipice of separation).
CCM wameshatuonyesha kuwa hawawezi kuutetea Muungano; hakuna kiongozi yeyote wa CCM mwenye uwezo tena wa kusimama kuutetea Muungano. Si wazee wao na wala si vijana wao; si wasomi wao na wala si wanaharakati wao; si wa Bara na wala si wa Visiwani.
Hakuna mteteziwa Muungano. Si Salim, wala si Bilal; si Makamba na kwa hakika wala si Kikwete. Tusiwaangalie kina Mkapa wala Sumaye kuutetea Muungano. CCM imepoteza ujasiri wa kuutetea Muungano, sasa kwanini tusiseme ukweli?
Huu ni wakati wa kutengana ili kuwe na mataifa mawili yaliyo huru na yenye kuhusiana kama vile mataifa mbalimbali yanavyohusiana duniani kwa kutumia mikataba na nyezo mbalimbali za kimataifa.
Kushindwa kutatua kero za muda mrefu kumetufikisha hapa
Ni lazima tuseme ukweli na ukweli ujulikane. Yanayotokea sasa hayakupaswa kutokea kama viongozi wetu wangeonyesha uwezo wa kuyamaliza matatizo ya ‘kero’ za Muungano.
Ndugu zangu kushindwa kutatuliwa kwa haya kumegeuza kero hizi kuwa ‘matatizo sugu’ ya Muungano. Yaani, ni matatizo yaliyoshindikana. Kwa vile yameshindikana kutatuliwa kwa muda wa miaka hii 50 wakati umefika sasa wa kukubali kushindwa na kusalimu amri kuuachilia Muungano.
Matatizo haya sugu yameonyesha na kudhihirisha pasi ya shaka kikomo cha uwezo wa viongozi wetu. Si mzee Mwinyi wala Mkapa waliokuwa na uwezo wa kuonyesha utatuzi wa matatizo ya Muungano. Kikwete ambaye aliingia kwa ahadi motomoto amethibitisha kuwa na yeye (pamoja na utawala wake wote) hana uwezo wa kutatua matatizo haya sugu.
Ni nani aliyesahau maneno ya kutia moyo ya Rais Kikwete kwenye Bunge la Muungano baada ya kuapishwa kuwa Rais na akilizindua Bunge hilo Desemba 2005?
Ni yeye aliyesema maneno haya “Tunalo jukumu la kihistoria la kuhakikisha kuwa Muungano wetu unadumu na unazidi kuimarika. Nafurahi kusema kuwa Muungano wetu ni imara licha ya changamoto za hapa na pale. Na, kinachonipa faraja zaidi ni ule ukweli kwamba pande zetu zote mbili za Muungano zinayo dhamira ya dhati ya kutatua kero zilizopo kwa lengo la kuuimarisha.”
Miaka sita baada ya maneno haya Muungano wetu ni dhaifu na ‘changamoto za hapa na pale’ zimekuwa matatizo ya kudumu! Kikwete naye kashindwa!
Wanaeneza chuki dhidi ya Wakristu na Watanganyika
Ieleweke kwamba wanaopiga vita Muungano kimsingi kabisa wana tatizo na Wakristu na watu wenye asili ya Bara na hasa wale ambao wanatoka Bara yaani Watanganyika. Baadhi ya viongozi wa mihadhara hii wanatoa kauli ambazo mtu wa kawaida anazichukulia kama kibali na wito wa kuwatendea uovu watu wa Tanganyika.
Maana, kama Watanganyika ndio wanawadhulumu Wazanzibar na Watanganyika hawa wako Zanzibar je si haki kwa Wazanzibari kuwatendea vibaya wadhalimu wao? Maana, kama ni kweli Tanganyika inaikalia Zanzibar kama koloni lake si haki kwa wanaotawaliwa kimabavu na Watanganyika kuinuka dhidi ya Watanganyika?
Na cha kushangaza zaidi (na kuudhi) serikali yao nayo inakuwa kimya kwa vitendo hivi. Hivi makanisa yameanza wiki hii kuchomwa Zanzibar? Hivi baa zimeanza juzi kuchomwa huko Zanzibar au ni kwamba watu wana usahaulifu wa ghafla?
Taarifa iliyotolewa juzi ya kuwahakikishia “watalii” kuwa hali ni shwari haikutaja kabisa kuhusu watu wa Bara ambao siku ya Jumatatu wamekuta vipeperushi vikiwataka waondoke Zanzibar. Hii si mara ya kwanza kwa vipeperushi vya aina hiyo kutokea Zanzibar na inathibitisha kushindwa kwa mfumo wa inteligensia wa nchi yetu!
Lakini Wakristu wa Zanzibar wamekosea nini? Hivi ni kweli wanataka Wakristu wawe wale waliozaliwa Zanzibar tu na wengine wakija na kuhamia huko ni makosa? Kama alivyosema Sheikh Fared mwezi Machi, kama mtu hajakutangazia uadui wowote wala kukuinulia silaha dhidi yako iweje wewe umtangaze adui?
Muda wote makanisa yanapochomwa Zanzibar haijatokea mwendawazimu hata mmoja kufikiria kuchoma msikiti; hivi kweli akatokea mtu wa aina hiyo si ndiyo vita dhidi ya Wakristu itatangazwa?
Tena utaona haihitajiki hata Mkristu kufanya hivyo kwani muhuni mwingine akiamua kuwakorofisha Waislamu kwa kuchoma Msikiti (akijua watalaumiwa Wakristu au Watanganyika) si ndio hawa watoa mihadhara watatangaza vita ya kudumu?
Sasa, hili lazima lidaiwe kwa hawa viongozi – kama hawataki Wakristu Zanzibar kabisa watamke wazi ili Wakristu waondoke Zanzibar kwa amani! Kama wanaitaka Zanzibar ambayo haina dalili ya Ukristu kwa sababu Waislamu ni wengi waseme hivyo badala ya kuwachomea watu makanisa yao na kutishia maisha ya watu.
Ninasema hili nikiamini ya kwamba vitendo vya kuchomewa makanisa na kutishiwa Watanganyika vimevumuliwa mno na havijakemewa kwa uzito unaostahili. Hatujawasikia Wazanzibari maarufu kama kina Dk. Salim, Mzee Mwinyi, Dk. Bilal na wengine kutoa kauli za kuwalinda Wakristu na Watanganyika hawa. Wao wako kimya. Ina maana gani? Hatujawaona hata mmoja wao kutembelea nyumba hizi za Ibada za Wakristu zilizoteketezwa tangia Januari mwaka huu? Wanaogopa nini?
Tuuvunje Muungano vizuri
Kwa watu wanaosoma makala zangu watatambua kuwa msimamo wangu huu wa leo si mgeni. Aprili 27, 2011 niandika makala kwenye gazeti hili toleo la 183 yenye kichwa cha habari “Muungano wetu hauna watetezi tujiandae kuuvunja vizuri”.
Hata hivyo hiyo ilikuwa ni hitimisho la hoja niliyoijenga mwaka mmoja nyuma. Niliandika katika toleo la 147 Augosti 2010 katika makala yenye kichwa cha habari “Wanalivunja Taifa kwa kisingizo cha ‘kuimarisha Muungano’”.
Makala zote zilikuwa zinaonyesha tu kuwa Muungano wetu umefikia mahali tukubali tuuvunje ili tuhusiane kama nchi mbili. Wazanzibari ambao tokea mwanzo lengo lilikuwa ni nchi tumeshawakubalia mengi sana.
Tangu mwanzo wameachwa kuwa Zanzibar bila kulazimishwa kupotea kabisa lakini wanataka zaidi. Sasa Serikali ya CCM imewapa hivi vyote, bendera, wimbo wa taifa, rais wake, baraza lake la mawaziri, bunge lake, vikosi vyake mbalimbali sasa leo wanataka nchi yao tunawakatalia? Kwa vipi tunaweza kuwakatalia?
Hivi mtu kila siku anadai umpe meza, anadai apewe viti na makochi, anadai makabati na mapambano ya ndani, mara anakuja na kudai ukingo wa nyumba na vyote hivyo anapewa leo anaamua kudai nyumba tunashtuka? Hivi tulifikiria hizo meza na makabati alikuwa ayaweke chini ya mwembe?
Tayari CCM imeshakubali kuipa Zanzibar vyote vinavyohitajika kwa nchi, sasa wakati umefika kwa Zanzibar kuwa nchi; watoke kwenye Muungano.
Kwa vile kama nilivyosema mwaka mmoja uliopita, kuwa Muungano wetu hauna watetezi basi mimi nimejichagua kuwa mtetezi wa kuvunja Muungano. Tuuvunje ili tuwe salama.
Bado ninaamini katika umoja wa Afrika kama kanuni ya msingi iliyozaa Tanzania na bado ninaamini ni katika umoja tu vi-nchi vyetu hivi vitaweza kufanikiwa lakini umoja huu kama wa Wazanzibari hatuutaki. Wakati umefika kwa watu wa Bara nao kuanza kujitokeza na kufanya makongamano na maandamano ya kuukataa Muungano.
Si kwa sababu Zanzibar wanatuonea au wanaweza kufanya lolote dhidi ya Tanganyika – hawawezi – bali ni kwa sababu hatutaki kama watu wa Bara kutembea na hatia kuwa tunawaonea Wazanzibari!
Hatutaki kuishi na kujihisi kama wakoloni wakati hakuna lolote ambalo Wazanzibari wanalifanya au kutolifanya linalotudhuru sisi au hata kutuongezea lolote sisi.
Tanzania Bara haiitegemei Zanzibar kwa lolote bali Zanzibar inaitegemea na itaendelea kuitegemea Tanzania Bara! Sasa kama hili ni kweli – na ni kweli – basi Zanzibar iachwe iwe. Mwanafunzi yeyote wa historia anajua kabisa nini kitatokea tena Zanzibar.
Kwa vile CCM na Serikali zake wameshindwa kuutetea Muungano na kutatua matatizo ya Muungano, wakati umefika wa kuiachilia Zanzibar iende.
Tuwaache Wazanzibari waende na warudi kwenye nchi yao yaishe kwa amani. Tunawapenda sana Wazanzibari kiasi kwamba hatuwezi kuwang’ang’ania! Wanataka kwenda waachwe waende. Hadi kitakapokuja kizazi kitakachowahukumu wanasiasa na viongozi uchwara wa dini ambao wanapenda migongano kuliko umoja, chuki kuliko upendo, vurugu kuliko amani. Hawa wanaosimama kutaka kulivunja taifa kipo kizazi kitawahukumu vikali.
Kwa sisi wengine tunasema let Zanzibar go!
Maoni ya Wasomaji
Ulichoandikwa ni ukweli
Ulichoandikwa ni ukweli usiopendwa na wanafiki wa ccm! Let them go!
Badala yakumalizia let Zanzibar go, ungestahili Muandishi kumalizia makala yako kwa let Zanzibar go to hell. Kwani inaonyesha umekunywa shubiri wakati ulipoiandika. Tunakumbuka wito wa let my peole go unaoashiria wito waukombozi. Wewe unayatumia maneno hayo kuwatabiria Wazanzibari giza usoni. Isitoshe unanukia ubeberu. Nakumbuka siku zile zakupigania uhuru wale waliokuwa hawajiamini walikuwa wakiuliza, kwa kejeli, ikiwa shindano hatuwezi kutengeneza, vipi tutaendesha nchi. Uhuru umepatikana na nchi inasota. Kusota huku ni chaguo letu kuwarejesha kila uchaguzi wale wale waliotufikisha hapa. Ungelibakia na hoja yako nzito kuwa yote haya yametokea kwa sababu ya Utawala wa CCM kushindwa kutatua tofauti zilizokuweko hadi leo hii kufikia matatizo sugu basi ungenituliza. Bahati mbaya matokeo unayachanganya na sababu. Tunajua sote ujirani na nchi kubwa ni matatizo. Mkiwa marafiki na dola kubwa basi inatarajia siku zote siasa zake uzikubali. Mkitofautiana nayo basi mtakiona cha mtema kuni. Sitaki kukumbusha ya Kina na Vietnam. Kwa nini umepuuza moja kwa moja kuzingatia ile fikira asili ya Mwalimu Nyerere? Kwani Zanzibar inaweza kujiunga katika Umoja wa Afrika Mashariki na kuendelea na maingiliano si na Tanganyika tu bali na majirani wengine vile vile. Tanganyika itabakia kaka. Sina nia yakuandika barua ndefu lakini nitachukua fursa hii kukupongeza kuyakumbuka yafuatayo:
Kama alivyosema Sheikh Fared mwezi Machi, kama mtu hajakutangazia uadui wowote wala kukuinulia silaha dhidi yako iweje wewe umtangaze adui?
If they don't see our
If they don't see our impontance let them go. They have been mis treated by CCM regime and if they demand autonomy let them go. The unite is a democratic phenomena and if the Most of them don't want to work and b'se they are promise with a good future after separation let them go. Let us also say openly we don't want them, in short we're fed up with this useless Union. They are promised good future from Oman and Soudia (UAE) let them unite with their fellow Arabs so that they can enjoy OIC. We can't work together to accamplish our common goals if are not in harmony, if we don't true cohession . Let the Union fall a part (Go) and hopefull Tanganyika will arise as agreat Nation in the universe b'se of we're endowered with all necessary condition to be great Nation . Watanagnyika tutamke wazi na tutende wazi kuwa hatuutaki Muungano ili Muungano ufe na haki itendeke tusonge mbele kama Taifa.
Mwandishi umeandika ukweli
Mwandishi umeandika ukweli kabisa lkn watu wenye madaraka wamefumba macho na masikio.Ila kuongezea tuu nataka mufahamu uchomaji wa Makanisa ischuliwe kua ni UISLAMU bali ni watu au kikundi fulani ndicho kilichohusika na Uhuni huu.Kuhusu Muungano wacha uende maana walio uanzisha huu Mvurugano wote hawapo tena duniani.Kwa usalama wa kila mtu tunaomba Muungano U V U N J W E E E!
Sioni manufaa yoyote kwa wananchi husika,wanaofaidika ni viongozi pekee yao
Let all that has been said be
Let all that has been said be done the region will witness an everlasting peace and tranquility. Wengi wetu wameshatoa option ya decent exit kupitia opinion polls lakini naona wenzetu are getting particularly jittery and restless. They cannot wait. Fine. Sisi tunashirikiana na kuwalea wanafiki kwa nusu karne and yet there is no visible appreciation of the sacrifices and the humiliation which Tanganyika has suffered throughout the period. Let them go tena tuwafungie huko huko kabisa wasirudi huku kuja kututemebelea. Umeme kutoka Bagamoyo tunaweka meta mpya ya kulipia kwa dola, tena at full tariff! Watakapoanza kutembezeana majambia tuwatumie tu salaam za rambirambi. Enough is enough!
Na mimi naungana na maneno
Na mimi naungana na maneno yako japo kuna baadhi ya sehemu umepotosha " Let us go", tuacheni tupumuweee, Muungano hatuutaki. Na tunaona nyinyi Watanganyika ndio munaotuchereweshea huu muungano kuvunjika mumetuwekea vibaraka wenu akina Abood, kwa ajili ya kulinga muungano usiokuwa na mantiki, hata layman anajuwa kuwa muungano huu ni ujanja wa kuikalia Zanzibar kimabavu.
Tanganyika ni wakoloni hata kuliko wareno na wajerumani
Mwandishi eme- exhaust!! na
Mwandishi eme- exhaust!! na huo ndio ukweli asioutaka basi.
Dhana nzima ya ukoloni si jambo la starehe, au la kitalii, au la kujifurahisha tu. Ukoloni siku zote una economic interests either short term au long term!
Sasa sijui Tanganyika ina interest gani Zanzibar hadi iitwe majina haya yote.
Zanzibar hakuna chochote cha kufaidi economically......... zaidi ya kuwa sehemu ya cultural tourism.
Hawa watu waachwe waende zao tena haraka sana..... hatuwataki!!!!!!!!
Tabia hujenga Mazowea,kwa
Tabia hujenga Mazowea,kwa wale wenye vyombo vya Habari wao wamezowea kutumia kalamu zao kwa kuwakandamiza wengine na kwa sababu hao wanaokandamizwa hawana sauti kwa sababu madia zote ni zao basi haki ya kuhukumu iko kwao.
KamaINGEKUWAwanatumia HAKI basi wasingetoa hukumu kuwa waliofanya hujuma hizi ni WAISLAMU , bali wangeliachia nafasi ya Uchunguzi na kama HAKI haikutendeka ndio waseme.
Uzoefu ulipo Visiwani sote tunaujuwa wako watu ni kazi yao FITNA ,CHUKI, NA UONEVU wamakusudi, wakimaliza kufanya hayo huwa wamewasha moto wako pembeni kusubiri Matokeo.
Inawezekana kuwa watu walihamasishwa kutenda maovu. Lakini pia wako wanaofanya maovu ilikusingizia jamii Fulani kuwa ni wao waliofanya kwa kutimiza malengo yao na chuki zao dhidi ya wengine
Ndpo niliposema Waachiwe Polisi na vyombo husika kuna siri kubwa imejificha chini ya kiza kinene , na hii sio mara ya kwanza kwa watu hawa kufanya hivyo ilikushibisha Shahawa zao,
Nawasilisha
Huo ni ukweli amabao uko wazi
Huo ni ukweli amabao uko wazi kwa Sasa chama Tawala CCM hakikiko katika nafasi ya kutatua matatizo yoyote ya Watanzania sio swala la muungano tu bali mambo mengi.Mambo ambayo yanataka utatuzi wa haraka wanakaa kupiga soga za usanii na kuunda kamati zisizokua na kichwa wala miguu ambazo zinatumia pesa zetu nyingi za walipakodi.Huwezi kua na nia nzuri ya kuatatua matatizo ya muungano wakati unapotokea mwanya wa kujadili mapungufu ya muungana mfano katika rasimu marekebisho ya katiba chama tawala CCM na serikali kinakua mstari wa mbele kusema ya kua swala la muungano lisiguswe!!!?Ssasa hizo kamati au tume zinajadili nini kama swala la muungano halipashwi kuguswa??????!!!!Ni usanii amabao madhara yake tumeanza kuyaona.Pia naungana na Zitto kuhusu swala la mafuta na gesi badala ya kulitafutia ufumbuzi na kuwapa mazingara mazuri wafadhil kuanza mara moja utafutaji wa mafuta na gesi tunaendelea na ngonjela zisizo na kichwa wala miguu.Matatizo yote haya ni CCM chama ambacho kimepooza ubongo na kinaona mwisho wake,hivyo hakioni sababu ya kuchukua maamuzi yoyote ya maana kwani kinajua hakitabaki madarakani.Hii ni hatari!Kwani kikotayari kuhujumu na kufanya kila kitu ili wale watakaokirithi wapate muda mgumu wa wapi pa kuanzia.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Mimi nadhani muungano ndio
Mimi nadhani muungano ndio unaishia. Kama ni hivyo, kuna masuala muhimu yatafuata na ni vizuri kuanza kujiandaa. Isije ikawa ghafla na mambo mengine yakafanyika kwa jazba. Kwa mfano, nini kifanyike kuhusu raia wa kila upande walioko upande mwingine baada ya muungano ku-expire? Ndio ku expire maana muda wake utakuwa umeisha! Je itabidi kila sehemu ichukue watu wake? Au itabidi waachiwe waamue watakuwa raia wa nchi gani? Hili la pili binafsi silipendi. Lakini kuna watu wameoa/olewa upande wa pili. Watoto watakuwa raia wa nchi gani? Watafuata kwa nani? Baba au mama? Wazo la kuwa na sarafu moja, passport moja na vitu kama hivyo itakuwa sawa na kuwa na serikali moja. Itabidi tushirikiane kama tunavyoshirikiana na Kenya, Ugand na nchi nyingine za Jumuia ya Afrika Mashariki. Kuna zoezi la vitambulisho linaendelea. Labda lingesitishwa ili dhoruba hii ya muungano ipite. Tusije tukawapa vitambambulisho raia wa nchi nyingine!
Mimi kama Mzanzibari mzalendo
Mimi kama Mzanzibari mzalendo naunga mkono mia kwa mia hoja ya muandishi ya kutaka wakoloni wakitanganyika kutupa UHURU wetu. Tuatafurahi sana.
Tanganyika wanasema hawapataki kitu Zanzibar. Sio kweli,hata Nyerer alisema waziwazi kuwa kama angelikuwa na uwezo angekisukuma kisiwa cha Zanzibar mbali?
Wazanzibari hawauwogopi Ukiristokwani ulianza Zanzibar kabla ya kuja Bara. Visiwani ulishindwa. Mreno alifikia hata kuuwa watu ili wabadili dini lakini hawakufuzu. Sasa Tanganyika na Kanisa baada ya kuona si rahisi kuikafirisha Zanzibar wakaja na mbinu za kuwaleta wakiristo Zanzibar kama njia ya upanuzi wao. Wakaitumia CCM kutunga sheria kuwa Mtanganyika atakekaa Zanzibar kwa zaidi ya miaka 10 mfululizo anaweza kuwa Mzanzibari. Maana yake hata jambazi likikaa miaka 10 litakuwa Mzanzibari
Wazanzibari wameliona hili na katu hawakubali liendelee. Hakuna mtu mwenye chuki na Watanganyika lakini silka inatuzuia kuwa naushirikaino na nyinyi.
Sawa baada ya kuumaliza utajiri wetu wa Karafuu sasa eti mnasema hatuwezi kuishi. Mbona yale mafuta yetu hamtaki kutuachia?
Tanganyika kwa Zanzibar ni mkoloni na lazima aondoke. Kama tuliwapinduwa watu waliokuja kutusaidia kumuuondoa utawala wa kidhalimu wa Kireno tutashindwaje kuwafukuza watanganyika Zanzibar?
Zanzibar na watu wake wamefikia pahala hata kupoteza heshima yao. Leo ukienda nje ukitaja tu umetoka Tanzania basi kila mmoja anaanza kuficha mali zake na hata watoto kuogopa kuchunwa ngozi.
Fikiria hawa maaskofu kmakwao wapi. Si wanatoka kwenye jamii ya kuchuna ngozi watu na kukata viungo Maalbino?
Hivi Zanzibar hakuna viongozi wa kidini ya wakiristo mpaka watoke Bara? au mambo ya dini na Imani yameshaingizwa kinyemela kwenye mambo ya muungano?
WATANGANYIKA TUPENI NCHI YETU HARAKA SANA
Napingana na mwandishi.
Napingana na mwandishi. Wazanzibari na watanganyika ni ndugu wa damu, panapotokea kutokuelewana basi tukae pamoja kusuluhisha. Hata ndugu wa familia moja huwa wanagombana, basi sembuse sisi? la muhimu ni kukaa na kusuluhisha, nashauri suluhisho kubwa na la mwisho kabisa ni kuunda SERIKALI MOJA ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kusiwe na SMZ wala serikali ya Tanganyika hili ndio suluhisho la pekee na maridhawa kabisa. Wazaanzibari wabaki kama wachaga, wamanyema, wasukuma, wanyamwezi kwa sababu wazanzibari wakiachwa peke yao basi hatima yao itakuwa si nzuri watapigana tu, sasa kama mnataka wapigane basi vunjeni muungano muone.
Maelezo uliyayatoa kuhusu
Maelezo uliyayatoa kuhusu Muungano,mimi nakubaliana nayo kwa asilimia 100. Wacha waende.
Kwanza Wazanzibar itakuwa hasara kwao kuvunjika kwa muungano. Nasema hivyo kwa sababu wao ndiyo wapo wengi huku bara ukilinganisha na Watu wa huku bara. Pia ni wategemezi wakubwa wa chakula kutoka bara,wanategea umeme kutoka bara na mambo mengineyo. Kujitenga kwao watatupa nafasi wabara kufanya biashara nzuri kati ya Nchi na Nchi.
Wacha waende.
Watanganyika tuacheni haraka
Watanganyika tuacheni haraka iwezekanavyo na haina haja ya kutumia mabavu yenu , kutumia jeshi na polisi kuwapiga watu wanapodai uhuru wao, kwa usalama tukiachana tutakuza hasa ushirikiano hapo baadae.
Miungano namna hii mingi ilivunjika na muungano wa kijinga kama huu wetu haukutokea duniani. Muungano ambao unaweza ukadumu na hata ukawashawishi hata nchi za jirani kujiunga ni hule wa nmna ya munngano wa nchi za ulaya za magharibi. Aina yeyote nyingine sisi wazanzibari tutaendelea kuupinga mpaka uvunjike. Kama alivyosema mhariri wa mada hii ni kura ya maoni ndiyo itakayotuachisha kwa njia ya usalama, kwani sote huku visiwani tutaukataa muungano huu na kusababisha kurudisha utaifa wa Tanganyika na Zanzibar.
<p>Vurugu za zanzibar
Makala inagusa sana hisia.
Makala inagusa sana hisia. Kweli wacha waende, kama mambo yenyewe ndo hayo!
Nakupongeza kwa Makala yako
Nakupongeza kwa Makala yako nzuri. Ila ninapata shida kuamini kuwa suluhisho pekee la matatizo ya muungano wetu ni kuuvunja, kama vile kwa kufanya hivyo nchi yetu itakuwa imara katika suala zima la amani, umoja na maendeleo. Katika makala yako umeeleza vizuri kabisa kuwa tatizo la muungano ni viongozi wetu ambao si tu wameshindwa kuboresha maisha ya watanzania bali pia wameshindwa kushughulikia kero mbali mbali za muungano, kama ndivyo hivyo hata kama tukivunja muungano viongozi watakuwa ni wale wale na matatizo bado yataendelea kuwepo nje ya muungano. Kwa mantiki hii, hapa tatizo si muungano ni viongozi tulionao. Kama hizi kero zingekuwa zinafanyiwa kazi ipasavyo na kwa wakati sidhani kama leo hii tungekuwa tunaongea kuhusu suala hili la muungano. Ni kama mahusiano ya watu wawili, ambayo kuna kuhitilafiana, kukwaruzana, kutukanana na hata kupigana lakini baadae kuna kukalishana chini kutafuta suluhu na hatimaye kupatana na mambo kwenda kama kawaida. Katika hali kama hii ukiniambia kuvunja uhusiano ndio njia pekee kwa vile mpatanishi wao hana weledi wa kutosha kufanya shughuli hiyo nafikiri utakuwa huwatendei haki wawili hawa. Vivo hivyo katika huu muungano wetu, hebu tuwashirikishe wananchi kutafuta suluhu ya hizi kelo mbali mbali zinazoukabili kabla ya kufikiria kuuvunja na kama tatizo ni viongozi, 2015 sio mbali. Tutumie kura zetu vizuri kuleta mabadiliko ya kiuongozi. Tuchague viongozi ambao watakuwa ni chachu ya amani, umoja na maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.
Let them (Zanzibaris) go to
Let them (Zanzibaris) go to hell in peace.
Wasirudi na mitumbwi Dar kuja kuhemea, waondoke jumle and they should'nt turn their backs to us for any kind of help. Wang'oe kila kilicho chao watokomee kuzimu tumechoshwa na vitisho vya nyau. Aliyezoea mijeledi hawezi ishi kwa ngumi hadi last blow uwe mjeledi. Wamezoea utumwa waacheni waende kwa waarabu wakawe watumwa huko, mnawa bembeleza wa nini. Do we have anything to loose???